13 July 2011

Bungeni kwachafuka

*Ni kutokana na mchango wa Kafulila
*Samuel Sitta achangia, awasha moto
*Mwenyekiti aahirisha bunge kiana


Na Gladness Mboma, Dodoma

HALI ya hewa ndani ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, ilichafuka jana baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), Bw. David Kafulila kuirushia
makombora serikali, akidai imekuwa legelege kukusanya kodi.

Mchango wa Bw. Kafulila uliwafanya wabunge wa CCM kusimama na wakitaka kutoa taarifa wakionekana kutoridhishwa na kauli aliyotumia mbunge huyo.

Hali hiyo pia ilimfanya Kaimu Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni, Bw. Samueli Sitta, kushindwa kuvumilia na kulazimika kusimama kutoa msimamo wa serikali kuhusu yaliyokuwa yakisemwa.

Wakati hayo yakiendelea ilionekana wazi Mwenyekiti wa Bunge, Bi. Jenista Mhagama kupata wakati mgumu kwa kushindwa kuwatuliza wabunge ambao sauti zao zilikuwa zikisikika kupitia vipaza sauti na kutoa maneno ya kejeli kabla ya kuruhusiwa na meza.

Bw. Sitta alianza kwa kutoa kauli iliyoonekana kuwatuliza wabunge, pale aliposema kuwa anachofanya Bw. Kafulila ndiyo kazi ya vyama vya upinzani. Alisema kazi ya vyama hivyo ni kubeza kila jambo linalofanywa na serikali, lakini na wananchi wanajionea wenyewe.

Lakini Bw. Sitta ambaye pia ni Waziri wa Afrika Mashariki alionekana kuchafua hali ya hewa zaidi, pale aliposema 'wapinzani wamezoea kuzungumza maneno ya kinafikinafiki', hali ambayo ilizua malumbano zaidi kwa wabunge.

Kauli alizokuwa akitumia kwenye mchango wake Bw. Kafulila kujenga hoja, zilionekana kuwachoma wabunge wa CCM ambao walisimama mara kwa mara kutoa taarifa kwa mbunge huyo, lakini hata pale aliposimama kuendelea na mchango wake alikataa kuzipokea taarifa hizo.

Kauli ya Bw. Kafulila iliyoonekana kuwaudhi wabunge hao, ni pale aliposema kuwa serikali ni legelege, hivyo imeshindwa kukusanya kodi.

Baada ya kutoa kauli hiyo Mbunge wa Nzega, Dkt. Khamis Kigwangwala, alisimama na kuomba mwongozo wa Mwenyekiti wa Bunge, Bibi. Mhagama, akimtaka Bw. Kafulila kufuta kauli hiyo kwa kuwa ni ya kuudhi.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba mbunge afute kauli kuwa serikali ya CCM si legelege na haijashindwa kukusanya kodi. Kauli hii imeniudhi, serikali inakusanya kodi na imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka,” alisema

Baada ya taarifa hiyo, Bi. Mhagama alimtaka Bw. Kafulila kufuta kauli hiyo lakini alikataa kwa maelezo kuwa maneno hayo ni nukuu ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Pia alisema mpaka sasa serikali haijafanikiwa kuongeza kiwango cha ukusanywaji kodi, kwani wakati ikikusanya kiwango juu hicho dola moja ilikuwa sh 1,000, lakini sasa dola imepanda na kufikia sh. 1,600.

Kutokana na maelezo hayo, Bi. Mhagama alisema kuwa hoja ya Bw. Kafulila ina mantiki, lakini haiendani na maelezo aliyokuwa akitoa, kwani ameitumia vibaya nukuu hiyo na kusisitiza Bw. Kafulila kufuta kauli hiyo.

Wakati Bi. Mhagama akieleza hayo, baadhi ya wabunge walikuwa wamewasha vipaza sauti wakipinga maelekezo ya kumtaka mbunge huyo afute kauli, huku wale wa CCM wakisika kukiwabeza wenzao.

