12 August 2011

Fabregas ahesabu saa kuhama Arsenal

LONDON, Uingereza
CESC Fabregas sasa anakaribia kutimiza ndoto yake ya kuhamia timu ya Barcelona ambayo awali ilimlea kisoka kabla ya kuahamia Arsenal


Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, kiungo huyo wa wa kihispania atalazimika kulipa fedha zake mwenyewe pauni milioni
4.5.

Arsenal sasa inajipanga kukubalia ada ya pani milioni 35.9 kutoka kwa Barca pamoja na nyingine ambazo zitatokana zitatokana na kutwaa ubingwa wakiwa na mchezaji huyo.

Ada hiyo oia itajumuisha pauni 900,000 kwa mwaka ambazo Fabregas amekubalia kuilipa Arsenal kutoka kwenye mshahara kwa muda wa miaka mitano atakayoingia mkataba na Barca.

Baada ya malumbano kuhusu ada ya mchezaji huyo katika ya barcelona na Arsenal kinachoonekana kinaweza kufanyika  kwa sasa ni kwa Fabregas kwenye miaka 24, kufanya makubaliano na Barca kuhusu  maslahi yake  na kumaliza msigano wa miaka mitatu akitaka kurejea Nou Camp.

Juzi usiku alirejea katika uwanja wa mazoezi wa
London Colney na kufanya mzoezi wakati sakata la usajili wake kilishughulikiwa.

Nahodha huyo wa Gunners kwa muda mrefu hakufanya siri kuhusu hamu yake ya kutaka kurejea Barca, timu ambayo aliihama akiwa na umri wa miaka 16 na kwenda Arsenal ya London.

Arsenal ilikuwa ikitaka kitita cha pauni milioni 45 ili kumwachia mchezaji huyo na Kocha Arsene Wenger  alimwambia Fabregas hawezi kumruhusu kuondoka.

Lakini klabu hiyo imeona kuwa kuendelea kumzuia kuhama itakuwa ni makosa.

Kwa sasa mchezaji mwingine anayetarajiwa kuondoa katika timu hiyo ni Samir Nasri ambaye anatakiwa na timu ya Manchester City.

Kiungo huyo wa kifaransa mwenye umri wa miaka 24,amebakia mwaka mmoja kwenye mkataba wake, ingawa Wenger amedai kuwa anaweza kuacha kumuuuza.


City inajiandaa kumlipa Nasri paunik 180,000 kwa wiki huku ikiwa imetenga ada ya pauni milionik 25.


Mshambuliaji Marouane Chamakh  alisema: "Ninafikiri wote Cesc na Nasri wanaweza kuondoka."

Wakati huohuo, Arsenal inajipanga kunasa beki wa kati wa Birmingham, Scott Dann ambaye pia ana umri wa miaka 24 kwa da ya pauni milioni 8.

No comments:

Post a Comment