20 September 2011

CHANETA, CHANEZA zajiandaa na Olimpiki

Na Mwandishi Wetu

VYAMA vya Netiboli Tanzania Bara (CHANETA) na Zanzibar (CHANEZA), vinaanza mchakato wa michuano ya Olimpiki kwa netiboli itakayofanyika mwakani
London, Uingereza.

Taifa Queens tayari imefuzu moja kwa moja kushiriki michuano ya Olimpiki, baada ya kunyakua medali ya fedha katika michuano ya Mataifa ya Afrika iliyomalizika Maputo, Msumbiji wiki iliyopita.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Bayi alisema wamevunja kambi ya timu hiyo ya taifa, ili kupisha wachezaji kupata mapumziko mafupi, wao waendelee na maandalizi ya Olimpiki yatakayofanyika mwakani.

"Kambi ya Taifa Queens, tunaivunja ili kila mchezaji apate mapumziko kutokana na kazi kubwa walioifanya Maputo, hasa ukizingatia kuwa timu yetu inaundwa na wachezaji wa Bara na Zanzibar," alisema Bayi.

Taifa Queens ndiyo pekee waliotwaa medali katika michuano ya mataifa ya Afrika, licha ya Tanzania kuwakilishwa na timu sita za michezo tofauti.

No comments:

Post a Comment