26 August 2011

Kanisa laijibu serikali kuhusu dawa za kulevya

Na Edmund Mihale

KANISA Katoliki nchini limesema haliridhishwi na utaratibu wa unaotumiwa na serikali kulituhumu kanisa hilo  kuwa linajihusisha na biashara ya dawa za
kulevywa.

Kanisa limetoa kauli hiyo siku siku chache baada ya semina ya wabunge kuhusu athari za dawa za kulevya nchini iliyofanyika hivi karibuni mjini Dodoma.

Semina hiyo ili kuwa ni ahadi ya serikali kutekeleza ahadi iliyoahidi kuhusu kuonesha  mkanda wa video wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya kuonesha hadharani.

Kanisa Katoliki nchini na Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) yalikuwa miongoni mwa taasisi za dini ambazo zilitajwa kutumiwa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu kufanya biashara ya dawa za kulevya.

Taarifa iliyosainiwa na Katibu wa Baraza la Maaskofu (TEC), Padri Anthony Makunde na kusambazwa kwa vyombo vya habari jana ilieleza kanisa hilo linaamini kwamba biashara hiyo itakomeshwa iwapo wahusika wote, pasipo kujali wadhifa wao katika jamii, watakamatwa na kufikishwa mbele ya sheria na si kwa malumbano na kauli zenye utata ambazo malengo yake yanatia shaka.

"Tumepokea habari hizo kwa mshtuko mkubwa kwa kuzingatia hadhi na ushawishi ambao kanisa inao mbele ya jamii pamoja na maadili yanayofudishwa na kusimamiwa na taasisi hiyo.

"Habari hizi zimelisikitisha na kulifadhaisha sana Kanisa Katoliki kwa vile, kwa mujibu wa vyombo hivyo vya habari kauli hiyo imetolewa katika semina ambayo sisi kama Taasisi hatukualikwa au kuwepo hivyo kushidwa kutoa maelezo juu ya shauri hili.

Alisema kuwa kanisa hilo limeshangazwa na taarifa hizo kwa sababu halijawahi kudokezwa ama kushirikishwa juu ya suala hilo ili kutoa ufafanuzi na pengine ushirikiano iwapo ungehitajika.
 
Ni kwa mantiki hiyo, Kanisa Katoliki linasubiri maelezo na taarifa rasmi kutoka mamlaka husika ili liweze kutoa ufafanuzi na pengine ushirikiano iwapo utahitajika.

"Tukio lililotajwa katika magazeti ni Kongamano la Vijana lililofanyika huko Australia 2008. Katika tukio hilo ni kweli kwamba Baraza la Maaskofu liliratibu safari ya vijana na walezi wao waliohudhuria Kongamano hilo.  Kwa mujibu wa taarifa zetu, vijana na walezi waliopitia TEC walienda na kurudi wote. 

"Hatuna taarifa za vijana waliobaki Australia kutoka katika kundi la vijana ambao safari yao iliratibiwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.

"Hata hivyo inashangaza kuona kwamba safari iliyofanyika miaka mitatu iliyopita inanukuliwa katika siku hizi katika hali ambayo Kanisa Katoliki halijawahi kuulizwa, au kuamriwa na mamlaka husika kutoa taarifa zozote kuhusu kundi ambalo safari yao ya kwenda Australia iliratibiwa na Kanisa hili ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Ilieleza kuwa hata hivyo mwaka huu kuanzia tarehe 16/8/2011 vijana wa Kitanzania wakiwa na walezi wao walikuwa Madrid- Hispania kwa Kongamano la aina hiyo. Kilele chake kimefanyika Agosti  21 mwaka huu  kwa Ibada ya Misa iliyoongozwa na Baba Mtakatifu Benedicto VI.

"Ikumbukwe kuwa si mara ya kwanza Kanisa Katoliki kuratibu safari za Kiroho na Kichungaji kwa makundi mbali mbali ya waamini wake.  Ziko safari za kwenda nchi Takatifu, Roma, Fatima, Lurdi na sehemu nyinginezo za Hija.

"Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania limekuwa ikiratibu safari hizo baada ya kujiridhisha kwamba wale wote wanaokwenda kushiriki katika Hija hizo wamefuata taratibu zilizowekwa kikanisa na kuridhika kwamba wanakwenda huko kwa lengo la kuhiji na si vinginevyo.

"Kwa vile si sera ya Kanisa Katoliki kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya, Kanisa Katoliki linaamini kwamba hata ikitokea kwamba mmoja wa mahujaji amebainika kujihusisha na biashara hiyo, atakuwa amefanya hivyo kama mtu binafsi na si kwa jina ama kwa niaba ya Kanisa.

"Kanisa linaunga mkono harakati zote za serikali na watu wote wenye mapenzi mema za kupiga vita biashara hiyo haramu. Hata hivyo taarifa ilisema kanisa halitaunga mkono kauli za jumla jumla zinazotolewa na baadhi ya watu kuhusu dawa za kulevya ambazo pengine zinatia shaka iwapo lengo lake ni kweli kupiga vita dawa za kulevya ama kulichafua, kulidhalilisha na kulipotezea hadhi na mvuto lililonao mbele ya jamii.