Bw. Kafulila alishikilia msimamo wake na hata pale alipopewa nafasi na Bi. Mhagama alisema;

“Nashangaa tunachukua muda mrefu kujadili suala hili. Huu ni ukweli mchungu na nipo tayari kuufia,” alisema.

Baada ya malumbano hayo, Bw. Sitta alisimama na kuwasihi wabunge wa CCM kuwa watulivu, kwani wapinzani kazi yao ni kubeza kila kitu kinachofanywa na serikali.

“Wabunge wa upinzani kazi yao ni kubeza kila kitu kinachofanywa na serikali, lakini sisi tutahukumiwa na wananchi. Siku zote wapinzani mambo yao ni ya kinafikinafiki,” alisema.

Kauli ambayo iliendelea kuibua mizozo ndani ya ukumbi wa bunge.

“Nitatoa mfano, baadhi yao wanadai posho za vikao ni kuwaibia wananchi, lakini wapo baadhi yao walichukua posho hizo miaka mitano iliyopita. Warejeshe posho hizo ndipo wananchi watawaelewa… kila siku wataendelea kuwa wapinzani,” alisema.

Melezo ya Bw. Sitta hayakuweza kuzima mzozo uliokuwepo, kwani wabunge wengi wa upinzani walisimama wakitaka mwongozo wa Mwenyekiti wa Bunge, lakini aliahirisha bunge kutokana na muda wa kikao kumalizika, ndipo wabunge wa upinzani walianza kupiga makofi wakisema huku wakisema; CCJ... CCJ...CCJ"

Baada ya kuahirishwa kwa kikao hicho, baadhi ya wabunge wa upinzani na wa CCM walionekana kunyoosheana vidole huku baadhi yao wakimpongeza Bw. Sitta.

Awali, akichangia hoja ya bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bw. Kafulila alisema inasikitisha kuona kuwa wakati nchi inaelekea kusherehekea miaka 50 ya Uhuru, bado bajeti ya sekta ya afya ni tegemezi.

Alisema hali hiyo inatokana na tatizo la kimtazamo katika serikali na kumtaka waziri asikubali bajeti ndogo na hata ikiwezekana ajiuzulu.

“Leo dunia nzima sisi ndio tuna uwiano mbovu kati ya daktari na wagonjwa. Ni aibu bajeti ya sekta ya afya kuwa tegemezi kwa asilimia 97. Haiwekezani.

“Serikali haitozi kodi. Serikali imeshindwa kukusanya pesa inasikitisha kwa sababu sekta ya afya inahusu maisha ya Watanzania,” alisema.

Bw. Kafulila alisema hazungumzii suala hilo kama mpinzani, bali ni ukweli na kuongeza kuwa serikali inashindwa kuwekeza katika masuala mengine ya afya kutokana na utegemezi.

“Kuna matatizo mengi zaidi ya Ukimwi, lakini kutokana na kuwa tegemezi tunashindwa kuwekeza katika masuala mengine ya kiafya,” alisema.

Mbunge huyo alieleza kuwa watoto wa wabunge na mawaziri wanatibiwa katika hospitali bora ndani na nje ya nchi, lakini watoto wa wanyonge wanatibiwa katika hospitali ambazo hazina hata dawa.

Kutokana na kauli hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Ezekiel Maige, alisimama na kuomba mwongozo wa Mwenyekiti na kumtaka mbunge huyo kutotoa kauli za jumla jumla, ambayo iliibua minong’ono miongoni mwa wabunge wa upinzani na mwenyekiti kusimama na kuwataka wabunge kuheshimu nidhamu ya bunge.

Baada ya maelezo ya Mwenyekiti, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dkt. Mary Nagu, alisimama na kuwataka wabunge kuzungumza kwa nidhamu, akidai kuwa mtoto wake ni daktari Muhimbili na wanaye wanatibiwa katika hospitali za kawaida.

