12 August 2011

Chelsea yaibuka na jezi mpya

LONDON, Uingereza
KLABU ya Chelsea katika msimu huu itatumia jezi tofauti na zile za msimu uliopita zwenye rangi ya bluu.

Kwa mujibu wa gazeti la Sun Chelsea katika msimu huu itakuwa ikitumia jezi zenye rangi nyeupe, njano na bahari.

Kampuni ya kutengeneza na kusambaza vifaa vya michezo ya adidas imezielezea jezi hiyo kuwa ni nzuri,kufurahisha na mtindo mpya.

Jezi hizo zina rangi mchanganyiko huku ufito wa njano ukikatiza kifua.

Lakini jezi mpya inaweza kuchukua muda kuweza kuzoleka ambapo wachezaji kama Frank Lampard na wenzie ambao watakuwa wakivazaa wakiwa ugenini.

No comments:

Post a Comment