*Adaiwa kupanga njama za ushindi wa CCM jimboni humo
*CHADEMA wambeba juu juu, watendaji pia wakong'otwa
Na Benjamin Masese, Igunga
MKUU wa Wilaya ya Igunga Bi. Fatuma Kimario, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kudaiwa kukutwa akiendesha kikao cha siri na
watendaji wa Kijiji, kata, tarafa, na wazeee maarufu kwa lengo la kuchafua Mkutano wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mkutano huo wa CHADEMA ulitarajiwa kufanyika katika Kijiji cha Isakamaliwa Kata ya Isakamaliwa na kitendo cha Mkuu huyo wa wilaya kukutwa akifanya mkutano ulisababisha kiongozi huyo kuvurutwa na kubebwa juu juu na wafuasi wa CHADEMA huku watendaji wakiambulia kipigo.
Viongozi waliokuwemo katika kikao hicho walikimbia na kubaki mtendaji wa kijiji hicho Bw. Shokoro Karedia, na mtendaji wa kata aliyefamika kwa jina moja la Bw.Nyamwamga ambao walipewa kipigo na wafuasi wa CHADEMA kabla ya kutokomea kusikojulikana.
Kikao hicho kilivunjwa haraka huku nyaraka mbalimbali zilizokuwa ajenda zikikamatwa na viongozi wa CHADEMA na kukabidhiWA Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Willibroad Slaa.
Baada ya Bi. Kimario kubebwa na kuwekwa katikati ya barabara alihojiwa na viongozi wa CHADEMA pamoja na waandishi wa habari uhalali wa kufanya kikao hicho.
Mkuu huyo wa wilaya aliyekuwa na gari lake yenye namba STK 38O6 alihojiwa na viongozi hao wa CHADEMA na wafuasi wake huku akishindwa kujibu na kuishia kuomba maji ya kunywa huku akihema na kuomba msaada kwa wasaidizi wake.
Alipoulizwa kama alijua kwamba kuna mkutano hapo alijibu kuwa hakujua na hata ratiba ya mikutano hiyo haijamfikia ofisini kwake na kuahidi kufuatilia ofisi za Halmashauri.
Akijieleza alisema yeye kama kiongozi wa serikali aliitwa na uongozi wa kata na serikali za mitaa kujadili mambo mbalimbali ya mifugo kuhamishwa, masuala ya mimba mashuleni, mipaka ya shule, elimu bora, ujenzi wa vyoo na nyumba bora za walimu pamoja na uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga.
Hata hivyo nyaraka zilizodaiwa kukamatwa na kukabidhiwa Dkt.Slaa zilidaiwa kuwa na ajenda ya mbalimbali za kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo pamoja na kuwahamasisha vijana waliopata mafunzo wanafanya kaziz kama walivyoagizwa.
Hata hivyo Bi. Kimario alikiri kufanya makosa kutokana na kutokuwa na ratiba ya uchaguzi huo mdogo na kuomba kuonana na Dkt. Slaa kumuomba radhi kwa kitendo hicho na kukubali kufanya hivyo baada ya mkutano huo kumalizika.
Kutokana na hali hiyo viongozi wa CHADEMA na wananchi waliondoka eneo hilo na kwenda eneo la mkutano alikokuwa anahutubia Dkt. Slaa na Bw. Kashindye huku wakimsubiria kwa hamu kuja kuomba radhi.
Awali kabla ya tukio hilo wakati wananchi wakiwapokokea viongozi wa CHADEMA akiwemo mgombea wao Bw. Joseph Kashindye, ghafla kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Juma Mwangara, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Zahanati alijitokeza mbele ya maandamano hayo na kuzua tafrani.
Ilidaiwa kuwa wananchi wa Kata ya Isakamaliwa ndio walitoa taarifa ya kikao cha Mkuu wa Wilaya katika ofisi ya kata na kwamba lengo ilikuwa kuvuruga mkutano wa CHADEMA.
Tukio hilo liliongozwa na wafuasi wa CHADEMA pamoja na Mbunge wa Maswa Mashariki Bw. Slyvester Kasulumbai, Mbunge wa Viti Maalum Bi. Suzan Kiwanga huku Dkt. Slaa na mgombea ubunge Bw. Kashindye walibaki majukwaani wakiendelea kuhutubia wananchi waliokuwepo.