"Baba yangu anatibiwa hospitali ya Katesh na mimi natibiwa huko, Naomba Kafulila ukubali taarifa hii,” alisema.

Hata hivyo, Bw. Kafulila alikataa taarifa hiyo na kuongeza kuwa familia ya mbunge na waziri zinatibiwa bure tena nchi za nje na ndio sababu inawafanya wasiwekeze kwenye sekta ya afya na kumtaka Waziri wakati mwingine asikubali bajeti ndogo.

Bw. Kafulila alisema inawezekana serikali kuwekeza katika sekta ya afya vijijini, kwani nchi hii ni tajiri.

“Tanzania ni nchi tajiri, lakini ni taifa la saba kwa kupatiwa misaada duniani, tunaongozana na nchi zenye machafuko. Haiwekezani kuwa maskini kiasi hiki,” alisema huku akionyesha jarida la Ecomomist.

Akizungumzia bima ya afya, Bw. Kafulila alisema kitendo cha kutopatikana dawa ni utapeli kwa wananchi na kuitaka serikali kujipanga.

23 comments:

  1. HAKIKA BUNGE LETU SAFARI HII NI MWIBA MKALI
    NA LINASTAHIKI SIFA ILLA INABIDI WAWE NA NIDHAMU KIASI MAANA IKIZIDI MNO WATAKUWA BAADHI YAO HAWANA THAMANI KTK JAMII!NI KWELI UPINZANI NI KUKAIDI LAKINI WANACHOKAIDI AU KUPINGA KINA HOJA ZA MSINGI KITU KINACHOTAKIWA NI KWA SERIKALI IYAKUBALI NA KUYATAFAKARI NA KUYAFANYIA KAZI,SIO MRADI LIMECHANGIWA NA UPINZANI BASI HALIFAI NA HATA SASA WABUNGE WA CCM NAO WAMEKUWA WAPINZANI KWA HOJA ZA MSINGI ZA UPINZANI HIVI LENGO LENU NI NINI? KUJENGA NCHI AU KUSHINDANA WENYEWE KWA WENYEWE HAPO BUNGENI?MZEE SITTA NAWE NI MTU
    MUHIMU LAKINI HOJA NYINGINE SIO SAHIHI HUWEZI KUDAI WARUDISHE POSHO ZA NYUMA KWANI SHERIA IKIPITA LEO INAANZA LEO HUWEZI KUDAI HUKO NYUMA LEO SHERIA ZA KUBAKA KIFUNGO CHAKE ZAIDI YA MIAKA 30 HIVI UTADAI WALE WALIOHUKUMIWA KABLA YA HAPO WARUDISHWE TENA RUMANDE ETI WALIFUNGWA KIDOGO?BUNGE NA WABUNGE NI SEHEMU MUHIMU YA KUTUNGA NA KUPITISHA MAMBO MUHIMU NA DIRA YA KUENDESHA SERIKALI LEO KAMA HAMNA NIDHAMU AU MNAFANYA KIHUNIHUNI SIDHANI KAMA INAKUWA SAHIHI PANDE ZOTE ZIWE NA UMAKINI SIO KILA KITU CHA SERIKALI KIPINGWE NA UPINZANI NA PIA SIO SAHIHI HOJA AU USHAURI WA UPINZANI UPINGWE NA SERIKALI

    ReplyDelete
  2. Kwani alichokisema Mh. Kafulila cha kuudhi ni kipi haswa? Ukweli ndio huo watoto wa wakubwa kwa maana ya viongozi wetu hata siku moja hutawaona wakitibiwa kwenye hospitali zetu haswa za serikali. Wenzetu familia zao zinatibiwa nje kwa gharama za serikali kwa mujibu wa sheria walizojiwekea wenyewe. Halafu suala la Mh. Sitta kuwaita wabunge wenzake wa upinzani kuwa ni wanafiki mimi naona sio sahihi kwa sababu wao pia wamechaguliwa na wananchi kama yeye. Lugha aliyotumia Mh. Sitta sio ya kistaarabu kwani hata baadhi ya wabunge wa CCM ni zaidi ya wahuni na ni zaidi ya wanafiki kwani wakiwa nje ya Bunge wanaisema serikali vibaya lakini wakishaingia bungeni wanafyata mkia hata siri nyingi za serikali haswa Ikulu wao ndio wanazitoa. Huo sio unafiki uliobobea? Cha muhimu serikali iwe makini na masuala ya maslahi ya wananchi.