16 comments:

  1. kuna mpango mahususi wa kuchafua ukristo tanzania

    ReplyDelete
  2. Shutuma hazikuibuliwa Tz bali Australia. Vyombo vyote, Kanisa na Bakwata wana masuali ya kujibu iwapo wajumbe wao wamekamatwa au kutuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya.

    Vyombo vyote vikuu vya dini nchini vimetajwa katika kashfa hii. Sioni sababu kwa ndugu Anonymous kuwa na wasiwasi, kwani bila ya kuambizana ukweli, Kanisa au Bakwata wanaweza kuendeleza biashara zao na kuathiri jamii na sifa ya taifa letu.

    Wacha sheria ichukue mkondo wake kwa wote waliohusika.

    Hatutaki kurudia uharibifu mkubwa uliofanywa wa kunajisiwa watoto wa kiume na kufichwa na Kanisa kule Ulaya na Marekani.

    ReplyDelete
  3. TUNASISITIZA, WAUMINI NI WATU, HUWEZI UKAOANISHA JINA LA TAASISI NA UPUMBAVU WA MTU MMOJA MMOJA......MTU AKAMATWE NA AFIKISHWE MBELE YA SHERIA YEYE KAMA YEYE NA SI VINGINEVYO. UNLESS OTHERWISE, HIZI KAULI ZA KIPIMBI ZA RAISI NA WASAIDIZI WAKE ZINAONYESHA UPUNGUFU WA AKILI UNAOISUMBUA JAMII YA VIONGOZI WA TANZANIA

    ReplyDelete
  4. Mim naomba ndugu zangu mpunguze jazba,ukweli ni kwamba hata hawa waumin wanamapungufu,ni binadamu km binadamu wengine sasa km kweli padri au shehe amefanya dhambi hiyo wacha sheria ichukue mkondo wake,haina kusema tunadhalilisha kanisa,kwan hata ndan ya makanisa tunajua machafu yanayofanyika,halafu sheria ziko wazi km hao viongoz wa din wameonewa wafuate utaratibu,lakin hatutoogopa kusema eti kwasababu ni kanisa katoliki or whatever,halafu msemaji uliopita si busara kumtukana MTU YEYOTE,ww ni mtu mzima toa maon yenye busara,hapa tunazungumza madawa ya kulevya na kanisa sio Rais NA Wasaidiz wake,kuwa mstaarabu.

    ReplyDelete
  5. Kuna Weakness kubwa sana za kiuongozi ndani ya TZ. Itakuwaje Rais wa nchi na wafuasi wake wanakuwa walalamikaji? watoa majungu wakati sheria zipo? Mkosaji lazima afikishwe kwenye vyombo vya sheria. Sasa kama Rais wa nchi anakuwa mlalamikaji hii inaashiria nini? Ni mpango mahsusi unaongozwa na Rais mwenyewe kulichafua kanisa. Sisi ni watu wazima na tunajua huyo katumwa. Nchi imemshinda anakimbilia kwenye udini sasa.

    ReplyDelete
  6. Mfama maji haachi kutapatapa. Rais wetu kweli nchi imemshinda alianza kwa kishindo sasa anadondoka kwa kishindo pia. Maamuzi yake hayana msimamamo wa dhati, leo atasema hivi kesho atabadilisha hivi. Wakati mwingine alichokisema sicho alichonuia kusema. Habari ya madawa ya kulevya aliisema mahala si pake; swala la waziri Magufuli alilisema kumdhalilisha, jana tena suala la Jairo kamsimamisha kazi. Yapo mambo mengi yanayo ashilia ulegevu na uwezo wa kiuongozi kwa Rais. Kumbe aliyesema hawezi kutoa maamuzi magumu alikuwa sawa kabisa.

    ReplyDelete
  7. Kweli kabisa ile kauli aliyoitoa Mbinga ilikuwa si mahali pake kabisaaaaa. Kwa nahisi aliwaharibia sherehe waliomwalika na nafiri wanajilaumu kwa nini walimwalika. Haiwezekani wewe nimekualika halafu unakuja nisemea mbovumbovu na vitu ambavyo huna uhakika navyo. Najiuliza hivi ingekuwa ndo Mkapa angewaambia vile Mashehe sikukuu ya Eid! Waislamu wangekubali?? si ingekuwa balaaaa!! Washauri wa JK vipi jamani??? Mshaurini vizuri.

    ReplyDelete
  8. Wacheni upumbavu nyinyi kwa nini mnakuwa watumwa wa dini zenu na kupinga kila ukweli unaosemwa ,sasa mlitaka serikali inyamaze kimya huku raia wake wakiangamia kwa manufaa tu ya wachache kwa sababu ni wakatoliki.Tumeona kule inchini Ireland wamefunga ubalozi wote wa vetican kutokana na vitendo vyao viovu vya kulawiti watoto wadogo sasa wale sio makadinal. Kumbukeni Tanzania haina dini wacheni hizi longologo.Zama za kuficha ukweli zimekwisha ,ndugu zetu wakatoliki jisafisheni kwanza kabla ya kutaka utakatifu msio kuwa nao.

