23 August 2011

Mata safi, Modric aililia Chelsea

LONDON, Uingereza

WAKATI klabu ya Chelsea imekubali ada ya pauni milioni 26 kwa uhamisho wa Juan Mata kutoka Valencia, Luka Modric, juzi alikataa kusafiri na timu yake kwenda
kucheza Manchester United usiku wa kuamkia leo.

Chelsea ilikuwa imetuma ofa ya pauni milioni 30 kwa Tottenham kwa ajili ya Modric (25), ambaye anataka kuhama katika timu hiyo.

Kiungo huyo wa Spurs alimwambia Kocha Harry Redknapp kwamba, hakusudii kuichezea tena timu hiyo.

Redknapp alikuwa akitumaini kuwa, Modric angekuwa fiti kwa mechi iliyopigwa Old Trafford, baada ya awali kuwa na maumivu ya korodani.

Chanzo kutoka ndani ya Spurs kilisema: "Luka anataka kuondoka na kujiunga Chelsea.

Kocha wa Andre Villas-Boas anamtaka pia Juan Mata, akiamini anaweza kusaidia kuimarisha sehemu ya kiungo.

Mata mwenye umri wa miaka 23, jana alitarajiwa kwenda London, Uingereza kwa ajili ya kuchunguzwa afya yake, kabla kukamilisha uhamisho.

Chelsea imethibitisha kwenye taarifa yake: "makubaliano yamefikiwa na Valencia kwa ajili ya uhamisho wa Juan Mata.

"Kilichobaki sasa katika uhamisho ni mchezaji kupimwa afya na kukubaliana kuhusu maslahi binafsi."

Villas-Boas amezipiga bao timu mahasimu za London, Arsenal na Spurs.

Mchezaji huyo aliyewahi kuichezea Real Madrid alipokuwa kinda, alijiunga na Valencia mwak 2007 na kufunga mabao nane na kuisaidia kushika nafasi ya tatu katika msimu uliopita wa La Liga.

Mata  alikuwa miongoni mwa wachezaji wa timu ya Hispania waliotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini, ni nahodha aliyeisaidia timu ya nchi hiyo kutwaa ubingwa wa Ulaya  wa mashindano ya wachezaji wenye miaka chini ya miaka 21.

No comments:

Post a Comment