    ReplyDelete
  3. UKweli utabaki kuwa ukweli na utasemwa daima. Ukweli ulio wazi ni kwamba Wabunge wa CCM sasa hivi ndio wamegeuka kuwa WAPINZANI wa WANANCHI kwa kupiga hoja zenye maslahi kwa sisi wananchi wa chini.

    Mbunge mwenye huruma na watanzania huwezi kutetea serikali kutenga 2% tu ya mapato yake na ndani kwaajili ya wizara ya afya! This is no brainer.

    Watanzania tufuatilieni mikutano ya bunge kwa umakini ili 2015 tufanye maamuzi makini, vingievyo tutaendelea kupandishwa vibajaji kama ambulance karne hii ya science na teckonologia. YOUR FUTURE IS YOUR VOTE.

    ReplyDelete
  4. Mheshimiwa Sitta tulikuamini kama mtetezi wa wanyonge kumbe na wewe upo kwa ajili ya vyeo tu, KUKAIMU NAFASI YA PINDA KWA KIPINDI KIFUPI, UNAANZA KUWATUSI WABUNGE WA UPINZANI WANAO USEMEA UMMA, AMBAO NYINYI WABUNGE WENGI WA CCM MMESHINDWA KAMA SI KUKATAZWA. HAKUNA LOGIC YOYOTE YA KUWAITA WABUNGE WEZIO WALIOCHAGULIWA NA WANANCHI NI WANAFIKI, KWA LIPI, MBONA KAFULILA AMETOA DATA, JIBU KWA DATA, MBONA AMEZUNGUMZIA FAMILIA ZA WAKUBWA, JIBU KWA HOJA SIO UNATUSI MDOMO WA WANYONGE UNAOKANDAMIZWA NA SERIKALI DHARIMU INAYOKUMBATIA WEZI NA MAFISADI.. KWA TAARIFA YAKO WEWE NDIO MNAFIKI MKUBWA TENA NDANI YA CCM, UKIWA MJUMBE WA KAMATI KUU ULISHIRIKI KUANZISHA CCJ, IT MEANS ULIKUWA HAUKUBALIANI NA MAMBO NDANI YA CCM, ULIPOAHIDIWA CHEO UKAMTOSA MPENDAZOE, SHAME ON YOU SITTA. NDIO MANA WEZIO WALIKUVUA USPIKA KWA MIZENGWE.

    ReplyDelete
  5. Katika safu ya wanaotaka kugombea 2015 Mh. Sitta naye ana hizo ndoto. Kamwe hazitakaa zitimie kwa sababu yeye anawaona wabunge wenzake ni wanafiki na wahuni je yeye aliyekuwa mstari wa mbele kuwezesha chama cha CCJ kianzishwe wakati yeye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na ni Waziri si mnafiki aliyezidi kiwango? Jamani haya mambo yaangalieni sana msiwe wepesi kuropoka ropoka tu. Mkuki usiwe mtamu kwa nguruwe kwa binadamu uwe mchungu. Mh. Sitta kuisaliti CCM kwa kuanzisha chama cha CCJ naye tumuiteje?
    Si ni afadhali hao wapinzani kuliko hawa wabunge wetu wa CCM ambao kazi yao imekuwa si kutetea tena wananchi waliowachagua ila wanatetea serikali ambayo imeonyesha wazi kutukandamiza na kupora haki za wananchi wake?

