Na Mwandishi Wetu, Mbeya
JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya jana lililazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya wananchi wa Kata ya Inyala waliondamana hadi kituo kidogo cha Polisi cha Inyala kwa
nia ya kushinikiza kuachiwa wananchi wenzao wanne waliokamatwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kuhusika kumuua mtumiwa wa ujambazi.
Ilieleza kuwa vurugu hizo za wananchi kuandamana hadi polisi, zilitokea asubuhi Agosti 27, mwaka huu na zilisababishwa na jambazi mmoja aliyevunja duka na kubomoa nyumba ya mkazi mmoja wa eneo hilo, kisha kuiba vitu vilivyokuwemo ndani.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa sharti la kutotajwa majina yao baadhi ya wananchi walisema baada ya kumkamata jambazi huyo waliamua kumpa kipigo.
Walisema polisi baada ya kufika eneo la tukio kujaribu kuokoa jambazi huyo, ilishindikana kwani tayari alikuwa alikuwa amefariki.
Alisema polisi walifanikiwa kukamata watu wanne wakiwatuhumi kuhusika na mauaji ya mtuhumiwa wa jambazi huyo.
Akizungumzia tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Bw.Anecletusi Malindisa, alikiri wananchi hao kuandamana hadi polisi.
"Nipo njiani naelekea huko kujua undani wa tukio hilo. nitakujulisha baada ya saa tatu," alisema.
Gazeti hili lilishuhudia magogo na mawe yakiwa yamepangwa barabarani.
No comments:
Post a Comment