08 June 2011

Ukulu: Viongozi wa dini si malaika

Na Grace Michael

SIKU moja baada ya viongozi wa dini kumpa saa 48 Rais Jakaya Kikwete kuwataja kwa majina ya baadhi yao wanaojihusisha na biashara ya dawa za
kulevya, Ikulu imeshindwa kutaja majina hayo, badala yake ikasema kauli hiyo haikutarajiwa kutoka kwa viongozi hao kwa kuwa nao si malaika ama watakatifu hapa duniani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu jana na kusainiwa na Mwandishi Msaidizi wa Rais, Bi. Premy Kibanga, kauli ya viongozi hao wa dini ni ya kusikitisha na haikutarajiwa kutoka kwao.

“Viongozi wa dini ni watu wa kutumainiwa sana katika jamii yeyote, lakini ikizingatiwa kuwa wao sio malaika ama watakatifu hapa duniani, nao wanatumbukia katika majaribu na kujikuta katika vitendo au hali isiyo tegemewa kabisa,” ilisema taarifa hiyo.

Badala ya kutaja majina ya wauza 'unga', taarifa hiyo ilieleza kuwa hivi karibuni wapo viongozi wa dini waliokamatwa kwa rushwa, ngono na kutuhumiwa kujihusisha na vitendo mbalimbali ambavyo ni kinyume na maadili ya jamii na wapo ambao wamekamatwa na watafikishwa kwenye vyombo vya sheria, lakini wapo wanaochunguzwa hivyo kutokana na hayo viongozi hao hawakutakiwa kujitetea kwa kauli nyepesi kwa kumpa Rais saa 48."

Ilisisitiza kuwa kiongozi anayejishuku ajisalimishe mwenyewe na anayeshukiwa na jamii afichuliwe ili afanyiwe uchunguzi na hatimaye sheria ichukue mkondo wake, lakini si kusubiri Rais awataje hadharani ndiyo viongozi hao waanze kuchukua hatua.

Vyombo vya habari jana viliwakariri baadhi ya viongozi wa dini wakimpa Rais Kikwete muda wa saa 48 kuwataja viongozi aliowatuhumu kwa ujumla kuwa wanajihusisha na biashara hiyo haramu.

Taarifa hiyo ilifafanua mambo aliyoyazungumza Rais Kikwete kwenye sherehe ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu John Ndimbo wa Jimbo la Mbinga ambapo Rais Kikwete alitoa ombi la kuwataka viongozi hao kujihusisha kikamilifu katika mapambano dhidi ya biashara na matumizi ya dawa za kulevya.

“Ni tatizo linalozidi kukua pamoja na jitihada za Serikali kupitia vyombo vya usalama kuwabana, kuwawajibisha watumiaji na wafanyabiashara ya dawa za kulevya. Athari zake kwa jamii zinaeleweka, hivyo sihitaji kuzirudia...

“Kila siku kuna watu wanaokamatwa kwa kujihusisha na dawa za kulevya na hiyo inaashiria kuimarika kwa vyombo vyetu vya usalama, lakini inasikitisha sana kuona kuwa biashara hiyo sasa inawavutia hata watumishi wa Mungu.

"Huku sasa tunakoelekea kwa kweli ni kubaya sana.  Nawaomba mtoe uzito unaostahili kwa tatizo hili. Viongozi wa dini mnasikilizwa, Nawaomba kemeeni, onyeni na elimisheni jamii juu ya madhara ya dawa za kulevya, waelimisheni vijana ambao ndiyo walengwa wakuu, waepuke na waache kujihusisha na biashara na matumizi ya dawa za kulevya,” alisema.

Taarifa hiyo iliongeza: “Mtu akikuonya kuwa nyumbani kwako kumeonekana nyoka, huanzi kwa kuuliza kama kweli,  ni wa rangi gani?  Unatakiwa kushtuka na kujiandaa kumsaka kwa nia ya kumwondoa nyumbani kwako hata ikibidi umuue ili asije akaleta madhara makubwa kwako na kwa familia yako, hivyo Rais alikuwa na nia njema katika kulielezea jambo hili, na mwenye nia njema haumbuki,” ilisema taarifa hiyo.

Pia viongozi hao walitakiwa kuweka mikakati na vipaumbele vya kufanyia kazi changamoto hiyo na sio kuahirisha tatizo hili ambalo linazidi kuwa kubwa na kazi ya kupambana na dawa za kulevya haimhusu Rais peke yake bali inamhusu kila Mtanzania.

