22 August 2011

Mbio za ubunge Igunga Dkt. Slaa, Zitto kuzindua kampeni

*CHADEMA kutumia helikopta Igunga
*Yaanika mikakati ya kushinda jimbo
*CCM yavuta pumzi, yasubiri CC


Na Benjamin Masese

VUGUVUGU la uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, mkoani Tabora linazidi kupanda
huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikitangaza safu ya viongozi wa kitaifa watakaozindua kampeni za chama hicho Septemba 9, mwaka huu.

Mbali na kuanika majina ya viongozi wake watakaozindua kampeni, chama hicho kina mkakati wa kutumia helikopta ili kufikia maeneo yote ya Jimbo la Igunga.

"Kama kawaida yetu tayari  helikopta imeandaliwa kwa mashambulizi ya kampeni jimbo la Igunga, lakini hatutaanza nayo, tutaanza na vyombo vya ardhini kwanza tukiona kuna ulazima, ndipo tutakaponyanyuka juu kwa juu na kumwaga sumu 'chini'."

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Habari Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Bw. Erasto Tumbo, wakati akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu akiwa Igunga. Alisema viongozi wa kitaifa watakaohudhuria uzinduzi wa kampeni za chama hicho ni Katibu Mkuu, Dkt. Willbroad Slaa na Naibu Katibu Mkuu Bw.Zitto Kabwe.

Bw. Tumbo alisema kuwa tayari Kamati Kuu ya CHADEMA ilikutana juzi na kupitia majina ya wagombea 16 waliochukua fomu, ambapo kwa kuzingatia sifa na mtu mwenyewe anavyokubalika kwa wananchi wa Igunga, ilimpitisha Bw.Joseph Kashindye, kuwania kiti hicho.

"Hapa tulipo hatujaanza kampeni, lakini wananchi wameonesha shauku kubwa ya kukiunga mkono chama chetu ili kuwaongoza, kwani wamedai kwamba kwa miaka mingi walikuwa hawajapata kiongozi wa kukaa nao na kujadiliana wanachohitaji," alisema Bw. Tumbo.

Alisema baada ya uzinduzi huo viongozi wa kitaifa watasambaa maeneo yote ya jimbo hilo kumnadi mgombea Bw. Kashindye, ili kuhakikisha jimbo hilo linaondoke mikononi wa CCM).

Alisema utafiti wa awali umeonesha kuwa  CHADEMA itaibuka na  ushindi kwa zaidi ya asilimia 80, huku vyama vingine vikigawana asilimia zilizobaki.

Alisema CCM ina hali mbaya kuliko vyama vingine vinavyoshiriki uchaguzi huo. Alisema dalili zinaonesha kuwa wananchi wamechoka na sera za chama hicho.

"Hadi sasa tunajua tunashinda na harakati za kumwaandaa mgombea wetu kwenda bungeni zimeanza na tutampeleka kwa maandamano hadi Dodoma na kufanya hafla fupi ya kumkaribisha,"alisema.

Naye Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi, CCM Bw. Nape Nnauye, alisema muda wowote kuanzia sasa Kamati Kuu itakutana kumteua mgombea wa chama hicho na kutangaza siku ya kuanza kampeni.

Akizungumza na gazeti hili jana,Bw. Nnauye alisema kauli za CHADEMA kujihakikishia ushindi ni mbinu za kuwatisha watu na wagombea wengine, lakini CCM inazichukulia kama kelele ambazo zimezoeleka kwao.

"Hakuna chama ambacho kinatangaza mikakati yake  barabarani,tunatarajia Kamati Kuu itakaa muda wowote kumpitisha mgombea mmoja na kutangaza siku rasmi ya uzinduzi wa kampeni, wao ndio wanasuasua sisi tuko imara na ushindi ni wetu kama kawaida,"alisema.

Awali alisema CCM ina asilimia 90 za ushindi katika jimbo hilo na kuongeza kwamba  kampeni za chini chini za baadhi ya vyama vya siasa zilizoanza Igunga ni mchezo wa watoto wadogo.

