LONDON, England
TIMU za Arsenal, mabingwa wa Jamhuri ya Czech, Viktoria Plzen na Lyon ya Ufaransa, zimeanza vyema michuano ya kufuzu fainali za Klabu Bingwa Ulaya, baada ya
kuibuka na ushindi dhidi ya wapinzani wao.
Katika mechi hizo zilizopigwa jana kwenye viwanja mbalimbali Ulaya, Arsenal wakiwa kwenye uwanja wao nyumbani, Emirates, waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Udinese ya Italia huku, Lyon ikiibugiza Rubin Kazan ya Russia mabao 3-1.
Mchezo ulioikutanisha Arsenal na Udinese ikicheza bila nahodha wake, Cesc Fabregas, iliichukua dakika nne kupachika bao kupitia kwa Theo Walcott na kufufua matumaini kwa mashabiki wa timu hiyo ambao walikuwa na wasiwasi kama timu yao itafanya vizuri baada ya kukumbwa na majeruhi, huku ikiondokewa na nyota wengi.
Hata hivyo, kikosi hicho cha Francesco Guidolin ambacho kinacheza ligi ya Serie A, kilistahili kuondoka na sare katika mchezo huo kutokana na kukosa mabao mengi, hivyo kujikuta kujiweka katika mazingira mabaya wakati wa mechi ya marudiano itakayofanyika Jumatano ijayo nchini Italia.
Arsenal, ikiwa haina nahodha wake Fabregas, ambaye amejiunga na Barcelona, huku ikimkosa Jack Wilshere, ilikosa kasi katika safu ya mbele kwani Gervinho alikuwa akipambana peke yake.
Nahodha wa mpya Robin van Persie amefungiwa.
Arsenal ilipata nafasi ya kulifikia lango la wapinzani wao mara mbili, lakini mipira iliyolekekezwa langoni mwa wapinzani wao na kugonga mwamba.
Washika Bunduki hao wa London, watamshukuru kipa wao, Wojciech Szczesny kwa kuokoa michomo iliyoelekezwa langoni kwake na Pablo Armero.
Benfica ilitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya FC Twente ya Uholanzi, wakati Sturm Graz ya Austria ilifungana bao 1-1 na BATE Borisov ya Bulgaria.
No comments:
Post a Comment