20 comments:

  1. CHOKOCHOKO MCHOKOE PWEZA BINAADAMU HUTOMWEZA KUNA UKWELI NDANI YA HILI WAPO BAADHI WANATUMIA KIVULI CHA UASKOFU KUFANY
    BIASHARA HARAMU. MAASKOFU MSIKURUPUKE
    FANYIENI UCHUNGUZI KWANZA,RAISI HAWEZI KUTAJA MAJINA KWANI KUNA BAADHI YAO WAPO KTK UCHUNGUZI NA KESI ZIPO POLISI NI AJABU KUMPA RAISI SAA 48.LAKINI NI DEMOKRASIA

    ReplyDelete
  2. JK ACHA USANII WAKO MANENO YAKO ULIYOYATOA HUKO IRINGA KUHUSU BAHADHI YA VIONGOZI WA DINI KUJIHUSISHA NA MADAWA YA KULEVYA ILIKUWA NI MBAYA NA KAMA RAIS UTAKIWI KUZUNGUMZA MAMBO AMBAYO HUNA USHAHIDI NAYO NA UNAVYODAI KUWA ULIKUWA UNAONYA NAYO PIA SI KWELI KWA MAANA RAIS UMECHAGULIWA KULINDA SHERIA KWANZA KWA KUWACHUKULIA WAALIFU HATUA KALI NA SI KUONYA KWANI WEWE SIYO BABU YAO. ULICHOKIFANYA UMEBADILI KAULI KUTOKA KUJIUSISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA NA KUDAI ULIKUWA UKIOMBA TU MSAADA WAO WA KUPIGA VITA MADAWA YA KULEVYA KAMA HIYO NDIO ILIKUWA KAULI HAKUNA MTU YEYOTE MWENYE AKILI TIMAMU ANGEKUPINGA OMBA MSAMAHA KWA VIONGOZI WA DINI WATAKUSAMEHE.

    ReplyDelete
  3. Kama kweli bado kuna viongozi wa dini wanahojiwa na uchunguzi unaendelea hapakuwa na sababu ya Mkuu wa nchi kutamka hadharani kwani tuhuma ni tuhuma zaweza kuwa za kweli au uongo,angekuwa na subira hadi angalau wapelekwe mahakamani,kwani kama alivyosema viongozi wa dini ni watu wanaoheshimiwa sana na jamii uwezi kuwatolea tuhuma bila uthibitisho,ni watu wenye ushawishi sana kwenye jamii na endapo ili halitapata ufafanuzi mzuri madhara yake kwa jamii ni makubwa.Kwanini ili hakuliongelea kwenye baraza la maulidi na akasubiri kwenye sherehe ya kikristo ndio aongelee?ina maana wanao hojiwa ni viongozi wa dini ya kikristo tu?walikamatiwa wapi ,mbona wanapokamatwa watuhumiwa wengine wa madawa uwa inatangazwa kwenye vyombo vya habari?mbona kwa awa haikutangazwa?tunampenda sana raisi wetu tunaomba atoe ufafanuzi ili izi kelele dhidi yake ziache.

    ReplyDelete
  4. Kama kweli bado kuna viongozi wa dini wanahojiwa na uchunguzi unaendelea hapakuwa na sababu ya Mkuu wa nchi kutamka hadharani kwani tuhuma ni tuhuma zaweza kuwa za kweli au uongo,angekuwa na subira hadi angalau wapelekwe mahakamani,kwani kama alivyosema viongozi wa dini ni watu wanaoheshimiwa sana na jamii uwezi kuwatolea tuhuma bila uthibitisho,ni watu wenye ushawishi sana kwenye jamii na endapo ili halitapata ufafanuzi mzuri madhara yake kwa jamii ni makubwa.Kwanini ili hakuliongelea kwenye baraza la maulidi na akasubiri kwenye sherehe ya kikristo ndio aongelee?ina maana wanao hojiwa ni viongozi wa dini ya kikristo tu?walikamatiwa wapi ,mbona wanapokamatwa watuhumiwa wengine wa madawa uwa inatangazwa kwenye vyombo vya habari?mbona kwa awa haikutangazwa?tunampenda sana raisi wetu tunaomba atoe ufafanuzi ili izi kelele dhidi yake ziache.

    ReplyDelete
  5. Raisi ana sources nyingi za information;
    Kuna uwezekano wa baadhi ya viongozi wa dini kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya kama ambavyo wanasiasa/ na viongozi serikalini wanavyoweza kujihusisha nayo.

