Na Zahoro Mlanzi
WAREMBO wa Redds Miss Ilala 2011 waliokuwa kwenye ziara ya kimafunzo na Utalii katika Majiji ya Nairobi na Arusha wanarejea leo na watapanda jukwaani
kuchuana katika shindano la kuonesha vipaji kwenye Ukumbi wa Savannah Lounge, Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa mashindano hayo, Jackson Kalikumtima alisema shindano hilo la vipaji litakuwa limefungua mashindano hayo kwa wilaya hiyo.
Alisema warembo wataonesha vipaji vyao kwenye kuimba, kucheza muziki, kucheza ngoma za kiasili, kuchora na kuigiza.
"Warembo watano watakaofanya vizuri zaidi watachaguliwa na majaji kufanya maonesho yao kwenye fainali zitakazofanyika siku ya Julai 29, mwaka huu kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja," alisema Kalikumtima.
Alisema awali shindano hilo lilipangwa liwe la watu maalum lakini hivi sasa wamefungua milango kwa kila mdau wa mchezo huo kwenda kushuhudia shindano hilo na kiingilio kitakuwa ni sh. 10,000.
Akizunguimzia safari yao ya Arusha na Nairobi, alisema imewaongezea upeo na kujiamini maana warembo wengi walikuwa hawajawahi kusafiri hata nje ya Dar es salaam.
"Sasa wana ufahamu wa kutosha baada ya kukutana ana watu mbali mbali walipokuwa safarini na kujifunza kuhusu urembo na kwamba shindano la kufunga mashindano ya Kanda litafanyika Julai 29, mwaka huu," alisema Kalikumtima.
Warembo watakaowania taji hilo ni na Maria Mrema, Jenifer Kakolaki, Priscilla Mschema, Nasra Salim, Diana John na Faizal Ally.
Wengine ni Maryvine Nkezia, Godliver Mashamba, Edna Mnada, Salha Israel, Augostina Mshanga, Lilian Paul, Mariam Manyanya, Williet Rwechungura, Liliam William na Alexia William.
No comments:
Post a Comment