"Pale Igunga, CHADEMA haina kitu hata kama wameanza kampeni za chini chini...ule ni mchezo wa watoto na kawaida ikifika saa sita usiku lazima watoto walale na ndipo tutakaposhinda. Pia tathmini tulishafanya na tumebaini zaidi ya asilimia 90 tunashinda ndio maana hatuna wasiwasi,"alisema.

Naye Rachel Balama anaripoti kuwa  Chama cha Wananchi (CUF) kinatarajia kutangaza ratiba na mikakati mingine leo.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu akiwa Igunga, Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Bw. Julius Mtatiro, alisema;

"Nipo Igunga kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi, lakini kesho nitatoa taarifa zote kuhusu kampeni za CUF."

Naye Mwenyekiti wa Chama cha National Reconstruction Alliance(NRA) Bw. Rashid Mtuta, alisema kuwa chama chake kina nia ya kusimamisha mgombea na kinasubiri timu iliyotumwa Igunga kuangalia mazingira ya kukubalika kwake jimboni humo.

Alisema tayari timu hiyo ya watu watano ipo kwa wiki moja sasa na inatarajia kurudi wakati wowote kuanzia leo.

"Tunapozungumza tayari timu ya watu watano ipo Igunga kuangalia mazingira na tutatoa tamko," alisema Bw. Mtuta.

Alisema kuwa timu hiyo inaonngozwa na Kaimu Katibu Mkuu Taifa Bw. Hassan Kisabya.

Mwisho.

15 comments:

  1. Maira mbona hamjatupa habari Za ujambazi unaomhusu katibu wa Lema wa Arusha? haisaidii mimi naweka hadharani. hao ni majambazi Igunga msiwape watawauwa baadaye.nayo ni hii

    "KATIBU wa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Goobless Lema, anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Arusha akituhumiwa kuhusika na matukio kadhaa ya ujambazi mkoani Arusha.

    Katibu huyo, Gervas Mgonja, pia gari lake binafsi linahusishwa na kuhusika kubeba watuhumiwa wa ujambazi wanaoshikiliwa na Polisi na wako katika vituo mbalimbali vya polisi mkoani Arusha wakihojiwa.

    Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye alipoulizwa jana kuhusu suala hilo, alisema yuko safarini, lakini aulizwe Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa, Leonard Paul kwa maelezo zaidi.

    ReplyDelete
  2. WACHA CHUKI BINAFSI, WAACHE WATU WA IGUNGA WAMCHAGUE MTU WANAE MPENDA. WEWE HABARI ZA LEMA, SIJUI KATIBU WA MBUNGE ANASHIKILIWA NA POLISI, HIYO SIO ISSUE,POLISI SIO MAHAKAMA, MAHAKAMA NDIO INAWEZA KUMHUKUMU MTU NA SII WEWE. NADHANI BWANA ZOMBE, JADILI MAMBO YA MSINGI, ACHA KUWARUBUNI WATU WA IGUNGA KWA MANENO YA KI.HUNI NA KICHOCHEZI. MIMI NIKO IGUNGA, NAKUHAKIKISHIA CHADEMA HAKISHIKIKI, MTAHONGA KAMA MLIVYO KAMATWA NA TAKUKURU YENU AMBAYO HATA HIVYO IMEKATAA KUWATAJA WAHUSIKA MAANA NI VIGOGO WA CHAMA GAMBA WALIOBOBEA KWA RUSHWA NA UFISADI STADI.TUTAWASINDIKIZA CHADEMA KWA MAANDAMANO HADI BUNGENI DODOMA. MIMI NIKO TAYARI NA WATU WANGU WOTE. CHADEMA HOYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE.

