15 September 2011
Polisi waua Geita wakizuia maandamano
*Yalifanywa kupinga M/kiti Geita kung'olewa
*Madiwani CCM nao watwangane makonde Kahama
Na Faida Muyomba, Geita
VURUGU kubwa zimetokea Kata ya Nkome wilayani Geita, ambapo mtu mmoja ameuawa kwa
kupigwa risasi, huku wengine watatu wakiwemo polisi wawili kujeruhiwa,katika mapambano ya polisi na wananchi waliokuwa wakipinga kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Katika vurugu hizo zilizotokea jana pia Mkuu wa polisi wilayani Geita, Bw. Kasagabo alitekwa kwa muda wakati akiwa katika kituo kidogo cha polisi cha Nkome, alikokwenda kwa lengo la kutuliza ghasia.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, walisema lilianza baada ya viongozi kadhaa wa vyama vya CUF na CCM, kupita mitaani wakiwa na matarumbeta wakiwahamasisha kufanya maandamano kupinga kuenguliwa madarakani kwa aliyekuwa mwenyekiti wa Halmashauri Bw.Joseph Msukuma.
Bw.Msukuma juzi alipigiwa kura ya kuondolewa madarakani na madiwani wakimtuhumu kwa uongozi mbaya, utovu wa nidhamu na kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Aliyefariki kutokana na tukio hilo ni Bw. Abdallah Kikundi (37) mfuasi wa
Chama cha Wananchi (CUF), ambaye alipoteza maisha akipelekwa hospitali kwa matibabu baada ya kupigwa risasi kichwani.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Geita, Dkt. Patrick
Bulugu, aliwaambia waandishi habari hospitalini hapo kuwa kifo hicho kilitokana na jeraha la risasi kichwani.
Akithibitisha tukio hilo kwa njia ya simu, Kaimu Kamanda wa polisi,mkoani Mwanza, Bw.Deusdedith Nsimeki,alisema lilitokea jana mchana ambapo kundi kubwa la watu zaidi ya 3,000 lilifanya maandamano yasiyo halali kinyume cha sheria.
Alisema watu hao mbali ya kutaka kuchoma ofisi ya ofisa mtendaji wa kata na ile ya diwani, pia walikizunguka kituo cha polisi kilichopo eneo hilo, ambapo polisi wakiongozwa na mkuu wa polisi wilaya waliwakamata baadhi ya watuhumiwa huku wengine wakirusha mawe na kumzingira OCD.
Alisema askari wawili waliokuwa
wameteremka kuyatoa njiani mawe hayo alipigwa jiwe mgongoni na kuanguka huku jingine likimpata mwenzake na ndipo polisi walijiokoa kwa kupiga risasi hewani.
Alisema katika purukushani hizo, risasi moja ilimpiga mtu aliyeuawa kisogoni na mwenzake Bw. Elikana alipigwa katika mkono wake wa kulia.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Geita, Bw.Philemon Shelutete
alisema kamwe hawatakubali amani
kuvunjwa kutokana na maslahi ya watu wachache.
Naye Patrick Mabula anaripoti kuwa madiwani wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kahama wamerushiana makonde baada ya kutofautiana katika suala la kuchangia maendeleo katika kata zao.
Madiwani hao Bw. Emmanuel Makashi ( CCM ) wa Kata ya Sabasabini na Bw. Joseph Masaluta (CCM )wa Kata ya Bulungwa walipigana kutokana kuhusu uchangiaji wa maendeleo katika Kata ya Bulungwa.
Wananchi hao walisema siku hiyo Diwani wa Kata ya Saba sabini Bw. Makashi alikwenda
nyumbani kwa Bw.Masaluta anayeishi kijiji cha mseki na kumtaka afute kauli yake
unayomzuia mtu mmoja mmoja kuchangia maendeleo akitaka michango ikusanywe kutoka katika ushuru wa vyama vya msingi vya tumbaku.
Bw.Makashi akiwa na Mtendaji wa Kata ya Bulungwa Bw.Christopher Lyogero walipofika
hapo Bw.Masaluta aligoma kufuta kauli yake ambayo kama maelekezo namna ya wananchi watakavyochangia michango yao ya maendeleo kutoka katika vyama vya msingi vya tumbaku ambavyo huwakata ushuru.
Wakiwa nyumbani hapo ghafla Diwani wa Saba sabini alimvamia Bw.Masaluta na kuanza
ugomvi ulioamuliwa na Mtendaji wa kata ya Bulungwa ambaye amekiri kutokea kwa ugomvi
huo nyumbani kwa Diwani.
Diwani wa Kata ya Saba sabini Bw.Makashi alipoulizwa na mwandishi wa habari hizi
alikiri kupigana na kusema ugomvi huo ulitokana na tofauti za kiutendaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Suala la polisi kuua watu linapigiwa kelele kila siku na serikali inaona kama movie,siku moja tukiwachoka patachimbika kiasi cha kutosha
ReplyDeleteipo siku tutapata uhuru wetu tu hata kama itakuwa kwa mtutu wa bunduki hatutaogopa
ReplyDeleteKuliko ukutane na Polisi wa sasa hivi ni bure ukutane na simba. Polisi ni wale wa enzi ya Nyerere wa sasa hivi wako kimaslahi zaidi. Tunadanganywa Polisi hawaruhusiwi kujiingiza kwenye vyama vya siasa lakini Polisi wa sasa hivi wanalinda maslahi ya CCM.
ReplyDeletePolisi hawasaidii chochote ni wala rushwa kamanini ukiwa na tatizo mpaka utoe hela ndo washughulikie lalamiko lako, bila hivyo hakuna msaada wowote.
ReplyDeletehakuna polisi bali wasanii ambao hawajui fani.wapo alimrad jina liko kwenye payroll ya mwisho wa mwezi.hakuna polisi hata wa dawa,hakuna tujilinde wenyewe!!
ReplyDelete