    La Msingi ni: Kila upande ufanye kazi yake uje na ushahidi wake

    ReplyDelete
  6. NATAKA KUTOA NAGALIZO KWA MAASKOFU WOTE KAMA NDIYO KWELI WAMETOA "ULTIMATUM" KWASABABU KIONGOZI WA NCHI ANALETEWA HABARI NYINGI NA VYOMBO HUSIKA,NA SIO KIMOJA NI VINGI,HIVYO MKUBWA ANAPOSEMA JAMBO INA MAANA KUNA DALILI ZOTE ZA JAMBO HUSIKA.KAMA BABA WA NYUMBA UKIPATA HABARI ZA MTOTO WAKO HUKURUPUKI;KWANZA UNATOA TAHADHARI.HILO NENO NI NYETI SANA,NINAHAKIKA RAIS HAKUKURUPUKA KUSEMA.TAASISI YA DINI NI CHOMBO NYETI SANA NA KAMA YATATAJWA MAJINA KIHOLELA SIJUI ITAKUWAJE KWA HILO KANISA. TUSIROPOKE.

    Bker Souza. DSM

    ReplyDelete
  7. JK HAJAWAHI KUKAMATA HATA KIGOGO MMOJA WA MADAWA YA KULEVYA. LAKINI KUDHIHIRISHA CHUKI YAKE KWA WAKRISTO AMEWATAJA MAASKOFU KAMA NDIO WANAFANYA BIASHARA HII.

    KAMA RAIS ANATAKA KUSAJILI MAHAKAMA YA KADHI NA AISAJILI TU ASITAFUTE KULICHAFUA KANISA.

    ATAISHIA KUPATA AIBU.

    ReplyDelete
  8. Huyo Kachanganyikiwa, hana lolote, Nchi imemshinda, Chama Kimemshinda sasa anaropoka tu kila anachojisikia.
    Hizo kesi za kipolisi siyo majukwaani Kachemsha huyo. Hata kama ni maaskofu tunataka tuone wakikamatwa na kufikishwa maahamani, siyo raisi kuongelea kwenye majukwaa.
    JK. Kachoka, Hana washauri, Hajui aongee nini wakati gani.
    Nchi yetu imeisha.

    ReplyDelete
  9. UNAJUA KABLA HUJASEMA CHOCHOTE LAZIMA UFIKIRIE MWISHO WA NENO HILO UTAKUWAJE,MHE.RAIS HAKUSEMA NI VIONGOZI WA DINI GANI SASA NYINYI MAASKOFU MNAVYOKURUPUKA NA KUMTAKA RAIS AWATAJE MAJINA KANA KWAMBA NYINYI NDIO VIONGOZI WA DINI PEKEE. NAA HII NI KUDHIHIRISHA NAMNA GANI MAASKOFU WALIVYOKUWA NA CHUKI NA RAIS NA NDIO MAANA WANAJARIBU KUTAFUTA KILA SABABU YA KUMKWAZA NA HILI LILIJITOKEZA TANGU KIPINDI CHA KAMPENI MAANA TULISHUHUDIA MAMBO AMBAYO HATUJAWAHI KUYAONA TANGU TUPATE UHURU MAMBO YA NYARAKA MAMBO YA MAHABIRI YA VIONGOZI KUWATAKA WAUMINI WAMCHUHUE MTU WA AINA GANI NA HAYA NI MIONGONI MWA MAMBO YALIYOWAKWAZA WAUMINI WENGI AMBAO WAMEZOEA KUISHI KWA UPENDO BILA YA KUANGALIA DINI ZAO AMBAPO ILIFIKIA STEJI AMBAPO MKRISTO ALIKUWA AKITAKA KUMCHINJA MNYAMA ALIKUWA ANAMTAFUTA MUISLAM AMCHINJE NA BAADAE KUMKARIBISHA KWA FURAHA KABISA LENGO NI KUMUONDOA MASHAKA MUISLAMU ASIJE AKAHISI ANALISHWA VITU AMBAVYO NI HARAMU KATIKA IMANI YAKE NI HII ILIKUWA NI KUTAKA KUIMARISHA ULE MSHIKAMANO NA UNDUGU WA KIBINAADAMU NA NDIO MAANA WATU WENGI MWAKA HUU HAWAKUJITOKEZA KUPIGA KURA HII KUTOKANA NA HAWA VIONGOZI WA DINI KUWAWEKA NJIA PANDA KWAHIYO TATIZO SI JK, TATIZO NI CHUKI ZA VIONGOZI WA DINI KWA JK NDIO ZIONEKANE KILA ANACHOKIONGEA JK BASI NI ISHU KUUBWA MIMI SIJAONA KIBAYA ALICHOKIZUNGUMZA JK.

