Na Mwali Ibrahim
MWENYEKITI wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Idd Kipingu, amesema mashindano ya Copa Coca Cola kuitwa mashindano ya kuvumbua vipaji, sio sahihi.Mashindano ya
Copa Coca Cola yanawashirikisha wachezaji wenye miaka chini ya 17, huandaliwa na Kampuni ya vinywaji ya Coca Cola kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), yakiwa na lengo la kuibua vipaji vya mchezo huo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kipingu alisema kwa upande wake mashindano hayo ni ya kujutia vipaji ambavyo vimechelewa kuipatia sifa nchi katika mashindano mbalimbali.
"Kawaida vipaji vinavumbuliwa kwa watoto kuanzia miaka mitano hadi 12, kwa mtoto wa miaka 17 ni wakati wake kulitumikia Taifa katika mchezo husika, kama ilivyokuwa katika nchi za Ulaya," alisema.
Alisema katika mataifa mbalimbali ya Ulaya, wachezaji wenye umri huo huzipatia sifa nchi zao katika michezo husika.
Alisema kama lengo ni kuvumbua vipaji, taasisi husika inatakiwa kuanzisha ligi kwa watoto wadogo ambao umri wao ndiyo unaotakiwa katika kuvumbua vipaji.
Alionya kuwa, watu wanajidanganya kuwa, umri huo wanavumbua vipaji, wakati ni kipindi cha kujutia vipaji.
No comments:
Post a Comment