15 August 2011

Messi amtabiria makubwa Aguero

BARCELONA, Uingereza

MSHAMBULIAJI Lionel Messi anaamini kuwa, Sergio Aguero atapata mafanikio katika soka baada ya kuhamia Manchester City inayoshiriki Ligi Kuu England huku
akiamini pia Manchester United itatwaa ubingwa.

City ililipa kwa Atletico Madrid pauni milioni 38 na kumsaini Aguero mwenye umri wa miaka 23 ikiamini kwamba ataisaidia timu hiyo kuondokana na ukame wa vikombe.

"Sina mashaka kwamba atafanikiwa katika soka akiwa City," alisema Messi na kuongeza;

"Atawapatia manufaa ya kweli.Ni mchezaji wa kipekee, Ana uwezo wa mkubwa, nguvu na ana uchezaji wa kipekee na kucheza kwa nichamu.

"Atafanikiwa na atasaidia kuiletea matunda City. Walinzi watapata shida sana katika kucheza dhidi yake.

"Hakuna mashaka kichwani kwangu kwamba City imemsaini mchezaji wa kipekee sana."

Messi ambaye anaonekana kuwa mchezaji wa kipekee duniani, aliongeza: " Ni mchezaji anayebadilika anayecheza katika namba tofauti. Kuzoea Ligi Kuu haitakuwa tatizo kwake.

"Carlos Tevez  amefanikiwa sana akiwa England na Aguero hakutakuwa na tofauti kwake.

"Ninafikiri inaonesha umakini ilionayo Manchester City  wakati walipomsaini mchezaji mwenye ubora wake.

"Binafsi ningependa abakie Hispania lakini amepanda kwenda Barcelona na nimefurahi na changamoto hiyo na malengo City. Fedha si kigezo cha kwenda kwake ila anapenda changamoto.

"Cha muhimu zaidi ni kwamba anapenda makombe na wazi anahisi kuhamia kwake England kunaweza kumpatia nafasi."

Lakini Messi amewaonya mashabiki wa City kutokuwa na matumini makubwa ya kutwaa ubingwa na kueleza kuwa anaona kama Manchester United ina nafasi kutwa ya kutwaa ubingwa.

Messi aliifungia Barcelona  katika mechi ya fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya United Mei, mwaka huu na anajua mambo mengi kuhusu United.

" Itabaki kuwa ni timu ambayo kila mmoja anapenda kuifunga,' Messi aliliambia gazeti la Sunday Mirror.

No comments:

Post a Comment