    ReplyDelete
  10. Usihofu baada ya uchaguzi wa 2015 inchi itatulia Jacob akiwa rais. Sisi wenye akili tunachukua data. Enzi ya Mwl ilifika mahali hapakuwa hata na mswaki lakina haya hayakuepo. Alipo kuja Ali matusi kibao lakini Alipokuja Ben mambo swari EPA ilifanywa watu walipigwa risasi njaa ilikuepo ujambazi usiseme. Sasa kaja Mrisho mitusi na kejeli imerudi ilele. Nchi yetu sote. Uliona wapi wamesemwa viongi wa dini dini moja inakaa pekeyake na kumkaripia raisi. hivi hii diyo state religion pakisemwa DINI tu basi inakuja juu? Mwenye macho hambiwi tazama DINI ndiyo kamba itakatikia HAPO

    ReplyDelete
  11. Ukirusha jiwe kwenye kundi, atakayeguna ujue limempata. Maaskofu mbona mmeguna?

    ReplyDelete
  12. athari ya madawa ya kulevya ni kubwa sana, na si jambo la kulichukulia kwa URAHISI kama hivi, mweheshimiwa RAIS polisi wako wapo na mamlaka unayo kwa mujibu wa KATIBA, huna haja ya kuongea, kama wapo wakamatwe tu

    ReplyDelete
  13. Tatizo la Rais wetu ni mlalamikaji utfikiri ni raia wa kawaida. Rais huyu ni Rais Mtendaji, sasa kwa nini asichukue hatua badala ya kuongea kwa kufumba fumba? Hana maamuzi, hana "guts" za kusema ukweli ulivyo na kuufanyia kazi. Ni msanii, anapenda kuonekana mzuri, yaani hataki aonekane mbaya usoni mwa mtu, ila moyoni ni mtu wa kulipiza kisasi sana sana sana!!!

    ReplyDelete
  14. Mnazunguka tu na kumpamba JK, Sisi hatutaki kelele za majukwaani tunataka utendaji. JK anawajua viongozi wa dini wanofanya biashara ya Madawa ya kulevya tunataka wakamatwe wawekwe ndani siyo longo longo zake.
    Mnamtetea tu kesi ya madawa ya kulevya siyo ya majukwaani ni ya kipolisi.
    Kwangu mimi uwezo wake ni mdogo ndiyo maana hawezi kukamata wahusika anakimbilia tu majukwaa. Hakuna kitu hapa.
    Endeleeni kumpamba kwa tabia zake za kipuuzi.

    ReplyDelete
  15. Ni kweli viongoi wa dii si malaika. Kumbuka walivyopia kelele misamaha ya kodi ilipotaka futwa? Wenajulikana kwa kukwepa kodi na kusaidia wengine kukwepa. Ukitaka kukwepa kodi unaongea no basi watapitisha makontena bila ushuru. Si madawa ya kulevya peke yake, wafutiwe misamaha ya kodi. Shenzy sana hao

    ReplyDelete
  16. Nadhani umefika wakati JK aanze kutawala nchi na apunguze kulalamika. Wananchi tulimpa rai ya kutawala na sio kuwa mtu wa porojo na ulalamikaji. Juzi kawalalamikia mawaziri wake, jana cama chake, leo viongozi wa dini. Tutafika kweli?
    I think this man is not a Presidential material!

    ReplyDelete
  17. huyu mtu hajataja ni viongozi wa dini gani lakini inathihirisha sasa ni jinsi gani hawa wakristo wanavyochukia waislam mna udin sana nyie kwani huyo nyerere na mkapa walikua wanawapa matumizi kila siku? kama kweli kuna viongozi wa dini haijalishi dini gani wanajihusisha na maovu kwa kupitia mgongo wa dini wakamatwe na sheria ichukue mkondo wake tena hapo rais hutakiwi kubembeleza kamata watu, watu wasikie tu fulani yupo jela kwa sabb fulani .umekua mpole sana ndo maana wananchi wako hawakuheshimu hata kidogo yaan watu wanatoa tamko la kukutaka uwataje watu kwa masaa huo ni udhalilishaji kwa rais kama kiongozi wa nchi.ni sawa na mzazi kumwambia mtoto siku hizi umeanza tabia mbaya na mtoto kumwambia mzazi huyo nakupa muda wa siku kadhaa unitajie tabia hizo la sivyo nakuwajibisha,shame

    ReplyDelete
  18. Hata waende marekani mara 1,000,000. Hamna kitu. Akirudi Mume anaenda mke. aliofatana nao wote dini yake. hata aibu haoni.

