05 August 2011

Kashfa UDA yatinga kwa Polisi, TAKUKURU

Godfrey Ismaely,Dodoma na Tumaini Makene


Wabunge Dar es Salaam wachachamaa
*Idd Simba azungumzia kilichotokea

SERIKALI imemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG, Mkurugenzi mkuu wa Makosa ya Jinai (DCI) na Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi wa kina juu ya kashfa ya uuzaji wa Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam (UDA) ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya viongozi waliohusika.


Tamko hilo lilitolewa jana na Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda bungeni mjini Dodoma wakati akitoa taarifa fupi kwa wabunge kabla ya kuendelea na kipindi cha maswali na majibu.

“Suala jingine lililoongelewa kwa hisia kali na waheshimiwa wabunge wengi wakati wa mjadala ni matatizo ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam, Mheshimiwa spika serikali imesikia kilio hicho cha waheshmiwa wabunge,” alisema Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda na kuongeza:

“Kwa sasa, serikali imewaagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi wa kina na kuwasilisha taarifa serikalini mapema iwezekanavyo.”

Waziri Mkuu alisema kuwa mara baada ya uchunguzi huo kukamilika wahusika wote watachukuliwa hatua kali za kisheria.

“Baada ya uchunguzi kukamilika, serikali itachukuwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu kwa wote watakaobainika kuhusika kulihujumu shirika hilo,” alisema Bw. Pinda.

Wakati huo huo wabunge wa Dar es Salaam jana wakiongozwa na mwenyekiti wao Bw. Abbas Mtemvu (Temeke-CCM) walizungumza na  waandishi wa habari mjini Dodoma na kueleza kusikitishwa na tuhuma za ufisadi, ukiukwaji wa sheria, kanuni, taratibu na maslahi ya wananchi katika mchakato wa ubinafsishaji wa UDA.

“Wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam tunamshukuru Waziri Mkuu kwa taarifa na ufafanuzi alioutoa bungeni Agosti 4, mwaka huu, ambapo aliagiza vyombo vya dola hususan, TAKUKURU, CAG na DCI kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma husika, tupo tayari kutoa ushahidi kwa vyombo hivyo pamoja na kushirikiana na serikali ili hatua stahiki zichukuliwe,” alisema Bw. Mtemvu.

Wabunge hao ni pamoja ni Bw. Mtemvu, Bw. John Mnyika (Ubungo), Bw. Mussa Zungu (Ilala), Dkt. Faustine Ndungulile (Kigamboni), Bw. Idd Azzan (Kinondoni), Bi. Eugen Mwaiposa (Ukonda), Bi. Halima Mdee (Kawe), Dkt. Makongoro Mahanga (Segerea) na wengine wa viti maalumu akina Philipa Mturano, Mariam Kisangi, Zarina Madabida, Ester Bulaya, Angellah Kairuki na Fanella Mkangara.

Wabunge hao walisema kuwa pamoja na vyombo vya dola kuagizwa kufanya uchunguzi kwa UDA pia wanatoa wito kwa serikali kuagiza kusitishwa mara moja mkataba batili uliofanyika awali.

“Wabunge wa jiji la Dar es Salaam tunatoa wito kwa serikali kuagiza kusitishwa mara moja kwa mkataba batili na maamuzi haramu yaliyofanyika kwa kukabidhi hisa, mali, uendeshaji wa UDA kwa kampuni ya Simon Group Limited ili katika kipindi hiki cha uchunguzi masuala yote ya kampuni hiyo yaratibiwe na Bodi huru itakayoundwa na kusimamiwa na Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC) kwa mujibu wa sheria zinazohusika,” alisema Bw. Mtemvu.

“Pia tunataka Meya Massaburi, Mkurugenzi wa Jiji, Bw. Bakari Kingobi na watendaji wote wa jiji la Dar es Salaam walihohusika wasimamishwe  mara moja katika kipindi chote cha uchunguzi na kuchukuliwa hatua stahili baada ya uchunguzi huo kwa mujibu wa sheria, kanuni na maslahi ya umma, aida hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa mwenyekiti wa bodi ya UDA, wajumbe wote wa bodi na watendaji wote walihohusika na kashfa hiyo,” aliongeza.

Iddi Simba ajibu tuhuma dhidi yake

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo, Bw. Idd Simba amejibu tuhuma zilizoelekezwa kwake, akisema mchakato wote ulikwenda kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi, akisema serikali ilijulishwa kila hatua.

