26 August 2011

SAKATA LA JAIRO

Serikali ya JK yajichanganya

*Yaagiza Jairo asimamishwe kazi tena
*Ni kutokana na shinikizo la wabunge
*Pinda ahoji tena matumizi ya mil 578/-


Na Pendo Mtibuche, Dodoma

RAIS Jakaya Kikwete, amemsimamisha tena kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, Bw. David Jairo, ikiwa ni siku moja baada ya wabunge kupinga uamuzi wa serikali kumrejesha ofisini.

Hata hivyo hatua hiyo ya Rais kumsimamisha tena Bw. Jairo imeonekana kuwa ni ya kujichanganya kwa viongozi wa juu wa serikali akiwamo Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Wiki chache zilizopita Waziri Mkuu alimsimamisha kazi Katibu Mkuu huyo kwa tuhuma za rushwa, lakini juzi Ikulu ikaamuru arudi kazini, kabla ya Rais kutangaza kumsimamisha tena jana baada ya wabunge kuamua kuunda kamati teule kuchunguza tuhuma dhidi ya Bw. Jairo.

Hatua ya Bw. Jairo kusimamishwa kazi kwa mara ya pili, ilitangazwa bungeni jana na Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, wakati akijibu maswali ya hapo kwa hapo ya wabunge.

Bw. Pinda alikuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Hai (CHADEMA), Bw Freeman Mbowe, alihoji kuwa serikali haioni haja ya kumpa likizo Bw. Jairo kutokana na Bunge kupinga kauli ya Katibu Mkuu Kiongozi Bw Philemon Luhanjo aliyoitoa juzi na Bunge kufikia uamuzi wa kuunda tume ya kuchunguza swala hilo.

Akijibu swali hilo Waziri Mkuu alisema kuwa tayari hatua hiyo imekwishachukuliwa na Rais Kikwete  ya kumwagiza Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Nishati na Madini kwenda likizo ili kutoa nafasi kwa tume teule iliyoundwa na Bunge kuchunguza tuhuma zinazomkabili.

Alisema kuwa serikali itajitahidi kutoa ushirikiano juu ya jambo hilo  ili kuweza kubaini mambo mbalimbali yaliyojitokeza katika suala hilo zima.

Hata hivyo Mbowe aliitaka serikali kueleza kuwa ni hatua gani itazichukua kwa wale watakaobainika kutumia fedha zilizokusanywa na Katibu wa Wziara hiyo.

Hata hivyo Waziri Mkuu alihoji uhalali wa wizara hiyo kutaka kutumia sh. milioni 578 kwa ajili ya posho wakati Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo ilitumia muda wa siku tano kujadiliwa haikuweza kuwa na bajeti kubwa kiasi hicho ambapo ilitumia sh.milioni 174.5 tu.

Akijibu swali hilo pia Waziri Mkuu alisema kuwa jambo hilo liachiwe kamati hiyo itakayoundwa na kuchunguza mambo mbalimbali kuhusu suala hilo na kwamba kamati hiyo ya Bunge ndio itakayokuja na majibu kama katibu mkuu huyo alikuwa sahihi au la.

Juzi uamuzi uliotangazwa na serikali wa kumrejesha kazini Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. David Jairo,ulipingwa vikali na wabunge huku wakisema imeonesha dharau kwa chombo hicho.

Moto wa kupinga kurejeshwa kazini Bw. Jairo uliibuliwa Bungeni mjini Dodoma jana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA) baada ya kuwasilisha hoja binafsi kwa kuzingatia kanuni ya 51 (3)ambayo inampa mbunge nafasi ya kutoa hoja bila kufuata utaratibu wa taarifa nyingine.

Wakati Bunge likiamua kuuda tume, jijini Dar es Salaam Bw.  Jairo, juzi alizungumza na gazeti hili ofisini kwake na kujibu mapigo ya wabunge hao. Aliwataka wabunge hao kuisoma ripoti ya CAG kwa umakini ili wajiridhishe.

"Ni lazima wabunge wakubali kuheshimu vyombo vyenye mamlaka ambavyo wao wanaviamini katika maamuzi ya kitaifa, kama watashindwa kuamini ripoti ya CAG na PCCB katika hili, basi kutakuwa na mtu ana maslahi yake mengine anayo yataka,"alisema Bw. Jairo.

