Na Mwandishi Wetu, Morogoro
TIMU ya soka ya wachezaji wa zamani wa Mkoa wa Morogoro 'Moro veterani', imepata viongozi wapya watakaoiongoza kwa mujibu wa katiba yao.Katika uchaguzi
huo, viongozi wengi waliochaguliwa, ni wale waliocheza soka miaka ya zamani.
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Reli Morogoro, Madundo Mtambo, alichaguliwa kuwa mlezi wa timu hiyo.
Walezi wengine wa klabu hiyo ni Aziz Abood, Athuman Lujuo 'High Classic', Frank
Kavemba na Said Afif.
Nafasi ya mwenyekiti ilikwenda kwa Idd Majala 'Gicks' na msaidizi wake ni Hamis Madole 'Mboma'.
Nafasi ya Katibu Mkuu wa klabu ya Moro Veteran ni Abubakari
Fungo, atakayesaidiwa na Yasin Msangi, Mweka hazina ni Abdallah Kondo na msaidizi wake ni Nassoro Lihundi.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Pamba ya Mwanza na Taifa Stars, Amri Ibrahimu, alichaguliwa kuwa kocha mkuu, akisaidiwa na kiungo wa zamani wa African Sports ya Tanga, Ally Jangalu na mshambuliaji wa
zamani wa Reli Morogoro, Omary Mkesa.
Wajumbe waliochaguliwa katika Kamati ya Utendaji wa timu hiyo ni mshambuliaji wa zamani wa Majimaji ya Songea, Simba na Taifa Stars, Godfrey Kikumbizi, kiungo wa zamani wa Reli Morogoro, Boniphace Njohole
na mchezaji wa zamani wa SUA Morogoro, Bony Mapunda.
Pia, katika uchaguzi huo, walimchagua Nickson Mkilanya kuwa msemaji, huku Mohamed Mtono akichaguliwa kuwa, nahodha wa timu.
Viongozi hao wametakiwa kuandaa katiba ya klabu, ambapo watakaa madarakani
kwa miezi sita kuitisha uchaguzi mkuu wa timu hiyo.
No comments:
Post a Comment