    ReplyDelete
  3. hahaha, Huyo ni katibu wa mbunge na wala si mbuge mwenyewe..CHADEMA Tosha igunga, hizo ni propaganda za ccm na zombe wao,

    ReplyDelete
  4. Mtasuka,mtanyoa LEMA ni jambazi tu. na majmbazi walio ccm na chadema wamejaa kibao tu,hivi mkishinda Igunga mtajisifia? tunaelewa wazi wanaigunga watapiga kura ya chuki kwa ccm,mngeshinda enzi za Rostam kweli ningesema chama dume,hata huko kwingine mlishinda kutokana na upuuzi wa ccm tu vinginevyo mngetoka kapa

    ReplyDelete
  5. wewe chizi wa ccm acha kutapika keenye maoni mwizi wa fikra wewe.

    ReplyDelete
  6. ccm wamefuliaWACHA CHUKI BINAFSI, WAACHE WATU WA IGUNGA WAMCHAGUE MTU WANAE MPENDA. WEWE HABARI ZA LEMA, SIJUI KATIBU WA MBUNGE ANASHIKILIWA NA POLISI, HIYO SIO ISSUE,POLISI SIO MAHAKAMA, MAHAKAMA NDIO INAWEZA KUMHUKUMU MTU NA SII WEWE. NADHANI BWANA ZOMBE, JADILI MAMBO YA MSINGI, ACHA KUWARUBUNI WATU WA IGUNGA KWA MANENO YA KI.HUNI NA KICHOCHEZI. MIMI NIKO IGUNGA, NAKUHAKIKISHIA CHADEMA HAKISHIKIKI, MTAHONGA KAMA MLIVYO KAMATWA NA TAKUKURU YENU AMBAYO HATA HIVYO IMEKATAA KUWATAJA WAHUSIKA MAANA NI VIGOGO WA CHAMA GAMBA WALIOBOBEA KWA RUSHWA NA UFISADI STADI.TUTAWASINDIKIZA CHADEMA KWA MAANDAMANO HADI BUNGENI DODOMA. MIMI

    ReplyDelete
  7. Hayo ya katibu wa lema ni NJAMA za JESHI LETU LA POLISI lililojaa wezi kama akina zombe kutaka kukandamiza demokrasia ya kweli. Watanzania wa leo sii wajana, watanzania wa leo wana akili, na upeo wa kuchumbua mambo. Hakuna watu ambao siwamini duniani kama polisi wa Tanzania. wengi wapo kwa maslahi yao binafsi na ya wezi wa CCM

    ReplyDelete
  8. POLISI NAO NI MAKADA WA CCM, WANTUMIKA KUWADHALILISHA WAPINZANI HAKUNA UJAMBAZI WALA NINI NI SIASA MAJI TAKA, KAMA WAO HODARI WAKAMHOJI GAMBA JIPYA MSEKWA KWA SKENDO YA NGORONGORO, POLISI MSIPOBADILIKA MTABULUZWA NA CCM MPAKA WATOTO WENU, NYUMBA ZA BATI MCHANA JUA KALI, HAMPONI. CHADEMA WAKOMBOZI WETU NYINYI MNAWAONEA, MATESO YA UMEME, MAJI, MAFUTA NA UFISADI HATA NYINYI POLISI YANAWAHUSU, KWA TAARIFA YENU HATUDANGANYIKI CHADEMA WAKOMBOZI WETU, VIVA SLAA, VIVA LEMA, TUNDU LISU, ZITTO. GOOO CHADEMA CCM WEZI HADI WAZEE.

    ReplyDelete
  9. LEMA MWIZI NA JAMBAZI KUU ARUSHA. ANA MTANDAO WA MAJAMBAZI.MSUKE MNYOE SHAURI YENU,KATIBU ANAFANYA KWA NIABA YAKE. MPAKA BABA YAKO AULIWE NA HAO MAJAMBAZI NDIO UTASEMA KUMBE KWELI

