Na Moses Mabula Igunga
MTU moja Bw. George Salum (21)amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Igunga akikabiliwa na mashitaka mawili ya kujeruhi na kudhuru mwili kwa
kummwagia tindikali, Bw.Musa Tesha.
Akisoma mashitka hayo mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Bi. Sarah Nyamonge, Mwendesha Mashitaka wa Polisi Mkaguzi wa Polisi, Bw.Edison Mwamafupa, aliiambia mahakama hiyo kwamba Septemba 9, mwaka huu saa 5 usiku ndipo Bw. Salim alimjeruhi Bw. Tesha kwa vitu vya majimaji yaliyomsababishia maumivu makali usoni na mwilini.
Alisema majimaji hayo yalimsababishia maumivu makali majeruhi huyo ambaye bado amelazwa hospitali.
Aidha mwendesha mashitaka huyo aliendelea kuimbia mahakama kwamba majimaji hayo ambayo alimwangiwa machoni yamesababisha ashindwe kuona.
Mshitakiwa alikana shitaka hilo na alinyimwa dhama baada ya upande wa mashitaka kueleza kuwa hali ya majeruhi huyo bado ni mbaya.
Alisema majeruhi huyo anaendelea matatibabu hospitali ya Muhimbili.
Alisema kitendo cha mahakama kutoa dhamana kwa mshitakiwa kinaweza kuathiri usalama wa mshitakiwa.
Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena Septemba 26, mwaka huu.
Tesha (24) ambaye ni mwanachama wa CCM inadaiwa alimwagiwa tindikali a watu wasiojulikana.
Alimwagiwa majimaji hayo yanayodaiwa kuwa tindikali baada ya kumaliza kazi ya kubandika mabongo ya mgombea ubunge wa CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Igunga, Dkt Peter Kafumu.
No comments:
Post a Comment