23 June 2011

Watakaolangua dawa ya mseto kuadhibiwa

Na Agnes Mwaijega

WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii itawachukulia hatua za kisheria watakaouza dawa ya maralia aina ya mseto zenye nembo ya hati punguzo kwa bei ambayo
hajapitishwa na serikali.

Pia imewataka wananchi kuelewa kuwa  dawa iliyopitishwa na serikali kwa ajili  matibabu ya ugonjwa wa maralia ni mseto.

Akizungumza Dar es Salaam jana Katibu Mkuu wa Wizara Afya na Ustawi wa Jamii, Bi. Blandina Nyoni, alisema  dawa hizo zimetolewa na serikali kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa maralia na hazitakiwi kuuzwa zaidi ya bei elekezi.

"Ieleweke kwamba bei halali ya dawa ya mseto ambayo imepitishwa na serikali ni sh. 1000 na 500, yeyote anayeuza zaidi ya bei anakikuka agizo ya serikali na endapo atabainika atachukuliwa hatua kali," alisema.

Bi. Nyoni alisema baadhi ya maduka ya dawa na vituo binafsi vya kutolea huduma za afya vinakiuka maelekezo yaliyotolewa na serikali.

Aliwataka wananchi kutoa taarifa wizarani endapo watauziwa dawa hizo kwa bei nyingine ambayo haijapitishwa na serikali.

Pia alitoa mwito kwa  wanaotoa huduma wote na wenye maduka ya dawa binafsi kushirikiana na serikali ili kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma iliyokamailika.

Aliongeza kuwa wizara hiyo kwa kushirikiana na Kampuni ya Health Focus Network itaendesha kampeni maalum ya kuwaelimisha wananchi juu ya mapango wa kutokomeza maralia nchini.

No comments:

Post a Comment