Huku akitoa madai ya kughushiwa kwa saini ya Meneja wa UDA, Bw. Victor Milanzi kuonesha kuwa mnunuzi alielekezwa kuweka fedha katika akaunti binafsi, Bw. Simba alisema kuwa kutokana na mchakato wa uuzwaji wa UDA kufuata sheria na taratibu za nchi kadri zinavyojulikana, si sawa kusema kampuni hiyo imemilikisha hisa zake isivyo halali wala kuwa imetapeliwa fedha zake.

Akizungumza na Majira juu ya sakata hilo, hasa tuhuma kuwa alipokea sehemu ya malipo ya ununuzi na fedha hizo kwenye akaunti yake binafsi, Bw. Simba alisema kuwa fedha hizo hazihusiani na ununuzi na uuzwaji wa UDA, bali masuala mengine kati yake na Simon Group Ltd.

Bw. Simba ambaye amewahi kuwa kiongozi mwandamizi serikalini, alisema kuwa taarifa za mchakato wote wa uuzwaji wa UDA alikuwa akiziwasilisha serikalini, kwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi na kwa Kampuni Hodhi ya Mashirika ya Umma (CHC).

Alisema kwa mujibu wa kanuni za UDA, madaraka ya uuzaji wa hisa ambazo hazijagawiwa yako mikononi mwa bodi ya wakurugenzi, ndiyo maana bodi iliendelea na mchakato wa kumuuzia Simon Group kwa mujibu wa sheria na mkataba wa mauzo ukafanyika, huku hisa hizo zikilipiwa, hivyo si kweli kwamba ziliuzwa kiholela.

"Mchakato wote ulikwenda kwa mujibu wa sheria na kanuni. Tulikuwa tunapata ushauri wa wanasheria katika mchakato mzima. Hao wanaodhani na kusema kwamba Simon Group imetapeliwa na kwamba haikumilikishwa hisa za UDA kihalali si sawa, kwani uuzwaji ulifanyika kwa mujibu wa kanuni na sheria tunavyozielewa.

"Kibaya kilichotokea ni kwamba baada ya Simon Group kuhalalishiwa ununuzi wa hisa hizo na kulipia malipo ya kwanza ya milioni 285, mwenyekiti (wa Simon Group), Bw. Robert Kisena akataka kuingia katika utendaji wa kampuni na uongozi wake, hata kabla ya AGM (mkutano wa wanahisa wa mwaka).

"Alipokatazwa kufanya hivyo na kushauriwa kwamba asubiri mpaka taratibu zikamilike, akaingia kwa nguvu kwenye majengo ya kampuni (UDA), kinyume kabisa cha taratibu. Hapo ndipo vurugu zilipotokea. Alipohojiwa hajakamilisha malipo ya pili kama ilivyotakiwa alidai kuna pesa alishalipa katika akaunti yangu mimi Idd Simba, kwa mujibu barua aliyoandikiwa na uongozi wa UDA," alisema Bw. Simba na kuongeza;

"Moja, barua ni ya kughushi, kwa sababu Meneja wa UDA, Milanzi hakuandika barua wala hakukuwa na maagizo yoyote ya yeye kulipia hisa zake kupitia akaunti binafsi. Hilo jambo lisingewezekana.

"Lakini ieleweke kwamba muda mrefu kabla ya tukio hilo na katika shughuli ambazo hazihusiani hata kidogo na UDA, zilizotokana na ushauri wa jumla wa kibiashara aliotaka kutoka kwangu, alikuwa anastahili kulipa fedha zangu binafsi. Nilitoa amri ya kulipia katika akaunti yangu, alifanya hivyo kwa awamu tofauti kadri nilivyotoa maagizo."

Akizungumza mbele ya mwanasheria wake, Bw. Simba alipoulizwa iwapo watu hawawezi kuhoji mgongano wa maslahi ulio wazi katika suala hilo, la Simon Group kununua hisa katika shirika (UDA) ambalo yeye ni mwenyekiti wa bodi, huku pia wakati huo huo yeye akitoa ushauri wa kibiashara kwa kampuni iliyotaka kununua UDA, alisema;

"Ndiyo wanaweza kuhoji...lakini sasa mimi si mtumishi wa umma, pale UDA mimi si mwajiriwa. Mimi nauza maneno, natoa ushauri. Ukija kutaka ushauri siwezi kukutalia. Lakini kwenye bodi tulikuwa serious sana. Tatizo ni kwamba mwanzoni sikutilia maanani sana tabia ya Robert Kisena, kwa sababu mimi nilikuwa na hamu sana mzawa achukue UDA, siyo kila kitu nchi hii anachukua mwekezaji mgeni," alisema Bw. Simba.

