Na Benjamin Masese
SAKATA la mgomo wa Wahadhiri wa Taasisi ya Ustawi wa jamii Dar es Salaam imechukua sura mpya baada ya Bodi na uongozi kuwafukuza 16 kutokana na tuhuma
mbalimbali ikiwemo kudanganya elimu zao.
Sababu zingine zilizotajwa kuwa chanzo cha kufukuzwa kwa wahadhari hao ni pamoja na kuajiriwa kinyume cha sheria, kufelisha wanafunzi kwa makusudi, ulevi, utoro, matumizi mabaya ya fedha, uzembe, kuajiriwa sehemu mbili, wizi, na kufanya mgomo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kaimu Mkuu wa Taasisi hiyo Bw. Mlwande Madihi, alisema uamuzi wa kuwafukuza wahadhiri ulianza Februari 27 mwaka huu baada ya kuundwa Bodi ya Wakurugenzi.
Alisema kufukuzwa kwa wahadhiri hao kumefanyika kwa awamu tofauti na kwamba awamu ya kwanza ilianza Februari mwaka huu hadi jana.
Alisema kumekwepo kwa matukio mbalimbali ya migomo na makundi mbalimbali yanayotofautina mtazamo na kauli kati ya wahadhiri, wanafunzi, uongozi wa juu wa chuo na uongozi wa serikali ya wanafunzi huku kila pande ikitoa msimamo wake.
Alisema kutokuwepo kwa bodi tangu Septemba 2009 ndiko kulisababisha mambo kufanyika kiholela ikiwa ni pamoja na wahadhiri wasio na sifa kuajiriwa kinyemala huku chuo kikiendeshwa pasipo kufuata taratibu zilizowekwa.
Alisema baada ya bodi kuanza kuchunguza kila mwajiriwa ilibaini mapungufu ya wafanyakazi na kuwafukuza kitendo kilichosababisha wengine kufanya mgomo usiokuwa halali huku wakiwasilisha barua ya madai wakitaka ufafanuzi.
Alisema juzi alipokea barua ya wahadhiri ikimtaka kutoa ufafanuzi juu ya kufukuzwa kwa wenzao bila utaratibu, kuadhibu bila kupewa nafasi ya kujitetea na kutoshughulikiwa nyongeza ya mishahara yao tangu mwaka 2007.
Alismea pia barua hiyo ilihoji ubaguzi katika kazi, matatizo ya maendeleo ya taasisi na kutoa msimamo wao wa kutoingia darasani hadi hapo watakapopata suluhisho la matatizo yao.
Akifafanua zaidi alisema baadhi ya wahadhiri waliofukuzwa walipatikana na makosa ya kuwafelisha wanafunzi kwa makusudi kwa kuwaandikia ripoti mbaya katika matokeo yao pamoja na kutoandaa taarifa za maendeleo ya masomo ya wanafunzi huku wakisingizia kuwa hawakufanya mitihani kutokana na utoro.
Alisema wengine walibainika na makosa ya kutoa taarifa za uongo katika elimu yao, kuajiriwa kinyemela huku wakiwa na umri zaidi ya miaka 40 kutokuwa na uwezo wa kufundisha masomo yanatolewa hapo chuoni.
Alisema baadhi yao wamebainika kuchakachua fedha, kutokuwa na taaluma sahihi inayofaa mahitaji ya chuo na mambo mengine.
"Wahadhiri hao walianza kufukuzwa na bodi mmoja baada ya mwingine baada ya kuchunguzwa na kubainika kuwa na makosa, hadi sasa wamefikia 16 baada ya kuwasimamisha wengine wanne leo (jana) kutokana na kushiriki mgomo na kuwachochea wanafunzi na tunaendelea na waliobaki,"alisema.
Alisema hadi kufikia jumatatu ijayo nafasi hizo zitakuwa zimepata watu wenye sifa kwa kuwa yatari maombi zaidi 200 zimepokelezwa kujaza nafasi hizo.
"Ukikaa na kuwasikiliza wahadhiri malalamiko yao utachukia na kuanza kuwapiga kwa sababu madai yao ni ya kijinga utadhani yanasemwa na mwendawazimu.
Ukiwaleza ukweli wanakataa wanasema hadi kieleweke basi naona wakajiunge na CHADEMA wanaotumia msemo huo,"alisema.
Awali wakizungumza na waaandishi wa habari kwa sharti la kutotaja majina kabla ya kufukuzwa baadhi ya wahadhiri hao walisema hali ya Taasisi hiyo ni mbaya na kwamba kufukuzwa kwao kunatokana na mpango uliokuwa umeandaliwa siku nyingi.
Naye Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Taasisi hiyo Bw. Gerald Simbaye, alitoa mwito kwa wanafunzi kuwa watulivu na kutogawanyika kimakundi kutetea mtu yeyote ili kupata haki yao ya kufundishwa na si vinginevyo.
"Ukiwaleza ukweli wanakataa wanasema hadi kieleweke basi naona wakajiunge na CHADEMA wanaotumia msemo huo,"alisema."
ReplyDeleteKWANINI UTAJE CHADEMA AU KWA VILE WEWE NI CCM Hayo mambo usiyahusishe na vyama vya siasa. mwishowe mtasema wametumwa na chadema
wametumwa na chadema, hiki ni chama cha waharibifu, wanaochochea chuki, hila, roh mbaya, fujo na kupinga jitihada ngumu za kuilinda amani na upendo wa watanzania. Wapo washenzi wa Kimarekani wanaoadhamini hawa chadema ili eti kusababisha kile wanachoita mabadiliko ya mfumo wa kisiasa. Sio wazarendo, tangia historia zao. Watanzania tusifuate mkumbo, leo ukisimama ukauliza wangapi wanajua hicho cha kimeanzishwa lini na nani kwa madhumuni gani, ni watanzania wangapi watakujibu kwa ufasaha? Tuwe makini, tuipende nchi yetu, tusishawishiwe upinga maendeleo, au kufanya migomo inayorudisha maendeleo ya taifa letu nyuma, tuwe makini na wale wanaojiita viongozi wanaharakati wachochezi, yakitokea machafuko, huenda wao wana makazi yao washngton, texas na sehemu kama hizo. Mtanzania kuwa makini
ReplyDelete