    ReplyDelete
  6. ni pale tu wabunge watakapotofautisha kati itikadi zao na maslahi ya nchi....kule zanzibar hakuna u-cuf na u-ccm kunapokuja suala la maslahi ya nchi..lakini huku kwetu wabunge wanaongozwa na uanachama wao bila kujali mantiki na maslahi ya nchi....hata kama chama pinzani kitatoa kitu cha manufaa ya nchi wao watabeza na kukipinga kwa vile tu wao ni tawala..nchi haiwezi kwenda hivi hta siku moja....na kwa mstakabali huu kuna siku mambo yataharibika bungeni na kufuatiwa na nschi nzima kuingia kwenye tatizo....wabinge zindukeni...tumieni nguvu ya hoja na sio itikadi zenu.....

    ReplyDelete
  7. Mhe. Sitta, afadhali mnafiki kuliko msaliti. Na huo unafiki unaosema wewe ni upi, wa Wapinzani kuuteea umma uliwachagua? Mnafiki mkubwa ni wewe uliyejivika ngozi ya kondoo wakati ule wa uspika wako kana kwamba ni mtetezi wa wananchi, kumbe lengo lako ilikuwa kumchafua Lowassa. Ulipoahidiwa kanafasi ka uwaziri unliitekeleza CCJ kiaina. Sasa ni waziri, umeuvaa uhalisia wako wa unafiki na kuanza kuitetea serikali iliyo ICU? Ni vema ukaweka maslahi ya wananchi mbele kuliko nia yako ya Urais 2015. Umeshachafuka sana Sitta- UCCJ umekuumbua Urais ni ndoto ya Ndaria kwako sasa hivi. Heri mnafiki kuliko Msaliti. POLE!!!!!

    ReplyDelete
  8. Mh. sitta sasa umefulia. Lakini si ajabu kujikomba kwa sababu ulishasema kwamba CCM walikuwa mbioni kukufukuza chamani, sasa haishangazi kwamba sasa lazima ufagilie kitumbua chako kwa kula matapishi yako mwenyewe. Lakini kama ulivyotangulia kusema mwenyewe utahukumiwa na wananchi, na hili tumekusikia ukisema mwenyewe, usitunafikie baadaye kama ilivyo kawaida za chama chenu!

    ReplyDelete
  9. tatizo ni dogo hapa,na kubwa pia, inapotokea mbunge wa upinzan ametoa uchambuzi yakinifu,hasa wa maswala ya wananchi kama ya afya,wabunge ccm hawataki kusikia maana hawako pale kutetea wanyonge,wako dodoma kutafuta kula yao.sita ameona watazid kumtenga ndo maana akasema wanafiki,sasa yeye si wanadai ni ccj,huoni kama hiyo ni mbinu chafu jaman.upinzan waendelee hivo hivo kupangua,ndo maana na vyama vingi na upinzan.huduma za afya hapa nchini ni kwa ajl ya wanyonge,wakubwa nje kutibiwa,tena kwa mapesa ya kodi.sasa wajitahd kukusanya hizo kodi ili watibiwe nazo ulaya,na sisi wakesha hoi tutibiwe nazo hapa.wasibishe.kodi hawaokoti.majumba yanapangishwa mikochen,masak kwa madola,na hakula kodi maana nyumba ni zao wakubwa.wakiambiwa wanasema unafiki,ya kweli hayo?

    ReplyDelete
  10. Mh.kama ni kuchemsha umechemsha unawaita wenzako wanafiki waliochaguliwa na wananchi kama wewe sasa hivi tukuelewaje wewe ambaye umechukua mambo yite mawili ya HYPOCRITY AND BETRAYAL si bora hata hawo wenzao ambayo wathubutu hata kutusemea sisi VOICELESS PEOPLE SITA SAHAU NDOTO ZA KUWA RAIS HAPA BONGO LAND FORGET ABOUT THAT THINGS

    ReplyDelete
  11. jamani wabunge wa upinzani nao ni watanzania kama ninyi mlivyo wabunge wa ccm sasa mbona hauelewani ktk maslahi ya wananchi waliowanyonge?ccm ccm ccm mara tatu inatosha sana kuiba mali za wananchi wenu mbumbu zama zenu zimefika waulizen wenzeni walioleta hizo nyodo akina MASHA,DIALLO,BASIL,NA WENGINEOWATAWAPA TAARIFA NZURI SANA

    ReplyDelete
  12. Sita kachemka,lakini kwa hili alofanya jana, anaachika.inaonyesha jinsi anavojipamba sasa hivi.yatosha!