Alisema kwamba inasikitisha kuona mpaka sasa serikali haijachukua hatua yoyote kuinusuru UDA, akionesha matumaini yake kwa CHC itachukua hatua za haraka kurejesha hali ya kawaida katika shirika hilo muhimu la usafiri Dar es Salaam, pia kwa kamati iliyoundwa kuchunguza suala hilo.

Wakati Bw. Simba akisema kuwa fedha zilizowekwa katika akaunti yake binafsi hazina uhusiano wowote na uuzwaji wa UDA, Bw. Kisena amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kuwa hawakuwahi kuwa na shughuli nyingine tofauti na hiyo ya ununuzi wa shirika hilo la umma.

Akinukuliwa katika moja ya magazeti ya kila siku jana, Bw. Kisena alisema kuwa walilipa fedha hizo katika akaunti ya Bw. Simba, kama sehemu ya malipo ya ununuzi wa UDA, kutokana na maelekezo ya uongozi wa UDA, akisema kuwa anazo nyaraka zinazoonesha hivyo.

20 comments:

  1. THIS IS ABSOLUTELY A MESS TO MR SIMBA AND HIS FRINDS .THE CONSEQUENCE OF OPPORTUNISM IN PUBLIC PROCUREMENT CONTINUE TO REVEAL THE NON UTILISATION OF SENIOR PROCUREMENT EXPERTS.
    ALTHOUGH MR MASABURI IS AN EXPERT IN PROCUREMENT I CAN NOW THINK WHAT HAPPENED TO HIS WAS AROUND SELF INTERESTED BEHAVIOUR AND TOTAL OPPORTUNISTIC CHEATING,GUILE AIMING TO STEAL PUBLIC PROPERTY.
    NOW TANZANIANS WE ARE NOT OF THE 1960'S WATCH OUT MAN!!!!!!NOW YOU ARE IN TROUBLE.ALL OF YOU NOW PLEASE FOR THIS MESS STEP DOWN BEFORE THE REPORT TO RESTORE YOUR REPUTATION.

    ReplyDelete
  2. SASA NATILIA SHAKA HATA USHAURI WA KITAALAMU WA MANUNUZI ANYOTOA MASABURI UMEJAA SHAKA KWANI KAMA MTAALAMU ALISHINDWAJE KUONA UWAZI HAUPO KATIKA SWALA HILI.

    KWELI HATA MNUNUZI AONE AIBU NA HATUKO TAYARI KUSIKIA UPUPU NA USENGE WA HAWA JAMAA ETI WALITAKA MZAWA ANUNUE SHIRKA WAKATI HAWANA UWEZO HAYA NI MAWAZO YA AJABU KABISA NA NI DHAHILI SWALA LA USHINDANI HAPA HALIKUWAPO HUU NDIO UKWELI NA WALIJIUZIA HILI SHIRIKA.
    HAIWEZEKANI LIKAUZWA NAMNA ILIVYO SASA MIMI SASA KAMA MTAALAMU PIA NILIYEBOBEA KATIKA MANUNUZI EBU HUYU SIMON GROUP ATUPATIE HISTORIA YAKE ALIKWISHAFANYA KAZI KAMA ZA UDA WAPI?NA ANA UZOEFU UPI KATIKA MASUALA YA PUBLIC TRASPORTATION.JE ALIWAHI KUWA NA MAGARI/MABUS MBONA HATUYAJUI!!!!!
    JE FINANCIAL HISTORY YAKE IKOJE MAANA NAONA HATA HUU MKATABA WA SASA ANALIPA KWA KUOKOTELEZA PESA !!!!!
    PIA NASHAURI SASA UTARATIBU WOTE UBATILISHWE NA AFILISIWE LIWE FUNDISHO KWA WASANII WANAOCHIPUKIA KWA KASI.

    PIA SASA ITANGAZWE KWA UWAZI NINI KIFANYIKE KUIMARISHA USAFIRI DAR NA NILIFIKIRI HATA MRADI WA MABUS YA KASI YAWE PART YA UDA NA IPEWE MTAJI NA UONGOZI WENYE UADILIFU SIO WASANII.