Alisema mtu wa kawaida akituhumiwa bungeni hapewi nafasi ya kujitetea, lakini kama kamati itaundwa nafasi hiyo itatolewa kwa kuhojiwa na kupitia vielelezo mbalimbali na kanuni kama zinavyotaka.

Bw. Jairo kwa siku ya juzi alionekana mwenye furaha, huku akisema alituhumiwa  na muhimili mwingine na yeye yuko chini ya muhimili mwingine ambao una mamlaka halali za kufanyia kazi suala hilo na zimefanikiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria. Alisema serikali imejiridhisha kuwa anafaa kutenda kazi kwa nafasi hiyo, hivyo Bunge lizingatie taratibu na mipaka ya mihimili mingine hasa taratibu za serikali.

Alitangaza kutoa msamaha kwa wale wote waliomkejeli wakati wa sakata hilo tangu lilipoibuliwa bungeni na Mbunge wa Kilindi, Bi. Beatrice Shelukindo, huku Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, akisema kama angekuwa na mamlaka angemfukuza kazi.





16 comments:

  1. JAMANI JK ANATUPELEKA PABAYA. SI ALIKA WAMSUBIRI SASA MBONA ANAJICHANGANYA? BASI AMSIMAMISHE NA RAFIKI YAKE LUHANJO. MAANA WAMEFUATANA TOKA WIZARA YA MAMBO YA NJE. KUNANI KATI YAO? SIRI NZITO YA KUWA WASANII TU. WABABAISHAJI.

    ReplyDelete
  2. Tatizo ni kuwa Rais wetu haonyeshi LEADERSHIP kwa lolote. Nafikiri anafurahia kuwa Rais wa TZ lakini hataki kufanya wajibu wake. Na hili litai cost CCM yake kwa kiasi kikubwa. Rais msanii , Luhanjo msanii mnategemea nini. Waondoke waache watu wawajibishe wazembe. Jairo ana milion 500 za sherehe tena kwa siku moja, Mtoto wa Mkulima milion mia na kitu tena kwa siku 5. Kuna siri ya LUHANO na JAIRO na wamekula sawasawa. By the way Luhanjo anastaafu lini?

    ReplyDelete
  3. SIAMINI KAMA TANZANIA INA VIONGOZI MAKINI! KATIKA HILI TUMEPOTEA.SERIKALI INATIA AIBU.KAPEMBE

    ReplyDelete
  4. Jakaya Kikwete UNAIUA CCM. HIVI UTAKUWA MGENI WA NANI NA KASHFA ZOTE HIZI SIKU UKITOKA IKULU. JIULIZE KAMA MTU MZIMA UTAPATA MAJIBU. DUNIA IMEBADILIKA SANA WATU WANAWEZA KUKUSHINIKIZA UTOKE. DUNIA YA SASA SI ILE YA AKINA NGUMBALU.

    ReplyDelete
  5. ha kumbe ndo uongozi wa nchi wenywe

    ReplyDelete
  6. kikwere nchi imekushinda

    ReplyDelete
  7. huy jairo ni nani hadi anabeza concern za wabunge? wenzake at this juncture hujikalia kimya!

    ReplyDelete
  8. Hii inadhihirisha wazi kabisa kuwa Luhanjo si mtu makini na ni mhuni fulani anyefanya kazi kwa kubabaisha. Wengi wetu tunafahamu uhusiano wa JK na Jairo, lakini Luhanjo hakuwa na sababu yeyote ya kujipendekeza kwa bosi wake kwa kumlinda mpwa wake. Kuna taratibu za serikali na Luhanjo angezitumia bila woga. Sasa tzama, inamtia aibu. Na sidhani kama atastaafu kwa raha. Ingalikuwa ni mimi, ningejiudhulu.