    ReplyDelete
  13. kwanza nasikitika nilipoteza kura yangu kwa ao wanafiki wa ccm,siku zote msomi na mtu makini anatoa hoja kwa data na sio kukurupuka kama alivokulupuka sitta, mh kafulila ametoa hoja kwa data tulitegemea wabunge wa ccm wangejibu kwa data kama alivofanya mh khamisi kingwangala ambeye alijua kuwa kukusanya maela mengi ivo ndo selikali sio legelege, mh kigwangala angepika mahesabu tu madogo wakati huo selikali inakusanya kiasi kile wananchi wake walikuwa wananua sukari na unga kiasi gani kwa kilo na sasa ni kiasi gani kwa kilo ni mahesabu maraisi atakama alipata F ya hesabu form 4

    ReplyDelete
  14. kama kweli wabunge wa ccm wapo makini na wanatutetea sisi wananchi na iyo selikali yao ya ccm sio legelege basi wangeanza kuwadhibiti wote wachachachuaji wa mafuta,kwasababu selikali ni legelege imeshindwa kuwadhibiti wachakachuaji wachache wa mafuta wameona bora kuwaadhibu wananchi wote ambao ni wanyonge kwa kuwaongezea bei ya mafuta ya taa, mimi natoa angalizo wabunge wa ccm wanaweza kupoteza ubunge wao 2015 kwa kuendelea kubariki ukandamizaji unaofanya na selikali kwa wanyonge kwa manufaa ya wafanya biashara wachache,
    waache waendelee kuipigia makofi serikali lakini mwisho wao unakaribia wataangalia bunge kama ambavyo tunaangalia sisi kupitia luninga ikifika 2015,
    NAMPONGEZA MBUNGE WA NKASI "MOHAMEDI-CCM" ambae aliwai kusema awajaenda bungeni kupigiana makofi ya pongezi wakani wananchi wanaitaji huduma kutoka kwa selikali

    ReplyDelete
  15. sita anajikomba kwa ccm yeye aliwai kunukuliwa na vyombo vya habari akinukuu maneno ya mwalimu kuwa ccm sio babayake na anaweza kuihama,leo hii iyo ccm imebadilika nini adi anawambia wenzake wanafiki, sitta ndo mnafiki na msaliti wa mpendazoe,
    ukitaka wapinzani warudishe posho zilizopita ndo waaminiwe na wananchi sisi tunakwambia ukitaka na wewe uaminiwe na wananchi nenda kaendeleze chama chako cha ccj ndo wajue kweli unawatetea.
    sisi wananchi tunawaamini wapinzani na atuwaamini wabunge wa ccm

    ReplyDelete
  16. Wabunge wa CHADEMA na NCCR-MAGEUZI ndiyo wazalendo hawa wengine ni wachumia tumbo tu na kama Sita alivyosema sisi wananchi ndiyo waamuzi ni kweli kwamba Sita kama wana CCM wengine wamechoka sana na wamevimbiwa na posho.watanzania tuamke.

    ReplyDelete
  17. tangia nisikie sita ccj,me nimekuwa nyongo tupu,maana sikutegemea haya.tusubir tena msajili wa vyama atoe ushahid,kama kweli sita alishaingia ccj,halafu anarud tena ccm,kweli ni kunguni tena mbaya,au msumari wa kuchoma kotekote.tulimwamin atuongoze,kama majungu akanushe,na kama kweli ccj tupewe ushahid mapema.anasaliti,anavuruga.hatukutegemea mtu makin vile.km kuhama ahame ataheshimika.kama kukaa akae kimya kama wale mafisad walivo kimya.