    WITO WANGU WAKATI WA MCHAKATO MPYA YAITISHWE NA KUOMBWA KU-SUBMIT PROPOSAL ZAO KAMPUNI ZA USAFIRI WA ABIRIA MJINI ZILIZOPO HAPA UINGEREZA KAMA NATIONAL EXPERESS,ARRIVAL,DIAMOND YATUSAIDIE HII ZANA YA UZAWA KATIKA MASUALA YA UENDESHAJI LAZIMA YAZINGATIE UTAAALAMU NA UWEZO KAMA HATUNA UWEZO TUWAACHIE WENGINE WATUSAIDIE HAPA TUNACHOHITAJI NI QUALITY SERVICE YA USAFIRI KWA WANANCHI WA DAR WANAOTESEKA NA USAFIRI WA PRIVATE OPERATORS NA KUZOOFISHA USHINDANI KATIKA BIASHARA HII.
    SERIKALI HISIJITOE KATIKA KILA JAMBO ALIMRADI WATU WAMEKALILI KUBINAFSISHA KWANI LAZIMA MASLAHI YA TAIFA YAZINGATIWE KWA SERIKALI KUWAJIBIKA KWA KARIBU KWA MASHIRIKA YENYE KUGUSA MASLAHI YA WANANCHI WAKE LIKIWAMO HILI LA USAFIRI DAR.

    NAHIMIZA TENA TUSOME NYAKATI NA TUWAOMBE NATIONAL EXPRESS WAMEFANIKIWA VIPI NA WAMEFANYAJE KUENDESHA SHIRIKA LA USAFIRI LA UINGEREZA NATIONA EXPERESS LENYE MABUS ZAIDI YA 1000 NCHI NZIMA.TUWE SIRIASI NA UWE WAKATI WA KUWATUMIA WATU WENYE UJUZI NA UTAALAMU BILA KUJALI USHIKAJI NDILO LIMETUFIKISHA HAPA.

    ReplyDelete
  3. IDDI SIMBA IDDI SIMBA...HUCHOKI TU KUTUIBIA WATZ JAMANI. HIVI NI LINI UTARUDI KWENU NA KUPAENDELEZA ANGALAU TUJUE UNAPAKUSHIKIA KAMA KINA MKONO?? ENZI ZA BEN ULIJIUZULU KWA KASHFA,HIVI LEO UNATAKA KUBISHA KUWA WEWE NI BINGWA WA UFISADI TENA?

    ReplyDelete
  4. Nchi hii sasa hivi ni kama haina serikali, Hata mafuta ya taa wanashindwa kuthibiti,Angalia bei ya sola ambazo serikali ilisema hazitozwi kodi, ni afadhali ukanunue Kenya ambako wanatoza kodi-Wizi gani huu. Hakika kuna siku Mungu atashusha gharika kutuangamiza wote. Madini yanatusaidia nini kama bado tuna matatizo makubwa kama haya. Maisha yamekuwa magumu sana kila kukicha. Serikali ya Kikwete imeshindwa na Inatakiwa wajiuzulu wote. Tumechoka!!

    Mabilioni ya kikwete yamemnufaisha nani?, Ona sasa hivi tunatumia noti mbili tofauti zenye thamani sawa, hii ni kitu gani?, Hata ukienda benki ATM au counter utapewa noti ya zamani na mpya. Maajabu!!!! Huu sio wizi? Angalia Mshahara anaolipwa msomi aliyehitimu chuo kikuu(TGSD), hata kula tu haitoshi, Elimu haina thamani kabisa tanzania. Pesa zilizoibwa BOT zilirudishwa zilifanya kazi gani mbona hatujasikia kwenye baugtet, Mabilioni ya Rada na Ndege Mbovu ya Rais Nani kahusika na amechukuliwa hatua gani? Utasikia tu maneno ya kisiasa kutoka kwa viongozi tuliowapa dhamana ya nchi....tubekabidhi TAKUKURU wanachunguza.....
    Ujinga mtupu!!!!!
    Hatuana imani na Serikaki!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. Pamoja na uchafu alionao inzi na maambukizi mengi ya maradhi anayoiambukiza jamii lakini cha ajabu huanza kwanza kupangusa mikono yake kabla hajala. Ndivyo ilivyo. Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  6. USHAURI GANI IDDI SIMBA ULIOUTOA AMBAO UNA THAMANI YA SHS. MILIONI 285??? NA JE KAMA NI KWELI ULITOA USHAURI WA PESA ZA KIASI HICHO JE ULILIPA KODI ZA MAPATO HAYO TRA ??? UNASEMA ULIMUAMURU KUWA ALIPE KWENYE A/C YAKO BINAFSI MALIPO YA KAZI YAKO LAKINI KUNA HAJA GANI YA KUAMURU MTU AKULIPE KWENYE A/C YAKO WAKATI NI WAJIBU WAKE KUFANYA HIVYO??? IDDI SIMBA NI MLA RUSHWA MKUBWA NA NI FISADI WA SIKU NYINGI ULIWEZA KURUKA MITEGO MINGI LAKINI HUU UNAWEZA KUKUFIKISHA PABAYA.

