*Awatwisha zigo vigogo wa siasa vurugu Igunga
Na Godfrey Ismaely
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema ni aibu kwa taifa linalokumbwa na mgawo mkali wa umeme na kuzusha kiwango cha uzalishaji kuilipa
Kampuni ya Dowans sh. bilioni 94 kwa uzembe wa serikali iliyopo madarakani.
Pia kimesena Mbali na hilo chama hicho kimesema vurugu za uchaguzi mdogo katika Jimbo la Igunga zinasababishwa na wanasiasa wenyewe na vyma vyao na si wananchi wa Igunga.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana, Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba, alisema kimsingi fidia ya tuzo ya DOWANS ni dalili ya uzembe na kukosa uzalendo kwa viongozi wa serikali ya CCM.
Alisema maamuzi ya TANESCO kutakiwa kuilipa DOWANS fedha hizo inatia shaka kwa kuwa wahusika ambao walichangia hasara hiyo wengi wao wapo serikalini huku wengine wakiwa wamestaafishwa wakati wananchi wakishindwa kuendeshea shughuli zao kutokana na mgawo wa umeme.
"Hazitakuwa tena zaidi ya bilioni 90 bali kwa sasa zitafikia zaidi ya bilioni 111, fedha ambazo TANESCO watalipa DOWANS,hii ni fedhea kwa wananchi ambao wanajikuta katika mgawo wa umeme na kushindwa kufanya kazi zao huku watu wakipoteza zaidi ya bilioni 111 kutokana na 'ombwe' la uongozi, rushwa na ufisadi wakiachwa," alisema Prof. Lipumba.
Akizungumzia Igunga Kiongozi huyo wa CUF alisema chama hicho kinalaani na kitaendelea kulaani vitendo vya ukiukaji wa sheria vinavyofanywa na baadhi ya vyama kwa kuanzisha vurugu katika jimboni humo.
"CUF inalaani wote walioleta vurugu, kutamba au kufyatua bastola, tunatoa wito kwa Tume ya Uchaguzi kupiga marufuku mtu yeyote isipokuwa askari walioko katika kazi za ulinzi kwenda na silaha za moto katika mikutano ya hadhara," alisema Prof. Lipumba.
Alifafanua kuwa haipaswi kusubiri hadi silaha zitumiwe na watu kuuwa au kuumizwa ndipo hatua za kupiga marufuku zikuchukuliwe na kuutaka NEC kutimiza wajibu wake kutokana na viashiria.
"CUF na mgombea wake wameendesha kampeni za kujenga hoja, hatukutukana mtu wala kufanya ubabe au kuleta vurugu au kumvua DC mtandio wake, bali kampeni za kistaarabu amabazo zinapaswa kuwa mfano wa siasa za kidemokrasia nchini.
"Wananchi wa Igunga hawana utamaduni wa fujo na vurugu kwa kuwa mila za Wanyamwezi na wasukuma zinasisitiza kuheshimiana na ninauhakika wameguswa na kufurahishwa na hoja alizojenga mgombea Ubunge wa CUF Bw.Leopold Mahona, na watamchagua kuwa mbunge wao," aliongeza Prof. Lipumba.
Akizungumzia ziara yake mjini Washington D.C Marekani itakayochukua muda wa miezi mitano alisema ziara hiyo inalenga kufanya uchambuzi na utafiti juu ya njia ambazo zinaweza kufanyika ili watanzania waweze kujikwamua na umasikini zikiwamo sera ambazo zinaweza kutumika ili kuchochea maendeleo ya taifa.
"Nimekubali kwenda Washington D.C kwa miezi mitano kutafakari na kufanya utafiti kuhusu ujenzi wa mfumo wa kuendeleza demokrasia sambamba na kukuza uchumi unao ongeza ajira na kuleta neema kwa wananchi wote.
Mungu akijalia kesho (leo), Septemba 30 mwaka huu nitaondoka nchini na nitarejea mwanzoni mwa mwezi Machi, 2012," alisema Prof. Lipumba.
Sawa walipeni hao Dowans fedha za ufisadi,Lakini hili jambo litaleta maana kama wausika nao watatupwa gerezani na sio kuwaangalia.Lazima sheria ichukuwe mkondo wake.
ReplyDeleteKuhusu Igunga ni kweli Igunga hatuna matatizo wala fujo za ku risasi wala kuvua watu mitandio.Vyama vilivyofanya hivyo vinajulikana.
ReplyDelete