12 August 2011

Masaburi amfuata Mtemvu Kariakoo

Na Peter Mwenda

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Dkt. Didas Masaburi amevunja Bodi ya Shirika la Uchumi na Maendeleo Dar es Salaam (DDC)ambalo Mwenyekiti wake ni Mbunge wa Temeke, Bw. Abbas Mtemvu baada ya kugundua kuna udhibiti hafifu wa mali za shirika hilo na uwepo wa mikataba ya kiujanja ujanja.


Katika ziara ya ghafla iliyofanywa na Dkt. Masaburi Dar es Salaam jana katika miradi ya DDC Kariakoo, DDC Magomeni na DDC Mlimani Park, aligundua kuwa mikataba ya maduka ya Kariakoo imekuwa ikiwanufaisha wachache na Jiji kuambulia patupu.

Hii ni bodi ya pili kuvunjwa na meya huyo baada ya ile ya UDA ambayo alivunja na kusimamisha menejimenti yake kwa tuhuma za ubadhirifu, lakini baadaye naye akatuhumiwa kuhusika katika mashfa ya ubinafsisha wa shirika hilo bila kufuata taratibu.

Kutokana na hatua hiyo umekuwapo mvutano baina ya Masaburi na wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam akiwamo Mtemvu, kwa hatua yao ya kupongeza kufanywa kwa uchunguzi wa suala la UDA, ambapo meya huyo alisema 'kama wamemwaga mboga, yeye atamwaga ugali'

Wajumbe wa Bodi iliyovunjwa jana mbali na Bw. Mtemvu ambaye ni Mwenyekiti, ni Bw. Jarome Bwanausi (mBUNGE WA , Bw. William Bomani, Bi. Rehema Mayunga, Bw. Wendo Mwapachu na Bw. Isaac Tasinga.

Katika ziara yake jana, Dkt. Masaburi alidai kugundua uozo huo baada ya kukuta mmiliki wa kwanza katika maduka ya DDC Kariakoo akiwa amekodishwa kwa mtu mwingine kwa gharama ya juu huku anayetambulika na DDC analipa gharama kidogo.

Shirika la DDC lina miradi ya shamba la Ruvu lenye ekari 10,000, Malolo ekari 5,000, miradi ya DDC Kariakoo, DDC Keko, DDC Mlimani Park, DDC Magomeni na Parval Garage ya Magomeni.

Raia wa China anayemiliki duka hilo analipa kodi ya sh. mil. 1.6 kwa mwezi wakati DDC inalipwa sh. 300,000 kwa mwezi  na duka la pili pia ambako kuna raia mwingine wa China analipa sh. milioni 2.6 kwa mwezi ilhali DDC ikipokea sh. 300,000 kwa muda huo.

Mmoja wa wajumbe wa bodi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Lulindi, Bw. Jerome Bwanausi katika maradi wa DDC Kariakoo ambaye alikutwa na msafara huo katika moja ya maduka hayo na kuelezwa jinsi bodi yao imekuwa ikipoteza mapato, hakujibu kitu, alimsikiliza Bw. Masaburi kisha kurudi dukani na kuendelea na shughuli zake.

Dkt. Masaburi aliwataka wenye maduka hayo kutoa ushirikiano kwa Kaimu Meneja wa DDC, Bw. Cyprian Mbuya ambaye amempa siku saba kukusanya mikataba yote ya maduka 80 yanayozunguka miradi ya DDC Kariakoo na mingine ya Keko, Magomeni na Mlimani.

Akitoa taarifa ya halia ya shirika hilo Kaimu Meneja shirika hilo, Bw. Mbuya alisema mpaka sasa linadaiwa sh. milioni 500 na kila mwezi linaingiza sh. milioni 46.6 kutokana na kupangisha ofisi, maduka 75, mgahawa na baa ambayo ni sawa na sh. milioni 559.7 kwa mwaka.

Hara hivyo, Dkt. Masaburi alisema endapo kutakuwa na uthibiti wa mali za shirika hilo, maduka ya Kariakoo peke yake yana uwezo wa kuingiza sh. milioni 600 kwa mwaka.

4 comments:

  1. Wacha wee! Mijizi inaumbuana! patamu hapo! Ndio maana nchi hii haitaendelea, mijizi kibao kila kona! Hii ni picha ya kihindi ' miji kamata miji'!

    ReplyDelete
  2. MASABURI UKO JUU LAKINI ANGALIA HAO JAMAA UNAOMWAGA MBOGA YAO WATAKUKOLIMBA. LAKINI MBONA UMEUZA UDA KWA BEI YA KUTUPA HALAFU HELA MKAWEKA KWENYE ACCOUNTS ZENU. UNACHOKIFANYA NI KIZURI ILA JISAFISHE PIA WEWE MWENYEWE. ULICHOKIFANYA UDA SIYO SAWA HATA KIDOGO. ILA KWA DDC NAKUPA BIG UP NA UKAMATIE HAPO HAPO. HALAFU ANGALIA HUYO MBUNGE WA LULINDI NI MJUMBE WA BODI HALAFU HAPO HAPO KAJICHUKULIWA PANGO HAPO INAKUJA KWELI?

    ReplyDelete
  3. Sasa hawa watu wameaminiwa kwa shirik dogo tu na wanafanya hivyo, je wakipewa wizara si watachengelize hawa!!!!!!

    ReplyDelete
  4. wanatuzingua tu hawa muda wote walikuwa wapi inamaana wameshakula vyakutosha kwann usifanyanye muda wote huo umeona umetajwa ndo na wewe unawaumbua huo ni unafki kidole hata ujisafishe bado mchafu tu yani hata aibu huoni kama vipi jiudhulu tu kwa madaraka ni lazima ni hayo tu!!!!!!!!

    ReplyDelete