    ReplyDelete
  7. Haya ndio matokeo ya serikali iliyolala usingizi na hakuna hata kiongozi iliyejuu anayechukuwa hatua.Kila mtu anafanya uozo wake akijua atambiwa ajiuzu na mambo yaishe.lakina kama watu wanaofanya makosa kama haya wange filisiwa mali zao pamoja na kwenda jela basi heshima ingekuwepo kwa viongozi wabovu kufanya mambo ya ajabu kama haya tunayo ona sasa.Tusubiri kidogo tu alafu utasikia kashfa nyingine tena ya ajabu.Sijui hii nchi ina viongozi wa namna gani hata hawaoni aibu na mambo wanayo fanya.Mkiambiwa serikali ni legelege mnakasirika.Hata legelege ina nafuu naona ni ndembendembe.Haya na majenereta yalio nunuliwa yameishia wapi?.Tumuulize waziri mkuu aliyekuwa anayapigia debe.Jamani kila kukicha ni kashfa juu ya kashfa tutafika kweli?.Hata jirani zetu wa Rwanda wanatuangalia na kutucheka maana inaoneka kama ni nchi ambayo viongozi wake wanajifunza mambo ya utawala.Hata hao wanaojifunza utawala wana nafuu kuliko viongozi wetu.

    ReplyDelete
  8. Naunga mkono na "August 5, 2011 2:05 AM" hapo juu. Imani na Serikali hakuna, Natoa mfano wa Somalia ambako kinaeleweka wazi kuwa hakuna serikali angalau kuna sababu. Sasa hapa kwetu miaka 45+ ya uhuru.... Jamani aibu aibu aibu aibu. Jambo moja lililobakia sasa ni wabongo kuamka kutoka usingizini, wabongo tumepiga kura na hizo kura lazima zilipe au sivyo ni mchezo mtupu wabongo wasifikiri itakuja siku Mungu atashusha gharika la hasha hapa sisi wabongo wenyewe tunaendekeza uzembe, ujinga, ufisadi, umeme... ihihiiiiii hebu fikiri kidogo tuu, hivi sasa ni miaka 18 tangu matatizo ya umeme yaanze na hakuna mkakati muafaka wa kukabili jambo hilo halafu unafikiri God will come down from the heaven and sort whoever doing shit? Bob Marley song; "Stand up for your right..." meaning no one will ever come and fight for your right, if you can fight then enjoy the situation.

    ReplyDelete
  9. Nimesikitishwa na kauli ya bwana Simba. Mambo yaliyofanyika UDA ndio yanayofanyika ndani ya serikali yetu. Watu hawana aibu kabisa, wizi umetawala. Njoo ndani ya halmashauri zetu ndo utakuta madudu. Hebu fikirieni watanzania wenzangi, Halmashauri inauza viwanja kwa ajili ya maendeleo ya wilaya husika. Cha kushangaza fedha yote inayopatikana kwa mauzo hayo mkurugenzi na waheshimiwa madiwani wanaanzisha ziara ya kwenda mahali kwa kutumia takriban Tsh. 18 milion. Halmashuri hii ina madeni ya ndani mengi, watumishi vibarua wanadai, shule zilizoko kwenye halmashauri hii hazina vyoo. Wanachukua magari yote ya serikali yaliyopo, posho kwao na madereva wao!!!! Je tutafika? Haya ndio aliyokuwa akiyafanya huyo mh. baada ya hapo akakumbwa na kashfa. Wapo wengi! serikali iamke iwe na meno na itimize inachokitamka kwa vitendo. Milion zaidi ya 18 zingefanya kazi nzuri kwa maendeleo! Inaniuma sana.

    ReplyDelete
  10. Idd Simba tunafahamu kuwa wewe si mtanzania mwenzetu ndio maana unafanya kila hila katika kila sehemu kuhujumu na kuharibu. WEWE RUDI KWENU KWENYE MAPANGA SHAA HUKO NDO PANAKUFAA.
    TUMEKUCHOKA!TUMEKUCHOKA!TUMEKUCHOKA!