    ReplyDelete
  19. JK alianza kwa kushambulia misamaha ya kodi inayotolewa kwa makanisa.

    Sasa amedai Maaskofu wanauza madawa ya kulevya.

    Yaani toka ameanza urais wake ni kushambulia wakristo na viongozi wake.

    sisi wakristo tuna marafiki zetu ulaya na usa na ni jadi yetu kusaidiana.

    Kama dini yenu hamsaidiani msitulaumu sisi. Uchungu wa JK dhidi yetu wakristo ni kichekesho.

    Kama anataka kuwa mkristo ampokee bwana yesu. Kuigiza ukristo hakumfanyi mtu awe mkristo.

    Viongozi wa dini ya kikristo wamesaidia hii nchi sana. Bila mchango wetu wa kristo na mataifa ya kikristo kama USA na UK, tanzania haiwezi kwenda kokote

    ReplyDelete
  20. NINYI NYOTE MNAOZUNGUMZIA UDINI NI WAPUMBAVU NA WAJINGA.

    MNADAMU YA KUTAWALIWA NA WAKALONI NA MMESAHAU TAMADUNI ZETU NA KUZIDHARAU NA SASA KWA UJINGA HUOHUO MNAJIFANYA NINYI MNAJUA DINI SANA KULIKO HATA WALIOKULETEENI .

    MPO TAYARI KUFARAKANA KWA TAMADUNI ZA KIGENI(DINI). KWANI DINI SI YAKO, RAISI KAENDA KUHUBIRI PALE IKULU???
    AKIFANYA KOSA LAZIMA AAMBIWE.

    ANAYETAKA MAHAKAMA YA KADHI NI UJINGA. HAYO SIO MAMBO YA SERIKALI NI MAMBO YA DINI NA NCHI YETU SIO YA KIDINI .
    DINI ZINATARATIBU ZAKE NA AZIHUSISHWI NA SERIKALI.SERIKALI KWENYE KATIBA INATOA UHURU WA KILA MTANZANIA KUABUDU ANAVYOTAKA YEYE.

    TANZANIA HAIWEZI JIUNGA NA OIC NA ANAYELETA MIJADALA KAMA HIYO NI HAO VIONGOZI WENYE USWAHIBA WA KIDINI. NI DHAHIRI AWAMU YA PILI NA YA NNE NDIO MMELETA MIJADALA YA KIPUUZI KWA WATANZANIA ETI IJIUNGE NA JUMUIA YA KIDINI, ETI KWA SABABU TUTAPEWA MISAADA MINGI KAMA SHULE,N.K.

    NI WAJINGA KIASI GANI MTU AKUPE KITU BILA KUTEGEMEA FAIDA FULANI KWAKO.WE ULISHAWAHI KUFANYA HIVYO KWENYE MAISHA YAKO? KAMA WAPO NI MOJA YA MILLIONI MOJA YA WATU!!!

    WATANZANIA MNAISHI KWA KUPENDA MISAADA? NI YALE MAKOSA YALIYOFANYWA NA BABU ZETU KUPOKEA HERENI NA SHANGA KWA WAARABU ILI WAWAUZE WATANZANIA WENZETU UTUMWANI!!!
    TUWE MACHO NA VIONGOZI WA SIASA WANAO CHOMEKA MAMBO YA DINI WAKIDAI DEMOKRASIA KUJADILI.
    PIA WALE WANAO SIMAMA MANZESE NA KUSHAMBULIA WAKRISTU KWA KUICHAMBUA BIBLIA NA KUSEMA YESU SIO MUNGU. NA WALE AMBAO BADO SIJAWASIKIA WANAOSIMAMA NA KUSHAMBULIA UISLAMU. NI WAJINGA NA WAPUMBAVU. HAMNA LENGO ZURI MNANIA YA KUMWAGA DAMU YA WATANZANIA KWA KUTUMIA KIVULI CHA DINI.