Dkt. Slaa alisema kuwa ni makosa kwa mkuu wa wilaya kufanya vikao karibu na mkutano wa kampeni huku akitumia gari la serikali lililokuwa na bendera.
Watanzania Someni Historia ya Lebanoni war. Mtajua kuwa amani inaweza kupoteal wakati wa wowote
ReplyDeleteHAYA HUO NI MWANZO SIJUI MWISHOWE ITAKUWAJE KILLA LA KHERI WANA IGUNGA,MUWE MAKINI NA MAAMUZI NA MUZINGATIE SHERIA MSIJE MKAPOTEZA MWELEKEO, MSIKURUPUKE!!
ReplyDeleteCHADEMA NI MAGAIDI. WAKIPEWA NCHI NI MAPANGA TU KWENDA MBELE.
ReplyDeleteMALARIASUGU JF
SOMA HAPA
http://www.jamaaforums.freeforums.org
CHADEMA NI MAGAIDI. WAKIPEWA NCHI NI MAPANGA TU KWENDA MBELE.
ReplyDeleteMALARIASUGU JF GAIDI NI WEWE MWENYEWE NA MAFISADI WENZAKO MNAOKUMBATIA CCM NA KUWEKA KAMBI ZA VIJANA MAPORINI SIJUI HUKO NDO KUNA WAPIGA KURA AU NDO MNAJIFUNZA MBINU ZA KUIBA KURA SAFARI HII IGUNGA MTAISIKIA INAENDA UPINZANI
TATIZO LA WAKUU WA WILAYA KUWA MAKADA WA CHAMA NDO HILI!TULITARAJIA YEYE KAMA MWENYEKITI WA USALAMA WA WILAYA AJUE NA KUFAHAMU RATIBA ZA MIKUTANO YA KAMPENI NA AINA YEYOTE YA MKUSANYIKO KWA LENGO LA KUHAKIKI USALAMA!MI NAOMBA VIONGOZI WETU WABADILIKE TUKO KTK MFUMO WA VYAMA VINGI KWA HIYO WANATAKIWA KUWA FAIR!KTK BUSARA YA KAWAIDA ANGEAHIRISHA KIKAO KWANI LAZIMA WATENDAJI WA KIJIJI NA KATA WALIMWELEZA JUU YA UWEPO WA KAMPENI LAKINI ALIPUUZIA HAYA MENGINE TUNAWEZA KUYAEPUSHA!!ILI KUEPUKANA NA LAWAMA AMBAZO SI ZA MSINGI!
ReplyDeleteWewe malariasugu kweli malaria imekupanda kichwani hujui hata unachokisema cjui ndo umelogwa kwa pesa za kifisadi, sijui? WEWE NA ccm ndo magaidi ndio maana mnapiga sana kampeni za udini but take care, moto wa kidini ukiwaka tanzania haitachagua ni mCUF mCHADEMA wala Mccm, wote watapata shida. mmekula rasilimali za watanzania sasa mnataka damu zao haya, damu ikimwagika itakauwa laana juu ya vichwa vyenu na vizazi vyenu vyote.
ReplyDeleteWewe MALARIA SUGU tunakujua tangu Jamiiforums. Wewe ni kibaraka namba moja wa CCM na MAFISADI. Tunakuonya kuwa hizi si zama za PROPAGANDA tena, na wewe unachangia kutujaza chuki kwa kutetea UDHALIMU wa CCM na SERIKALI yake. Hamtaki kujirekebisha (eti kuvua MAGAMBA), ila mnataka kutawala na kutunyonya MILELE. Mwisho wenu tayari sasa.
ReplyDeleteNdugu Mhariri!Katika habari hii ni wapi paliposema kuwa mkuu wa wilaya alipigwa!?Kichwa cha habari na habari yenyewe ni tofauti.
