Na Mwandishi Wetu
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida tiketi za fainali ya Kagame Castle Cup, jana zilizua kasheshe baada ya kutokea vurugu kubwa katika ununuaji wa tiketi hizo kwenye
eneo la Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Tiketi hizo zilianza kuuzwa saa 3 asubuhi, lakini hata hivyo kwa hali ya kushangaza gari lililozibeba lilikuja na tiketi 20 tu za sh. 7,000 kitu ambacho kilileta kizazaa.
Vurugu hizo kulisababisha baadhi ya mashabiki waliofika uwanjani hapo kuumia kutokana na kugombea tiketi hizo.
"Licha ya kuumia lakini lazima niingine kuungalia mpira huu, nimetoka Kibaha kwa ajili ya kuziona Simba na Yanga hivyo sitakubali kupitwa," alisikika mama mmoja aliyeumia na kuchuruzika damu miguuni.
Shabiki huyo alisema ameshangazwa na utaratibu wa kununua tiketi hizo, kwani wauzaji waliamua kuuza tiketi kwa sh. 10,000 kwa nguvu wakati zikiwa ni za sh. 7,000 kwa madai ya kwamba hawana chenji.
Katika mechi hiyo, mashabiki wa timu hizo walianza kufurika uwanjani tangu saa 2 asubuhi kwa lengo la kukata tiketi ambazo hata hivyo za sh. 3,000 hazikupatikana kihalali.
Kabla ya kufika kwa magari ya tiketi baadhi ya mashabiki walikuwa wakiuza tiketi za kulangua ambapo za sh. 3,000 ziliuzwa kwa sh. 5,000, na sh. 5,000 ziliuzwa sh. 10,000.
Michuano hiyo ambayo ilishirikisha nchi za Afrika Mashariki na Kati, ilidhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Castle Lager.
Hili suala la tiketi TFF wanatakiwa kuwa wawajibikaji kwa kila mechi ya simba na Yanga hili tatizo huwa linatokea.Kwanini tiketi ya elfu tano iuzwe elfu kumi?na ya elfu tatu inauzwa elfu tano.Ina maana hakuna polisi wanao angalia usalama hapo uwanjani?
ReplyDeleteJeshi la polisi kwa kushirikiana na TFF wanaweza kukomesha hiki kitendo lakini akili zao zote huwa zinakuwa kwenye pesa tu.