12 August 2011

Tutamfungia Mkurugenzi Arusha-Mbowe

Queen Lema na Richard Konga
Arusha

UONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
umetoa siku 30 kwa serikali kutoa jibu la kuridhisha ambalo litaleta muafaka katika suala la umeya wa Jiji la Arusha vinginevyo watamfungia nje ya ofisi Mkurugenzi wa Jiji jilo, Bw. Estomih Changa.


Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Mwenyekiti wa
chama hicho, Bw. Freeman Mbowe wakati akizungumza na wananchi wa Jiji la Arusha Juu ya uamuzi wa uliochukuliwa na chama hicho kuwafukuza uanachama madiwani watano wa chama hicho.

Bw. Mbowe alisema kuwa wanalazimika kuchukua hatua hiyo kwa kuwa mpaka sasa serikali kupitia Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda hawajatafuta muafaka wa suala la meya wa Arusha kwa
kuwa uchaguzi wake haukufuata sheria, taratibu, wala kanuni za uchaguzi.

Hali hiyo ilizua mtafaruku hadi kusababisha vifo vya watu watatu akiwamo raia mmoja wa Kenya waliouawa na polisi kwa risasi, majeruhi, uharibifu wa mali wakati wa maandamano ya kupinga uchaguzi huo.

Bw. Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alisema: “...Sasa hivi tunachosema ni kuwa tunaelekea kufunga ofisi ya mkurugenzi na kumtoa madarakani, manake serikali haitusikilizi kabisa na mpaka sasa hawasemi kitu cha maana juu ya muafaka huu, natangaza Rasmi.”.

Alisema hatua ya kumfungia nje Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha itakuwa ni fundisho kwa wakurugenzi wengine kwa kuwa mkurugenzi huyo hakutoa ushirikiano kwa mujibu wa sheria na kanuni za majiji na amekuwa akikiuka sheria kwa makusudi.

Naye Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa alisema, 
“Mimi namshangaa waziri mkuu kukatalia hili jambo
wakati ukweli unajulikana, na mpaka sasa ameshindwa kutolea maamuzi hili suala, kwa hali hii taifa linakwenda wapi? Mpaka tuandamane ndio haki ipatikane,” alihoji Dkt Slaa.

Kwa upande wa Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Bw. Goodbless
Lema alisema madiwani watano walivuliwa uanachama kutokana na ukiukwaji wa sheria na chama hicho hakingewavumilia kwa kuwa wamekisaliti.

Bw. Lema amesema kuwa ni wazi kuwa madiwani hao walifuata maslahi binafsi kwa CCM ambapo waliingia katika majadala wa makubaliano bila kuwashirikisha uongozi wa chama, hali ambayo imewafanya kuonekana 'makafiri' wa chama hicho.


9 comments:

  1. Huyu Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha ndio chanzo ya hawa madiwani kusaliti chama chao. Halafu IQ yake ni ndogo sana hana uwezo wa kukalia hicho kiti. Nashangaa Waziri wa TAMISEMI hataki kuteua Mkurugenzi tangu aliyekuwepo (Mr. R. Mbunda) alipoondoka. Huyu aliyepo amekaimu tu hana ubavu wa kuwa full Mkurugenzi na ndio maana wanatumia rushwa zaidi ili kuwarubuni madiwani kwani anajua kabisa Baraza la Madiwani likiamua kumkataa hana chake.

    ReplyDelete
  2. Hatukushangai wewe mchaga ni nia yenu kuivuruga Arusha isipate maendeleo. ole wenu wachaga siku waarusha wakiamua mtakiona. Arusha is for Waarusha,hatuhitaji wabunge wasi Waarusha. nendeni kwenu,mnatusumbua kwa ujambazi na sasa mnatusumbua na siasa

    ReplyDelete
  3. Hiyo ndiyo tofauti iliyopo kati ya Wanasiasa na Wanaharakati. Wanaharakati hawataki kufuata utawala wa sheria wanataka kutumia maneneo ya vitisho. Kama uchaguzi wa Meya haukufuata sheria ni kwa nini wao wasitumie utaratibu wa kisheria kuupinga kwa kwenda mahakamani ili Mahakama iamue?

    ReplyDelete
  4. Wachaga huwa waaribifu kweli hata kwenye familia zao si kwenye siasa tu. Wafukuzeni hao .

    ReplyDelete
  5. wape ukweli hao wachaga warudi kwao...Huwa hawawezekani kuchanyika na watu wengine..Tabia zao ni tofauti kabisa...SASA ONA ARUSHA SI KWAO LAKINI WANANG'NG'ANIA.

    Sijui huwa wakoje?

    ReplyDelete
  6. Kwani hamuoni kwa mkapa? Nyerere alimuamini ni muadilifu,alivyoshika urais tu,mkewe mama wa kichaga akamgeuza huyo mzee kuwa fisadi. hao si watu. watz mtakoma wakisha shika nchi hata huyo Slaa hana usalama akishawawekea mambo sawa. Wataanzisha vikundi vya kuawatisha watu,kuwapiga na kuwaua ili msiwapinge. Eee Mungu tuepushe na hili balaa la wachaga

    ReplyDelete
  7. Hivi wewe Mbowe unadhani kuchukua hatua mkoni ndio suluhu? Kama una hoja vyombo vya mahakama si vipo? kwa nini ukimbilie kumfungia Mkurugenzi. Jamani acheni kujitafutia umaarufu kwa kuzusha vurugu maana mkizusha vurugu tayari vifo vitokea kwa kuwa serikali haiwezi kukaa kimya na kuwaangalia mkijichukulia sheria mkononi. Sasa hivi mmeanza kurudisha maendeleo yetu nyumba kwa vurugu zenu. Huko nyumba mikutano mikubwa ya serikali ilikuwa inafanyika Arusha na hivyo mkoa wetu unapata mapato, sasa imehamia Dodoma. Sio vibaya kugawana rasilimali ya nchi lakini kugawana huko kusitokane na kukimbia mkoa kutokana na ukosefu wa amani. Nendeni mkafanye vurugu kwenu Moshi na sisi tuachieni Mkoa wetu. Mmewarubuni vijana wetu wanashinda juani kuwasikiliza mkimwaga sumu ya chuki. Lakini kumbukeni historia itawahukumu. Slaha naye arudi mkoani kwake akalee wajukuu.

    ReplyDelete
  8. Je, ni kweli kwamba watyu wote waliochangia leo walilenga kuzungumzia wachagga? Au moderator anafanya kazi yake? naogopa!!

    ReplyDelete
  9. Mimi nina washaangaa sana hawa viongozi wetu,hivi kwa nini kila wakati wanapenda kututumia tu hata katika mambo ambayo yanazungumzika?jamani na sisi vijana tumechoka kuumia,ninawashauri kuanza kubadilika tunajua mnatutafutia haki zetu lakini style yenu sasa inaanza kutuboar mimi niliumia sana kwenye maandano yaliyopita sikupata msaada wowote mbunge wangu Lema kanipiga kalenda mpaka nimechoka,sasa mnataka kulianzisha tena.Ah..mtatumaliza kiukweli.

    ReplyDelete