ReplyDeleteANGALIA! usije kupoteza heshima ya gazeti lako.
kila siku nasema hawa wachaga ni mafia,wameishaona dalili mbaya kwao sasa wanaanza vitimbi,msiwachague hao mashetani,wachaga walizaliwa na mashetani,mkiwachagua siku mkiwakataa watawapiga. chagua ccm/cuf achaneni na hao mambwa
ReplyDeleteHuyu anayejiita Malaria Sugu nadhani sasa imepanda kichwani !Mirembe bado inaendelea kupokea wagonjwa wa akili kama yeye! Hivi wakuu wengine wa wilaya wanachaguliwa kwa vigezo vipi? Au kwa kukata viuno? analipwa kwa kodi zetu na wala siyo kwa kodi za mafisadi wala CCM na wala si kwa kodi za wagonjwa wa akili wenye malaria sugu! ajue huyu malaria yake imekuwa sugu baada ya CCM kushindwa kumtibia!
ReplyDeleteHahahaaaa!yangu macho na masikio, lakini sina sauti ya kusema sana, ila CCM imenichosha mimi mama ananisimulia kuwa mimi nilizaliwa kwenye kichaka alikuwa anakimbia kodi ya kichwa, isingekuwa vyama vya upinzani sijui ingekuwaje. Nawaombea vyama vya upinzani mshike hiyo nafasi igunga iwe Chadema,Cuf, UDP na n.k. CCM piga teke wametuchosha, Labda na ajali hizi za mara kwa mara wanasababisha wenyewe wamekuwa na dhambi nyingi mno, nendeni kanisani mkaungame CCM mtatumaliza.
ReplyDeleteDk Slaa , DC hapeperushi bendera . na hakuna sheria inayomkataza kwenda kokote wakati wowote na kufanya kazi popote wakati wowotea . hiyo ni fujo . mtavuna mnachopanda , mtakaa kimya na magaidi wenu siku ya tarehe 2 oktoba.
ReplyDeleteUpuuzi mtupu , mnadhani mtashinda kwa kufanya vurugu? hampati kitu . utaona ubunge wa igunga ndotoni
ReplyDeleteKumpa shetani kura yako ni sawa na kujitia kitanzi,huyo anayesimulia habari ya mama yake na kodi ya kichwa nimwehu wala haelewi historia,simlaumu kwanza anasema kazaliwa kichakani,huenda aligonga kichwa kwanza hivyo akili kupungua, hawa wachaga wameshaona wanaigunga hawadanganyiki,sasa kilichobaki ni fujo. wanaigunga msiogope kwani hao mashetani kuchukua uongozi wa nchi hii ni balaa,walipta hizo nafasi baada ya ccm kutokuwa na mshikamano na ndiyo chimbuko la kina shibuda na mbilinyi,hivi hao wangepita kura za maoni ccm leo wangitukana ccm. nchi hii ni ujanja tu lakini bora hao ccm/cuf kuliko hao mashetani. wanyimeni hao manyangau wa chadema kura tunajua watakataa maana ndio staili aliyoanzisha Slaa lakini wapigeni mwereka
ReplyDeletedc mkinga; unadhani haelewi anachofanya? ndivyo alivyoagizwa kufanya ila mambo yamemtokea puani. halafu leo ni ajabu gazeti hili kuandika ukweli huo maana gazeti ni mtoto wa ccm kama s mjukuu.
ReplyDeletedc mjinga; unadhani haelewi anachofanya? ndivyo alivyoagizwa kufanya ila mambo yamemtokea puani. halafu leo ni ajabu gazeti hili kuandika ukweli huo maana gazeti ni mtoto wa ccm kama s mjukuu.
ReplyDeletehamna chama cha mashetani bwana, ccm yenyewe haya machache inayofanya ni kutokana na kelele za chedema lasiivyo wang'egawana mpaka maji, watu wangekuwa wanamiliki maji sio migodi 2. sasa unavyoseme kunachama cha mashetani take care!
ReplyDeleteHapa ndipo utakapojua kama baathi ya wa Tanzania uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana Hebu angalia mwenyewe mtu aliyejiuzulu kwa kashfa kubwa ya ufisadi leo hii ndio kachaguliwa kwenda kwenye ufungunguzi wa kampeni eti kwa ajili ya kuhamasisha watu wa Igunga kuchaguwa chama chenye siasa uchwala pamoja na raisi ileyejiuzia mgodi wakati akiwa ikulu wote hawa wawili wananuka rushwa na ni mafisadi,ama kweli CCM inawafanya nyinyi wananchi wa Igunga kama hamna akili kabisa na bado watu wanakimbia mitaani ma kushabikia CCM kama matahaira vile huku wako gizani.Hivi watu waamka lini?
