LONDON, Uingereza
MWANAMUZIKI kinda Justin Bieber, amesema anatarajia kuwa baba atakapotimiza umri wa miaka 25.Nyota huyo mwenye miaka 17 kwa sasa, amekuwa na
mahusiano ya kimapenzi na mwigizaji Selena Gomez alisema, "ninataka kuwa baba.
"Nitakapotimiza miaka 25 au 26 ninataka kujiona mwenyewe, kama nikioa au kuanza kutunza familia."
Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, Bieber alieleza matumaini yake hayo, wakati alipoulizwa na mtandao wa mitindo kuhusu ni kitu gani anapanga kufanya katika miaka mitano.
Alithibitisha kuwa amekuwa na mahusiano ya mapenzi na mwigizaji wa Disney, Gomez ambaye ana umri wa miaka 19, akimwelezea kuwa 'anasisimua'.
Lakini alisema kwa sasa hana mpango wa kuoa kwa haraka.
Alisema: "Kitu kimoja ambacho sikifikirii kwa sasa ni kuoa."
No comments:
Post a Comment