12 July 2011

Redd's Miss Temeke kujifunza uzalishaji bia leo

Na Mwandishi Wetu

WANYANGE wanaowania taji la Redd's Miss Temeke 2011, leo wanatembelea makao makuu ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ambao ndiyo wadhamini wakuu wa
mashindano hayokujifunza uzalishaji wa bia ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kumsaka atakayemrithi Geneveive Mpangala aliyetwaa taji hilo mwaka jana.

Redd's Miss Temeke inatarajia kufanyika Jumamosi kwenye Ukumbi wa Sigara,  Changombe Dar es Salaam, ambapo washiriki 16 kutoka vitongoji vya Kurasini na Chang'ombe, watapanda jukwaani.

Kwenye ziara hiyo, warembo hao watajifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na kampuni hiyo, ikiwemo Redd's.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Kampuni ya BMP ambayo ndiyo waandaaji wa mashindano hayo, Benny Kisaka alisema baada ya ziara hiyo jioni wanyange hao watajumuika na uongozi wa kampuni hiyo katika hafla fupi kiwandani hapo.

Geneveive ambaye pia ni Miss Tanzania 2011 kupitia kanda hiyo, alikuwa mshindi wa Redd's Miss Temeke mwaka jana.

Warembo wa wa mwaka huu watakaopanda jukwaani ni Cynthia Kimasha, Elizabeth Boniface, Eunice Mbuya, Husna Twalib, Irene Jackson na Joyce Maweda.

Wengine ni Lucia John, Mwajuma Juma, Naifat Ally, Naomi Ngonya, Prisca Stephen,  Sasha Seti, Sara Said, Sara Paul na Victoria Mtega.

Wadhamini wengine licha ya TBL ni Vodacom Tanzania ambao pia ni wadhamini wakuu wa Miss Tanzania na Sally Salon.

No comments:

Post a Comment