19 September 2011

JK aenda Marekani kuhudhuria kikao cha Baraza Kuu-UNGA

Na Mwandishi Wetu

RAIS Jakaya Kikwete ameondoka nchini jana usiku kwenda New York, nchini Marekani kuhudhuria kikao cha 66 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA).Akiwa
nchini humo, Rais Kikwete pia atashiriki mikutano mingine ya viongozi wa nchi na Serikali ambavyo vina maslahi kwa Tanzania na Afrika.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ,Dar es Salaam jana, ilisema atashiriki katika ufunguzi wa mkutano huo ambao utajadili jinsi ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza.

Kesho hiyo hiyo, Rais Kikwete atakuwa Mwenyekiti wa mkutano wa waandishi wa habari kuhusu Maendeleo ya Umoja wa Viongozi wa Afrika Kupambana na Malaria.

“Pamoja naye katika mkutano huo, miongoni mwa waalikwa watakuwa Rais Paul Kagema wa Rwanda, Goodluck Jonathan wa Nigeria na Rais wa mstaafu wa Marekani, Bw. Bill Clinton.

“Pia Rais Kikwete atashiriki mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Clinton Global Initiative na atahudhuria mkutano maalumu wenye mada ya Putting Teeth into Non-Communicable Disease ambao unaandaliwa kwa pamoja na nchi za Tanzania, Australia na Sweden,” ilisema taarifa hiyo.

Ilisema kuwa Rais Kikwete pia atashiriki mikutano, hafla mbalimbali na kuhutubia mkutano wa UNGA akiwa msemaji wa pili baada ya nchi ya Cyprus.

5 comments:

  1. WATANZANIA MLIO NEW YORK FANYENI MAANDAMANO KUONYESHA HATUMTAKI HUYU JAMAA! HALAFU ATAKUWA AMEVAA SUTI ZA YULE BASHA WAKE! MABANGO YASOMEKE' RUDISHA SUTI ZA MWARABU', 'REJESHA NYUMBA YA SERIKALI', 'TOKA KABLA YA 2015'

    ReplyDelete
  2. Kioo cha mtu ni Mtu hivi wewe na akili zako uchwara ukamwambie kiongozi wetu eti atavaa suti za Basha wake wewe ndio una mabasha usie na haya tabia zako chafu ndio unafikiria kila mtu kama wewe.Acha ujinga kumkashifu kiongozi wetu.Kama huna maoni ni bora ukanyamaza kuliko kuandika utumbo wako.

    ReplyDelete
  3. HA HA HA HA!!! KWELI CHUKI BINAFSI WA MBILI
    NI WA MBILI SIKU ZOTE,KELELE ZA MLANGO HAZIMZUII MWENYE NYUMBA KULALA,HUYO JAMAA KESHALAMBA DUME NI MPK 2015 HANG'OKI NG'OO LABDA MAUTI YAMKUTE KWA MAPENZI YAKE SUBHANA WA TAAALA,KUNYWA TONGWA LAKO ULALE.

    ReplyDelete
  4. Hofu yangu ni kuanguka huko alikoenda, itakuwa mtihani kweli, kwani ni lazima kila safari aende yeye? anaweza kumtuma Rais wa Zanzibar au Makamu wake! Pili ni idadi ya delegates ktk msafara huo, tumedokezwa inafika 50! si balaa hili?

    ReplyDelete
  5. Sio mbaya mwache ajifaidie mihela ya madini idadi hiyo mbona ndogo sana, kuna ujumbe unakujaga hapa kama watu 300 nini 50?Anamalizaga awamu yake kwa raha zake !!!
    Anaweza kupataga misaada ya vyombo vya muziki vya TOT,(Tanzania One Theatre)

    ReplyDelete