ReplyDeleteSamahani nimesahau jambo lingine kubwa kabisa,Sasa hivi wameshapewa shillingi elfu kumi kumi na wanashabikia CCM kama majuha.Ngoja uchaguzi uishe alafu mtajua kuwa mlikuwa mnashabikia ujinga wenu msioujuwa.
ReplyDeleteKuna kitu cha kujifunza khs huyo dc wa igunga. tunajaribu kuifanya ccm chama dola msitakabali wake ni mbaya sana. mheshimiwa rais wasikudanganye hao wachumia tumbo hali ni mbaya sana mitaani. sitashangaa chochote kutokea.
ReplyDeleteKuna baadhi ya wachangiaji wana mawazo finyi kuliko kawaida;mpaka napata mashaka inawezekana kuna watoto wa primary pia wanatoa comment zao humu,especially nikisoma mawazo ya malaria sugu.
ReplyDeleteTunajua fika kuwa CCM na SERIKALI yake wamepandikiza watu kwenye majukwaa haya ya kutoa maoni (kina Malaria Sugu et al) ili kuendeleza PROPAGANDA zao. Nyie badala ya kushughulika na mambo ya msingi ili kumkomboa mwananchi, nyie mnakalia PROPAGANDA ambazo hazina nafasi tena kwenye kizazi hiki cha dotcom. Tunawataadharisha kuwa, watanzania wa leo si wa jana.
ReplyDeletesijui kwanini ccm wanalipenda jimbo la Igunga hata kumtoa kafara dc wao?
ReplyDeleteNimeona JAMBO HAPA LA KUWAONYA WANA-IGUNGA. Kama mbunge wao wa CCM alilazimishwa aachie ngazi kwa tuhuma za UFISADI akiwaACHIA WANA-IGUNGA KUWA ANA-ACHANA NA SIASA UCHWARA, LEO HII IWEJE APANDE JUKWAANI NA MHESHIMIWA RAIS MSTAHAFU MKAPA KUHUSIKA KUMNADI MGOMBEA UBUNGE WA CCM? HAMJIFUNZI TU KUWA WANA-IGUNGA MMELOGWA NA CCM? SISEMI KAFUMU NI KAMA ROSTAM LAKINI HAMUONI KUWA KUNA HAJA YA KUWA MAKINI KATIKA KUMCHAGUA MWAKILISHI WENU ASIYE NA ILA YO YOTE ASIYE WAHI KUHUSIKA NA NAFASI YA UONGOZI SERIKALINI HASA WIZARA INAYOHUSIANA NA KASHFA NYINGI NA VILIO VYA WATANZANIA DHIDI YA WAWEKEZAJI? SIWACHGULII MWAKILISHI ILA NATAKA NIWAFUNGUE MACHO, CHONDE CHONDEE MUEPUKE KUHONGWA TISHETI/MAKANGA NA VJIFEDHA-HAMTAYAONA HAYO BAADA YA UCHAGUZI. KAMA MLIHONGWA POKEENI PESA TENA SANA LAKINI MUWE NA AKILI YA KUMCHAGUA MBUNGE MUMEPENDAO
ReplyDeleteWATANZANIA TUTUMIE AKILI ZETU VYEMA, IWEJE MTU ANATAKA TUMPEM DHAMANA YA KUONGOZA NCHI, LKN NDIYE MVUNJA SHERIA WA KWANZA?
ReplyDeleteTUKUMBUKE 1. UVAMIZI WA KITUO CHA POLISI ARUSHA NA KUSABABISHA MAUAJI YA WATANZANIA WENZETU. 2. UDHARIRISHAJI WA MKUU WA WILAYA.
TANZANIA HUONGOZWA KWA MUJIBU WA SHERIA NA SI VINGINEVYO, WAHUNI HAWA!!
KAMA HATUJUI THAMANI YA AMANI, TUOMBE VURUGU, TUTAJUA TU!
HAKUNA NCHI ULIMWENGUNI AMBAYO HAINA MATATIZO, LKN KUTUMIA MATATIZO YALIYOPO KUSHAWISHI UVUNJIFU WA AMANI SI HAKI
ReplyDelete