23 June 2011

Mtambo wa maji Ruvu waharibika

Na Anneth Kagenda

WAKAZI wa maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na Bagamoyo mkoani Pwani, watakosa huduma ya maji kutokana na mtambo wa Ruvu Chini kuzimwa kwa ajili
ya matengenezo ya siku tatu ambayo yanatarajiwa kukamilika leo.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana na kusainiwa na Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO), Bi. Tedy Mlengu, mtambo huo umezimwa kwa wastani wa saa 24 kuanzia juzi..

Alisema  mtambo huo umezimwa juzi hatua ambayo ilisababisha usambazaji maji kusimama.

Alisema matengenezo hayo yanatokana na kupasuka kwa bomba la inchi 54 eneo la Kerege kwa Kiwete wilayani Bagamoyo.

Maeneo yatakayokumbwa na uhaba wa maji ni Bagamoyo, Mapinga, Bunju, Tegeta, Boko, Mbezi Beach, Kawe, Mikocheni, Masaki, Oysterbay, Msasani na Mlalakuwa.

Maeneo mengine ni pamoja ni Kijitonyama, Sinza, Magomeni, Ubungo eneo la Viwanda, Manzese, Mwenge, Mwananyamala, Kinondoni, Ilala, katika baadhi ya maeneo ya Changombe, Keko, Upanga, Magogoni na maeneo yote ya katikati ya jiji.

Hata hivyo taarifa hiyo ilisema kuwa huduma ya maji katika maeneo hayo inategemewa kurejea katika hali yake ya kawaida kuanzia muda wowote leo.

No comments:

Post a Comment