    ReplyDelete
  9. Kwanza kabisa naunga mkono hoja ya slaa kwani takukuru walitakiwa kuchunguza haya matatizo kwa sababu alizozitoa.Rushwa kubwa kama hiyo ya jairo haiwezi ikawa na kumbukumbu sahihi katika mahesabu ya vitabu vya serikali kwa sababu watendaji wa hayo mambo wanajuwa nini wanafanya.Raisi hata kama sio mtendaji wa mambo yote lakini kuna wakati yeye mwenyewe anaona ya kuwa kwenye jambo fulani kuna walakini.Hivyo inambidi achukue hatua na sio kunyamaza kimya.Pia hii inaashiria ya kuwa katika serikali yetu kila kiongozi ana sauti ya kuzungumza vile anavyojisia na sio kupata maelekezo kutoka juu.Yaani hakuna mtiririko maalum wa utawala.Mtu akimka asubuhi anazungumza vile anavyoona yeye na anavyofikiri yeye.Hii ni aibu kubwa kwa nchi na hata majirani zetu sasa wanatucheka kwa jinsi mambo yanavyoendeshwa hapa nchini.Alafu ngao kubwa ya viongozi wa Tanzania ni kila siku kusema haa Tanzania bwana kuna amani sana lakini ukweli ni kwamba haa Tanzania bwana kuna wajinga kila utakachofanya wao ni hewala bwana.Huu usemi una mwisho wake na siku ikifika kila mtu atashangaa yatakayo tokea.Sisemi hivi kwa nia mbaya lakini ni kwa jinsi mambo yanavyofanyika.

    ReplyDelete
  10. Jakaya Kikwete, makatibu unawateuwa wewe. Vyombo vyote vya usalama na ulinzi viko chini yako. Iweje unashindwa kutoa maagizo ya busara hadi unaingia kwenye aibu hii? Hapa jambo la kukubalina ni moja tu Jakaya ni dhaifu - hajakomaa kuwa Rais wa nchi. Kumbe Nyerere alikuwa anaona udhaifu huu. Sasa komaa na ukuwe uwe mtu mzima mwenye busara. Uwe Rais kweli si usanii. Yaani madaraka yako anayachukua Luhanjo na wewe upo tu unatizama kana kwamba hakuna baya lililofanyika. Aibu kubwa hii yakhe.

    ReplyDelete
  11. Ikiwa itakuja kuthibitika kuwa hayo aliyoyafanya jairo ni makosa je JK atamfukuza,Luhanjo,jairo na Utouh au atwamezea ?

    ReplyDelete
  12. ...Nyerere alisema watu wanazungumza majina ingekuwa basi tungekusanya majina na kuweka katika kapu halafu akaitwa kipofu akaota jina moja na tukapta rais ikiwa umuhimi ulikuwa ni majina.

    Lakini Nyerere alisema tatizo sio majina bali ni matatizo ya nchi yetu...

    Babu aliona mbali..kikwete dhaifu kama mboga za majani.

    ReplyDelete
  13. wewe unaejiita anonymous unatoa maoni ya kisiasa. ni lazima wewe ni chadema unatakiwa kutoa maoni yasiyo na chuki wala kampeni za kumchafua JK. Toa maoni toka kichwani sio toka katika makalio

    ReplyDelete
  14. Ha! Ha! Ha! Maoni toka katika makalio? Unasema kweli anonymous?

    Ukweli ni kwamba wanatoa maoni toka kichwani ila yamejaa fitina na siasa. kitu afanye Luahanjo asemwe JK. Kitu afaye Ngeleja asemwe JK. Dah! Siasa hizi!

    ReplyDelete
  15. Nadhani ni vyema tuheshimiane wakati tukitoa opinions zetu. Nimekuwa niksema kila siku kuwa itakuwa ni vigumu kuwepo amani nnchini kwetu kama watanzania hatutajijengea tabia ya kuheshimu mawazo ya wengine. Huu usemi eti mtu anatumia akili toka makaalio, ni wa kulaniwa kwa nguvu zote. Huu ni uhuni usiotakiwa katika maoni/malumbano ya aina yoyote.
    Halafu wewe mkubwa unayetukana, kumbuka kuna kitu kinaitwa awajibikajiwa kisiasa, political responsibilty. Kama umeelimika kidigo, ambavyo sidhani maana usingetoa matusi hivyo. Kuna usemi katika kiingereza "the bucks stop on ones door" kwa mantink hii lazima kiongozi mkuu wa nchi achkuwe responsibilty kwenye mambo yote makubwa ya nchi. Nadhani "Anonymous matus" Utakuwa umenipata. Ama sivyo jaribu kujiorothesha na chuo kikuu uelimike. To me you seem to be too crude.

    ReplyDelete