23 August 2011

Mgogoro wa wakulima, wafugaji Kisarawe watolewa ufafanuzi

Na Salim Nyomolelo

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani Bi. Khanifa Karamagi, ametoa ufafanuzi juu ya mgogoro unaoendelea kati ya wakulima na wafugaji wa Kijiji cha
Gwata, wilayani humo.

Akizungumza na Majira kwa njia ya simu jana, Bi. Karamagi alisema uongozi wa Wilaya ulifanya mkutano na wanakijiji na kukubaliana kila mmoja arudi katika eneo lake la awali.

Alisema mgogoro ulianza baada ya mifugo ya wafugaji kuingia katika mashamba ya wakulima na kula mazao yao.

“Kimsingi tumekaa na kukubaliana kuwa, kila mmoja arudi katika sehemu yake ya ardhi sasa wafungaji walichelewa kurudi maeneo yao hivyo wanakijiji wakaona Mkuu wa Wilaya anazembea, walipaswa kuwa na subira.

“Wanakijiji wanasema unapofika wakati wa kiangazi, wafugaji wengi wanatoka Mkoa wa Morogoro kuja kulisha mifugo yao lakini sisi tunajitahidi kutoa elimu juu ya matumizi bora ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji,” alisema.

No comments:

Post a Comment