Na Patrick Mabula, Kahama
OFISI ya Katibu Tarafa Kamaha Mjini, mkoani Shinyanga, imemtaka Mwenyekiti wa Serikali wa Kitogoji cha Kasela, Kata ya Malunga, Bi. Bernadeta Mabula, kuludisha
fedha sh. 280,000 alizowatoza wanandoa kama adhabu baada ya kugombana.
Bi. Mabula ametakiwa kurudisha fedha hizo kwa Mzee Elias Chinba ambaye mtoto wake Bi. Photunata Elias, aligombana na mumewe Bw. Juma Hamis hivyo kusababisha vurugu katika Kitogoji cha Kasela, kinyume cha sheria na taraatibu.
Akisimulia tukio hilo, Mzee Nchiba alisema, siku ya tukio saa mbili usiku, waliletewa taalifa kuwa watoto wao ambao wanaishi katika kitongoji hicho wanagombana ndipo waliamua kwenda eneo wanaloishi na kukuta ugomvi huo ukiwa umetulizwa na majirani.
“Baada ya kufika eneo la tukio, tuliwakuta mke na mume wakiwa wamefungwa kamba na makamanda wa sungusungu, tulipohoji kulikoni tukambiwa mwanamke alitaka kumuua mumewe baada ya kutofautiana.
Kutokana na ugomvi huo, Bi. Mabula aliitisha kikao na kututaka tulipe fedha hizo lakini sikuwa nazo, iliamuliwa ng'ombe wangu wawili wauzwe mnadani kwa kiasi hicho cha fedha,” alisema.
Mtendaji wa Kata ya Malunga, Bi. Sesilia Clement, alisema alishangaa kupokea malalamiko ya Mzee huyo ambaye hakutendewa haki kwani suala hilo lilipaswa kufikishwa Serikali ya kijiji.
Kwa upande, Mtendaji wa Kijiji cha Malunga Bi. Josephina Kilimba, alisema hakuwa na taarifa za ugomvi huo bali alipata habari kuwa Mzee Chiba ametozwa sh. 280, 000, baada ya mtoto wake wa kike kugombana na mumewe.
Bi. Mabula alisema, adhabu aliyopewa Mzee huyo ilitozwa kwa kuzingatia utaratibu ambapo katika vurugu hizo, mtoto wake aliwaumiza makamanda wanne wa sungusungu ambao walikuwa wakituliza vurugu hizo.
“Adhabu hii ilitolewa mbele ya kamati ndogo ya sungusungu ambapo Mzee huyu alitakiwa kuwalipa makamanda sh. 80,000 ambao walidai kuumia na kila mmoja alipata sh. 20,000 ambapo sh. 140,000 ni fidia ya simu mbili za Mwenyekiti wa kitogoji na mumewe ambazo zilipotea.
“Mzee huyu pia alitakiwa kulipa sh. 60,000 kwa kosa mtoto wake kugombana lakini hakuwa na fedha hizi ndipo sungusungu walipokwenda kukamata ng’ombe na kuziuza,” alisema.
No comments:
Post a Comment