Na Benjamin Masese
MGOMBEA ubunge Jimbo la Igunga kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Joseph Kashindya jana aliwapandisha jukwaani watoto
wakr akikanusha madai kuwa ni msimbe huku akiomba kura za wananchi.
Kauli hiyo ilitolewa na Bw. Hassan Mwakasubi ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za CCM uliofanyika Uwanja cha Sokoine mjini Igunga.
Bw. Kashindye alilazimika kuwatoa watoto
wake shuleni na kuwapandishwa jukwaani kutokana na tuhuma zilizotolewa na CCM katika mikutano yake ya kampeni kuwa hana familia.
Aliwapandisha jukwaani watoto wake watatu wote wa kike katika mkutano uliofanyika Kata ya Ndembezi ambapo kila mmoja alijitambulisha anakoishi na shule wanazosoma na kisha wakamuombea kura.
Akizungumza na wananchi Bw. Kshindye alisema kuwa mke wake anaitwa Elizabeth Joseph ambaye hivi sasa yupo mkoani
Shinyanga akimuuguza mama mkwe ambapo muda wowote atarejea Igunga kuungana naye katika kampeni za uchaguzi huo.
"CCM ilipoana pale nyumbani hakuna mke wala watoto wakadai mimi ni msimbe wakadhani wamepata njia ya kunichafua, watoto ninao hebu pandeni jukwaani na mke wangu yupo mkoani Shinyanga anamuuguza mama mkwe," alisema.
Mbali na hilo alisema kuwa kuna taarifa za vitisho dhidi ya walimu na watumishi wengine ambao wanaonekana kumuunga
mkono ambapo aliahidi kufa nao kwa kuwatetea ikiwa watafanyiwa hivyo.
Bw. Kashindye alisema katika kata hiyo kumekuwepo na matatizo mbalimbali sugu na kuwaahidi kuyatatua ikiwa wananchi watampa ridhaa ya kuwa mbunge wao.
Baadhi ya matatizo aliyoyatajakuwa kero kubwa na sugu ni uhaba wa shule, vifaa, walimu, maji, barabara na kuongeza kwamba atasimamia miradi ya maendeleo na kuibua ufisadi uliokuwa ukifanywa na watendaji na madiwani kwa kula fedha zilizokuwa zikitengwa kwa ajili ya maendeleo.
Pia alidai viongozi hao wamekuwa wakitumia fedha za wananchi huku wakishindwa kuwasomea mapato na matumizi kwa muda mrefu na kusababisha kukwama maendeleo ya kata zote za
Igunga.
Naye Mbunge wa Maswa Mashariki Bw. Slvester Kasulumbai alisema kuwa njia ya muongo ni fupi na muongo hana giza akiwa na maana kwamba CCM imefikia mwisho wa uongo wake na ahadi zao zimekoma na kuwataka wananchi kuamka.
Hata hivyo alidai kuwa imegundulika kwamba baadhi ya watu waliozimia na kulia wakati Bw. Rostam Aziz anajiuzulu waliandaliwa kwa kupewa mafunzo na baadaye walifanyiwa majaribio ya kulia na kuzimia kwa ujira.
Bw. Kasulumbai alisema hivi sasa CCM inafananishwa na tunda la tikiti maji ambalo rangi yake ni ya kijani na likipasuliwa linatoka maji mengi ikiwa ni ishara ya kulia na hatimaye kifo.
kwa kuongezea tu kashindye ungewaambia kuwa watoto wangu wako hapa na wanasoma shule za hapa kama watoto wenu. je watoto wa kafumu watoto wake wanasoma wapi ? atawezaje kuimarisha shule hizi wakati watoto wake amewakimbiza shule zingine?
ReplyDeleteWatoto wa haramu hao kama kimada wa kihaya alivyomzalia Slaa karibuni,hivi kweli dini yenu ya kikiristo inakubali watoto wa nje?
ReplyDeleteKwani watoto wa nje ni haramu?Kitanda hakizai haramu hivyo hata huyo Dr Slaa ana haki ya kuoa na kuzaliwa watoto na mchumba wake usilopoke tu kwani watu huanzia uchumba na mwisho ndoa katika uchumba mengi huweza kutokea ikiwemo mimba...ni wachumba wangap wamezaa na baadae wakafunga ndoa?Fuatilia ndani ya familia yenu....
ReplyDelete