    ReplyDelete
  10. Umuhimu wa Wananchi wa Igunga kuchagua Mgombea wa Chadema, ni suala ambalo liko wazi na wala halihitaji tuumizane vichwa kulijadili. Wana Igunga wanajipenda na wanaipenda Tanzania, kamwe hawawezi kumwacha Bwana Kashindye. viongozi wa Chadema ni wakarimu na wanawapenda wanachi wao. Ndiyo maana wanawasaidia katika mambo mbalimbali ikiwamo kuwapatia wananchi wao usafiri wanapohitaji bila kuwabagua kwa namna yoyote ile. Sasa kama Wananchi wakishafikishwa walipotaka, wanaamua kufanya uhalifu hilo linakuwa ni jambo lingine kabisa. Sisi wengine tusiwalazimishe viongozi hawa kuwa wahalifu. Hata hivyo si vizuri kuinyesha dunia nzima jinsi akili ilivyo fupi kwa kuendekeza ushabiki kiasi cha kushindwa kutofautisha 'kutajwa kuhusika, kuhusika na kuthibitika kuhusika' na uhalifu hasa katika nchi hii ambako watuhumiwa sharti watokane na kundi ambalo halijashika UTAMU.

    ReplyDelete
  11. CCM imeishiwa hoja, Kamati yote kuu ya CCM wamejilimbikilizia ardhi maelfu ya maekari wakati wananchi wanahangaika huku na kule.

    Wananchi wa Igunga watachagua mgombea wa Chadema. Wananchi wa sasa wameamka. propagamda za CCM ni uchwara, someni alama za nyakati.

    Akina Shombo wameiba matrilioni, hawagusi. Zombe ni Jambazi aliuwa wafanyabiashara wa madini. Wananchi hatujasahau.

    ReplyDelete
  12. zombei tunakujua wewe ni jambaza la kutupwa. umeua watanzania wenzetu tena wajasilia mali wazuri wala hatujasahau. umeshirikiana na mafisadi wwenzio wa CCM kuua. Tunakuonea huruma maana siku yako inakuja. ikishindwa sheria tutachukua sheria mikononi kuona hatima yako. Tuache tuamue weenyewe waatu wa igunga hatukuhittaji jambazi mkubwa wewe. toka lini umekuwa na huruma wakati uliagiza watanzania wenzetu wauawe kwenye msitu wa pande. wanaigunga tuchague wapiganaji CHADEMA maana hata hoja zao bungeni zinajieleza ni za kutetea wananchi.

    zombe huyo huyo ndio antaka searikari maskini kama hii yetu imlipe mabilion ya pesa. hizo pesa zinatoka kwa watazania maskini kama sisi watu wa igunga. hivyo zombe anataka watanzania tumlipe. je huo uzalendo wa kuipenda igunga kautoa wapi? Si utapeli huo? Achana na sisi watu wa igunga hatuku-feel hata kidogo kichefuchefu mkubwa wewe.

    ReplyDelete
  13. Jamani Watanzania Wengine kweli ni Mambumbumbu kuliko mfano. Huyo anayesema kama Lema ni Jambazi! Hajaenda hata darasa moja. Anayegombea Igunga ni Kashindye na siyo Lema.

    Jamani acheni chuki binafsi. Tutaingia mitaani kama Libya.

    Na nyie Watu wa magazeti. Naomba muangalie mambo ya kuandika. Mambo ya kipuuzi msiwe mnaandika. Andikeni mambo yanayoingia akilini. Hivi mlimfurahia Jambazi Zombe alivyowauwa Watanzania wenzetu ambao wameacha familia zao changa zikiteseka?

    Iko siku uvumilivu utatushinda.

    Mwenye Uchungu na Watanzania.

    ReplyDelete
  14. Kuna upumbavu mwingine ni mkubwa kuliko uwendwazimu hivi ni mahakama ipi imethibitisha hayo? hata kama lema ni jambazi kama huyo mpumbavu zombe anavyosema, tusipomchagua kashindye lema ataaccccha huo ujambazi? Hivi lema ndo rimoti ya ubongo wa kashindye aheni ujinga hatudanganyiki msubiri aibu tu na mkiiba au forgery yoyote, PATACHIMBIKA WALAH'

    ReplyDelete
  15. NIMEIPENDA SANA HII YA MAKAMANDA WA CHADEMA MOTO NI ULE ULE IKISHINDIKANA NI KAMA MISRI

    ReplyDelete