    ReplyDelete
  9. Padri Makunde anatuambia:
    "...Kanisa Katoliki linaamini kwamba hata ikitokea kwamba mmoja wa mahujaji amebainika kujihusisha na biashara hiyo, atakuwa amefanya hivyo kama mtu binafsi na si kwa jina ama kwa niaba ya Kanisa."

    Maneno ya Padri hapana shaka yako 'biased'.

    Utapofanya uhalifu na ikatokea ni Muisilamu au una jina linalofanana na waisilamu, tayari dini ya kiisilamu inahusishwa.

    (Corrupt)Padri au Shekhe (asi) wafahamu jumuia zao zitaingizwa na uhalifu iwapo vitendo vyao vimevunja sheria.

    Iwapo tunataka kubaki wakweli, wacha msumeno wa sheria uchukue mkondo wake. Yeyote alehalifu sheria awajibishwe. Ikitokea upo uhusiano na Bakwata au Kanisa, vyombo hivo pia viwajibishwe.

    ReplyDelete
  10. Tunachosema hapa ni kwamba kama mtu amtenda kosa sheria zipo. Sasa mwenye jukumu la kumfikisha mahakani mhalifu ni Maaskofu??? au Shehe???? au Serikali???. Au Serikali iko Likizo inalalamika barabarani??? Hicho ndi tunachokitaka. Si kutuletea kashfa. Tunataka kuona Askofu muuza unga afikishwe Kortini na si kumuonyesha kwenye Video kwa faida ya nani?? Au mnataka tutoe video vya mtume SAW akilawiti ndo mtaamini?

    ReplyDelete
  11. You went too far man!

    Huwezi kulinganisha Mtume SAW na Askofu, Shehe au Kiongozi maarufu wa nchi fulani.

    Mitume yote ni chaguo la Mwenyezi Mungu, Mola wa Viumbe wote, Mfalme wa mashariki zote na magharibi zote.

    Kumlinganisha Mtume SAW na walawiti ni KOSA KUBWA SANA kwa Aliyekuumba wewe na kila kilicho-kuzunguka. Ewe mwana wa adamu, unaombwa ufute usemi wako na urudi kwa Mola wako kwa haraka sana, kwani athari zake ni unimaginable.

    The clock is ticking...!

    ReplyDelete
  12. Kwanza walihamaki na kuruka kimanga wakataka kama kweli wapo wanaoshughulikia mihadirati watajwe. Baada ya kukamtwa mihadirati hiyo live katika majumba ya viongozi wa dini na kutajwa majina yao kama walivotaka wenyewe, sasa wanapiga makelele tena.

    ReplyDelete
  13. Kuna mpango maalumu kuchafuwa ukristo Tanzania kwakuwa imetangazwa kuwa wakuu wa makanisha wameanikwa baada ya kukamtwa madawa hayo majumbani kwao, kwani nyie mlitaka serikali ikuogopeni muendelee na biashara hizo haramu nanyi mnajiita viongozi wa dini na vipi mlitaka mambo haya yafungiwe macho na huku biashara zenu zinaiangamiza nchi na vizazi vyake?

    ReplyDelete
  14. Nyinyi si viongozi wa dini kwasababu viongozi wa dini hwawezi kuwadhuru wananchi. Wacheni ukorofi wenu. Viongozi gani wa dini nyie si bira mkanyammaza kimya kuliko kujianika wenyewe. Nini sasa mnataka. Kila aliyekutikana na mihadarati hiyo apelekwe mahakamani na akithibitisha mkosa atiwe jela kama wanavotiwa jela maharamia wengine. Badawana ulimi wakukemea

    ReplyDelete
  15. Viongozo wa misikiti pia wakikamatwa na mihadirati majumbani kwao na ikithibitishwa kwa hayo vilevile wataanikwa pamoja na hizo bidhaa zao kama walivoanikwa hawa jamaa kwasababu wote watajulikana kuwa ni watu hatari na hawafai kuwa viongozi wa dini. Serikali haidhoofishi ukristo na wanaodhoofisha ukristo ni wale wanaokamatwa na hizo biashara za ndani ya majumba yao wakiwa waislamu au wakristo kwasababu dini hizo zote mbili zimeharimisha biashara hzo.

    ReplyDelete
  16. Nyie acheni ujinga,viongozi wa dini wanalawiti watoto,wanaozesha wasenge sasa kipi cha ajabu kuuza dawa za kulevya? wewe unayetetea viongozi wa dini wakikuambia wakulawiti utakubali ati tu kwa kuwa wao ni wasafi hata wakikulawiti sio dhambi

    ReplyDelete