15 September 2011
Fainali Airtel Rising kuanza J'mosi
Na Addolph Bruno
TIMU za soka za vijana wenye umri chini ya miaka 17 za mikoa ya Mwanza na Morogoro, zinatarajia kufungua pazia la fainali za michuano ya Airtel Rising Stars, itakayoanza
Jumamosi Jijini Dar es Salaam.
Fainali hizo zitahusisha timu za mikoa minne ambayo ni Iringa, Morogoro, Dar es Salaam na Mwanza na zitamalizika Septemba 24 mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana, mara baada ya kutangaza droo ya fainali hizo, Ofisa Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Iddi Mshangama alisema kila siku utachezwa mchezo mmoja siku.
Alisema Iringa itacheza na wenyeji Dar es Salaam Jumapili katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
"Kwa mujibu wa droo yetu, kutakuwa na mapumziko Septemba 19, siku itakayofuata Morogoro itacheza na Iringa na Septemba 21 wenyeji Dar es Salaam watacheza na Mwanza," alisema.
Alisema mechi nyingine itakayopigwa Septemba 23, mwaka huu Mwanza watamenyana na Iringa ambapo mechi ya mwisho itachezwa Kati ya Morogoro na Dar es Salaam na kisha mshindi kutangazwa.
Akizungumzia mashindano hayo Ofisa Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema wachezaji sita watakaofanya vizuri watachaguliwa kuungana na wenzao sita kutoka kila nchi ya Afrika inayoendesha mashindano hayo katika kliniki itakayofanyika Oktoba 27 hadi Novemba 23 Dar es Salaam.
Alisema wakufunzi kutoka katika klabu ya soka ya Manchester United ya Uingereza watakua nchini kuendesha kliniki hiyo ambapo Tanzania imechaguliwa kuwa kituo cha kuendeshea kliniki hiyo.
Alisema timu zitakazoshiriki fainali hizo zitaanza kurejea Jijini Dar es Salaa kuanzia ijumaa ambapo zawadi mbalimbali zitatolewa kwa mshindi wa kwanza mpaka wa tatu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment