19 September 2011

Manchester United ni noma

LONDON, Uingereza

MANCHESTER United, jana ilizidi kujichimbia kileleni katika Ligi Kuu England, baada ya kuilaza Chelsea mabao 3-1 kwenye mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa
Old Trafford.

Matokeo hayo yameifanya United kuwa na rekodi ya kushinda mechi zao zote tano na kufikisha pointi 15.

United ilihesabu bao la kwanza kupitia kwa Chris Smalling kwa kichwa katika dakika ya nane, akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Ashley Young.

Wakati Chelsea ilijikuta wavu wake ukitikiswa kwa mara ya pili na Luis Nani dakika 37.

United ambayo ilicheza kwa kasi na uelewano, ilipata bao la tatu kupitia kwa Wayne Rooney katika dakika 45.

Kipindi cha pili Chelsea ilijaribu kuanza kucheza kwa nguvu na kupata bao lililowekwa kimiani na Fernando Torres, dakika ya 46 akipata pasi ya Nicolas Anelka.

United ilipata penalti dakika ya 55, Baada ya Bosinga kumwangusha Nani lakini Rooney, alipiga na kupanguliwa na kipa Petr Cech.

Chelsea ingeweza kusawazisha kama mshambuliaji wake Torres, angekuwa makini ambapo alikosa goli dakika 71, dakika ya 83 baada ya kupenyezewa mpira na Ramires, aliyebaki peke yake na wavu baada ya kumlamba chenga kipa De Gea, lakini akatoa nje.

Katika mechi nyingine ya ligi hiyo, Tottenham ikiwa kwenye uwanja wao wa White Hart Lane, jana iliilaza Liverpool iliyokuwa na wachezaji tisa uwanjani mabao 4-0, hivyo kujiweka katika nafasi nzuri.

Nayo Manchester City ikiwa ugenini ilitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Fulham.
13.

Sunderland nayo ilipata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Stoke City.

No comments:

Post a Comment