    KWA UKAWAIDA DINI ZOTE MBILI KWA HALI YA KAWAIDA HAZINA MAMBO YA KIJINGA MNAYOYAFANYA, KUZOMEA DINI NYINGINE,KUJENGA CHUKI NA UHASAMA, KUTUMIA VIFUNGA VYA DINI KWA TAFSIRI ZA MASLAHI YENU,

    MNAO FANYA HIVYO NI DHAHIRI MNAFANYA KWA MASLAHI YENU. NI KAMA OSAMA ALIFUKUZWA KWNEYE NCHI YAKE SAUDIA ARABIA KWA UJINGA HUOHUO WA KUTUMIA KIVULI CHA DINI ETI ANATETEA UISLAMU KWA KUUWA WATU, NA WATANZANIA WENGINE KAMA UPEPO WAMEKUWA WAFUASI WA OSAMA. DINI ARABUNI ZILIZOTULIA HAWANA ITIKADI ZA OSAMA NA WANAMCHUKIA OSAMA KWA TABIA YAKE YA KISHARI NA AMEHARIBU TASWIRA NZIMA YA UISLAMU DUNIANI, WANAMCHIKIA KWA HILO, SASA WEWE MTANZANIA UNAJIFANYA UNAJUAAA NA WENGINE WANFUGA NDEVU KAMA OSAMA .DO!! MTANZANIA WA NAMNA HII UTAACHA UJINGA LINI

    MTAMBUE DINI NI IMANI NA HUWEZI THIBITISHA KWA UTAALAMU WA KISAYANSI KAMA YOTE YALIYOSEMWA NI KWELI AU SI KWELI.

    NA HAKUNA KUHOJI IMANI.ILA KUNAKUFUNDISHWA TU ILI UIFUATE VEMA.WENYE KUHOJI NI PHILOSOFA. WAFUASI WA DINI NI KAMA KONDOO WANAFUATA WANAKOELEKEZWA WAENDE FULL STOP.HIVYO NDIVYO ILIVYO.
    KWA HIYO UCHOKOZI KUTOKA KWENYE MAKUNDI HAYA YA KIDINI HATUONI SERIKALI IKIKEMEA UPUUZI HUO.
    WATANZANIA TUJITAMBUE TULIKOTOKA, TULIPO NA TUNAKOKWENDA.MAHUSIANO YETU SIO YA DINI WALA UKABILA, TULISHAVUKA HUKO, TUANGALIE NANI ANATAKA KUTURUDISHA!!!???
    SIO BUSARA KIONGOZI WA JUU KUYASEMA MANENO YENYE TUHUMA PASIPO KUWA NA UTHIBITISHO.
    KIONGOZI UNAPASWA KUWA NA BUSARA YA KUONGEA NINI NA KWA WAKATI GANI, MAHALA GANI.
    ONA ULICHOKIFANYA SASA, INAONEKANA UNALENGO LA KUCHAFUA DINI FULANI. KWA SABABU BUSARA HAIKUTUMIKA.
    JIFUNZENI BUSARA, NA PIA MSHAURIANE VIZURI KWENYE MATAMKO MNAYOYATOA, ISIWE KAMA MIPASHO AU UMBEA FULANI.MAMLAKA YA JUU MNATAKIWA KWENDA NA FACT. KAMA HATIMAE HUWEZI THIBITISHA HAKUNA HAJA YA KUONGEA.

    SHERIA YA NCHI HIPENDELEI DINI FULANI, YEYOTE ANAYEKAMATWA NA KOSA AFIKISHWE MAHAKAMANI. BOSI MKUBWA WA IMF ALIFIKISHWA MAHAKAMANI KWA NINI TANZANIA??

    UMAKINI PIA HAUPO, KWENYE KAMPENI ULIWASHIKA MAFISADI MIKONO NA KUSEMA WACHAGULIWE KWANI WAO NI WATU SAFI!!! THEN UKASEMA WENGINE NI AJALI ZA KISIASA!!!

    SIAMINI KAMA SERIKALI HAIJUI WAHALIFU WA MADAWA YA KULEVYA!!
    MAREHEMU CHIFUPA ALIKUWA NA ORODHA,MTADAI HAMNA UTHIBITISHO!!! WAKATI WATUMIAJI NA WAATHIRIKA WAPO, WASEME WANAPATA WAPI?

    NAONA NI MCHEZO WA KITOTO PENGINE WANAO YASEMA SANA NDIO WAHUSIKA.

    ReplyDelete