23 August 2011

Wahadhiri wapya 12 waingia mikataba Chuo cha Ustawi

Na Grace Ndossa

CHUO cha Ustawi wa Jamii, kimeingia mikataba na wahadhiri wapya 12 ambao watashirikiana na wahadhiri 45, waliokuwepo awali kutoa elimu kwa wanafunzi
chuoni hapo.

Akizungumza na Majira Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mafunzo chuoni hapo Bw. Andrew Mchomvu, alisema wameamua  kuingia mikataba na wahadhiri hao ili wanafunzi waendelee na masomo baada ya kufukuza wahadhiri 21.

Alisema chuo hicho kilifungwa tangu wahadhiri 21 walipoanza mgomo wa kutoingia darasani.

“Hivi sasa tumeajiri wahadhiri 12 wenye sifa zinazotakiwa ambao watatumia muda wao wa ziada kufundisha wanafunzi wetu kwa kushirikiana na wahadhiri wengine waliopo,” alisema.

Alisema kuwa Juni mwaka huu, walilazimika kufunga chuo hicho baada ya wahadhiri 21, kufanya mgomo wa kutoingia darasani wakidai nyongeza ya mishahara, kupandishwa daraja, kuthibitishwa kazini na kutoona maendeleo ya taasisi.

“Madai yote waliyotoa hayana ukweli ndani yake, mtu anapotaka kupandishwa daraja lazima afikie vigezo, awe na shahada ya uzamivu na kuandika maandiko ambayo yatapitiwa na watu wengine na kudhibitishwa,” alisema Bw. Mchovu.

3 comments:

  1. Kana wanaona wameonewa nadhani ni muhimu kwa wao kufungua kesi mahakamani ili haki itendeke.

    ReplyDelete
  2. lakini migomo hata lini wakati namsikiliza mkuu wa chuo hicho inaonekana wanachuo ndio wakorofi sijui lakini serikali inabidi iangazie vyuo vikuu sana ili wanapofika huko wasiwe na la kujisingizia.

    ReplyDelete
  3. Kwahiyo ile habari ya NACTE wamesitisha udahili pale maana standards hazijafikiwa ambalo ndo lilipelekea lecturers wagome sio ishu tena....!ila wahadhiri ndo wameonekana kuwa chanzo cha matatizo..kazz kweli nchi yetu na longolongo..

    ReplyDelete