    ReplyDelete
  18. Hali kama hii hutokea ktk mabunge strong kama India, Japan, Korea, Armenia! Mabishano huwa ni makali na mwishowe ni ngumi ndani ya Bunge! Sasa hapa kwetu haijazoeleka sababu ya wingi wa wabunge hutoka chama kimoja tu! Hii si ajabu, ndio mwanzo huu, bado tutaona mengi upinzani ukiongezeka bungeni!

    ReplyDelete
  19. Tatizo kubwa la serikali yetu ni pale wanapoambiwa ukweli huwa wakali,Hapa ni jinsi gani inavyo onyesha viongozi walio madarakani hawana hekima wala busara.Kazi yao kubwa ni kula posho tu pamoja na kodi za wananchi.Ni mara ngapi tumeona kwenye magazeti juu ya viongozi mbalimbali ambao wamekwenda India,Uingereza na marekani kwa ajili ya matibabu,Je walalahoi nao waende wapi?.Serikali imeshindwa kabisa kuimarisha huduma za afya,elimu na kathalika na ndio maana viongozi pamoja na famili zao huwa wanakwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu na watoto kwa ajili ya elimu.
    Ni ukweli usiofichika ya kwamba serikali ni legelege na tena hata legelege haitoshi ni ndembendembe maana imeshindwa kukusanya kodi kwa ajili ya misamaha kwa wawekezaji isiyo na kichwa wala miguu.Serikali za wenzetu huimarisha huduma za jamii kwa kutokana na kodi zinazokusanywa.Hebu kawekezeni huko nje alafu muuone kama mtasamehewa kodi.kwanza ukibainika tu unakwepa kodi unaweza kufilisiwa kila ulichonacho.Haya mafisadi nao ndio kama hivyo mnashindwa kuwachukulia hatua kisa mnawaogopa na mkiambiwa ukweli mnakasirika.
    Sasa nafikiri mnataka wananchi pamoja na viongozi wa upinzani wakae kimya na kuwa angalia jinsi mnavyo ingia mikataba mibovu,kodi hamkusanyi,na wala hamuwajali wananchi wenu,Hivi kweli nyinyi mnauchungu na hii nchi yetu?.

    ReplyDelete
  20. Mheshimiwa 6 wewe ndiye mnafiki maana unahangaika na vyeo uko tayari hata kuhama Hama vyama ili mradi upate cheo. Wewe unaufahamu sana unafiki maana wewe ndiye baba wa unafiki unayeweza kutoa Siri HATA za vikao vya mawaziri nje ili uonekane wewe ni mzuri la hasha wewe ni Gamba tu. Mpuuzi mkubwa. Kukaimu tu kiti hicho nongwa je ukipewa kabisa. Wewe ni mfinyu sana wa kufikiri.

    ReplyDelete
  21. INABIDI TUSEME KWA HERUFI KUBWA MHE 6 NIWEWE KWELI???
    KUMBUKA WEWE NI MPINZANI MTARAJIWA|||||||||||

    ReplyDelete
  22. siyo mpinzani mtarajiwa.yeye ni CCJ.kaulize ofisi ya vyama upewe minites zao. kila lakheri!!!

    ReplyDelete
  23. Hongera sana Kafulila pole sana Sitta.Sisi tulikupa kura zetu na ukapewa uspika wa bunge lakini bado wewe ukawa mnafiki zaidi kwa kuuficha ukweli kuhusu sakata la richmond kwa vile ulikuwa una chuki na Lowassa ukaamua kufa nae na kumficha muhusika uamuzi wako leo ndio unatufanya hatuna umeme na matatizo mengine mengine embu pima mwenyewe utuambie wewe ni mnafiki kiasi gani?

    ReplyDelete