Na Grace Michael
MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imezidi kusalimu amri kwa kutekeleza mahitaji ya wafanyabiashara wa mafuta baada ya kubali kukaa nao meza moja
kukubaliana jinsi ya kurekebisha kanuni ya kutathmini akiba ya mafuta yaliyoagizwa kabla ya kubadilisha bei.
Hatua hiyo ya EWURA inakuja siku chache baada ya kutangaza mabadiliko ya bei ya mafuta ambayo ililalamikiwa na kusababisha mgomo wa wafanyabiashara, hatua iliyoilazimisha mamlaka hiyo kuzipandisha upya ndani ya wiki moja, ikitoa sababu kuwa kupanda kwa bei katika Soko la Dunia na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ndio sababu.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa mamlaka hiyo, Bw. Titus Kaguo alisema kuwa mbali na mchakato huo, EWURA inafuatilia kwa karibu uanzishwaji wa mfumo wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja.
“Pamoja na maelezo tuliyoyatoa kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta, imeonekana wadau mbalimbali na umma kwa ujumla wangependa kuona mamlaka ikipitia upya utaratibu wake wa kutangaza bei za mafuta kila baada ya wiki mbili, kwa kuwa taasisi hii imekuwa sikivu na yenye kujali maoni ya wadau wetu tumeamua kuchukua hatua hizo,” alisema Bw. Kaguo.
Alisema kuwa mfumo wa uagizaji mafuta kwa pamoja utawezesha kupata kiasi halisi cha mafuta yatakayokuwa yakiagizwa na kujua bei zake kwa usahihi ili zitumike katika kukokotoa bei kwenye kila kipindi husika.
Hata hivyo, alisema mamlaka hiyo itaendelea kuhamasisha ushindani wa haki katika soko ili kuendelea kuboresha huduma na bei kwa walaji kwa kuzingatia maoni yanayotolewa na wananchi na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kanuni zinazotumika katika usimamizi na udhibiti wa biashara hiyo unaboreshwa.
Hiyo EWURA ni genge la walaji na wala rushwa tu hawana faida yoyote kwa wananchi wa kawaida. Huyo Masebu alikuwa National Housing ikaoza kabisa.Tusubiri nchi iende mrama zaidi ndio tuone viongozi wasio na upeo kama Masebu?
ReplyDeleteEWURA chaja ya KOBE inachaji huku na Huku!!!! hii haifai kabisa; walishusha bei ya mafuta ili wasikike; waonekane wapo; sina hakika kama hii EWURA si ya kindugu naizesheni; miungu watu katika biashara wataididimiza nchi! Wameweka wakili, watuambie kanuni iliyotumika kumteua na atalipwa Bilioni ngapi? Ki hivi kama nchi TUMEKWISHAA!
ReplyDeleteMsiilaumu ewura. Walilazimishwa kufanya hivyo ili bajeti ipite. Walaumu mafisadi na walaghai wanaoendesha nchi hii wakidhani kila mtu ni juha. Huu ulikuwa ujanja wa kuppoza Watanzania ili bajeti ipite. Parliament was fooled and cant do anything. They have been screwed real hard!
ReplyDelete