19 September 2011

.......................................................

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed shein,na mkewe,Mama  Mwanamwema wakisalimiana na wananchi wa Ziwani Wilaya ya Chake chake Pemba wakati  walipofika kuwafariji wananchi wa sehemu hiyo waliofiliwa na ndugu zao katika ajali ya meli ya Mv Spice Islander iliyozama hivi karibuni katika mkondo wa Nungwi kaskazini Unguja.

2 comments:

  1. Baba SHEN huu ni wakati hasa wa kulaumiana hasa ukizingatia kuwa nchi hii wewe na kikwete mnaiongoza kiholela.
    Ni lini ukaenda kiembe samaki ukaone watu tunavyopakiwa kama mikate kwenye magari yaliyopitwa na wakati? ni lini kikwete akaenda kutazama wananchi wake wanavyopakiwa kwenye vipanya na kuchukua hatua? Serikali zote mbili ni mfa maji na sikio la kufa. unaunda tume ya nini? hakuna osama kule wala bomu hiyo tume ya watu wengi ina maliza pesa zetu bure.
    Tunangoja msiba mwingine kama hatua hazitachukuliwa.
    Ndege, meli, mabasi, mapikipiki ndiyo usiseme, bajaji nk/ who will change this nation? Naomba tuombe michuki aje tanzania kwa mwezi mmoja maana hata wabunge wetu hutasikia wakikemea tabia ya usalama a raia kwani wengi ni wanahisa.

    ReplyDelete
  2. wasilaumiwe viongozi. walaumiwe wapiga kura kwani wao ndio wanaochagua viongozi. siku watayokemea uwajibikaji, viongozi watabadilika pia.

    ReplyDelete