    ReplyDelete
  11. Masaburi amezoea kukwapua mali ya umma, na ndiyo maana analalamika sana na kutaka kuibua kashfa za wenzake(wabunge wa dar).
    Kama alijua wabunge hao wana kashfa hizo mbona hakusema kabla.
    Ni Masaburi huyu huyu jamani aliyefilisi mradi wa mabasi ya wanafunzi, na kujenga majengo mengi yasiyo na tija pale nyumbani kwake Segerea, na kule nje ya jiji.
    TAKUKURU tafadhalini mchunguzeni huyu mtu mali alizonazo na source ya income for investing them kama hamkumkamata.
    Hawa ni wezi na mafisadi waliojificha nyuma ya bendra ya Chama Cha Mapinduzi na kusababisha wa-TZ kuchukia CCM na serikali yake.
    Ni wito kwa JK kama mwenyekiti kuibua kashfa ya mradi wa mabasi ya wanafunzi ambao Masaburi aliuua na kujinufaisha binafsi na kumvua Gamba.

    ReplyDelete
  12. Nchi hii inakosa uongozi madhubuti that's why every one is doing what he can! No one abides with rules, this is mess! Leaders wake up, show up the way. Take action for the interest of public. Pse try hard to build public trust. Don't you see people are now opting for opposition leadership.

    ReplyDelete
  13. Yote haya yanatokana na uongozi wa kuifisadi kuanzia ngazi ya juu kabisa inayouvumilia na kukingia kifua matendo ya ufisadi ambayo yamekidhiri kila mahali. Hakuna wa kumnyoshea kidole mwenzie. Uchafu huu utaendelea hadi lini kama hakuna anayechukua hatua madhubuti na kuhakikisha watu wanafikishwa mahakamani na kuadhibiwa. Mambo yamebakia ni kulindana tu, na porojo nyingi.

    ReplyDelete
  14. Majira lete habari mpya, tunasikia Spika wa Zanzibar Kificho kajiuzia nyumba ya serikali Migombani na kuteremsha "palace" lake, kwanza tujue mshahara wake unaomwezesha kuwa na kasri kama lile!

    ReplyDelete
  15. Wanaohusika na wizi huu wachukuliwe hatua. Serikali yetu haiwezi ku behave kama mbwa koko. jamani, this is too much for any human to take! matatizo yote haya lakini kila siku ni habari za wachache kujilimbikizia mali za wizi tu. They all should pay for this. there is no perfect crime. yaani Idd Simba ni mjinga kupita neno lenyewe. He should shut up and wait for his verdict. Eti "niliamuru pesa iingizwe kwenye acc yangu." kwani bila amri wangeingiza kwenye acc ya Saccos fulani huko Ilala? You stole the flippin' money you stupid thief!halafu hukutumia hata maarifa. rudisha pesa zetu na with this serikali itoe tamko pesa hiyo itatumika vipi. We've had it!

    ReplyDelete
  16. Mnunuzi mwenyewe anajulikana kwa utapeli wa miaka mingi. Hakuna lolote la maana hapa. Ni wizi mtupu. Tafuteni historia yake inajulikana.

    ReplyDelete
  17. Akhante sana watanzania kwa kuamka na kuamua kuchukua hatua dhidi ya mapaka shume yanayotuchakachua na kutufanya woote tuonekane WASENGE mbele ya jamii ya kimataifa. nitashangaa kama IDDI SIMBA atakuwa anapita barabarani na asipigwe maweI NYAU mkubwa kabisa alitaka kutuulia viwanda vya sukari kwa kusamehe ushuru importation ya sukari tani 50,000 bado tuna hasira na wewe!

    ReplyDelete
  18. uwamuzi wa uda upo pale

    ReplyDelete
  19. hivi watanzania sisi ni wapole au ni wajinga mana sekta muhimu kama hii kweli inaweza serikari kweli ikashindwa kusambaza mafuta mpaka kuwape watu ambao si wazalendo na nchi yetu.serikari ipo wapi raisi yupo wapi wabunge wapo wapi na sisi wananchi tupo wapi na tunafanya nini.

    ReplyDelete
  20. SERIKALI LEGELEGE HUZAA MAMBO LEGELEGE. ONA SASA KILA MTU ANACHUKUA CHAKE MAPEMA. UKO WAPI RAIS KIKWETE, UMEKAA KIMYA TU. WANANCHI HATUNA IMANI NA SERIKALI YAKO NA CCMAGAMBA YENU.

    ReplyDelete