06 June 2011

Taifa Satrs yaangukia pua Bangui

*yajiweka katika mazingira magumu
Na Mwandishi Wetu, Bangui

TIMU ya taifa 'Taifa Stars', jana imejiweka kwenye mazingira magumu, baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1, mbele ya Afrika ya Kati, katika mechi ya
Kundi D ya kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika mwakani iliyopigwa jijini hapa.

Kwa matokeo hayo, kundi D, linaongozwa na Morocco ambayo ina pointi saba sawa na Afrika ya Kati, isipokuwa zimetofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.

Stars inashika nafasi ya tatu ikiwa imebaki na pointi nne sawa na Algeria inayoburuza mkia kwa kuwa sawa na Tanzania,  zikitofautiana kwa mabao ya kufunga.

Afrika ya Kati ilikwenda mapumziko ikiwa inaongoza bao 1-0, bao lililofungwa dakika ya 37, baada ya mshambuliaji wa timu hiyo kuachia shuti kali la umbali wa meta 40 lililomshinda kipa Shaban Kado.

Katika kipindi hicho cha kwanza, Afrika ya Kati, ilifanya mashambulizi zaidi ya kumi, ambapo waliweza kuitumia nafasi moja waliyoipata na kuwafanya kwenda mapumziko wakiwa na bao 1-0.

Afrika ya Kati katika mchezo huo ilikuwa ikipeleka mipira mingi upande wa kulia, na kumfanya beki wa kushoto wa Stars, Idrisa Rajabu kuzidiwa kwa kiasi kikubwa.

Kipindi cha pili, kocha Jan Poulsen aliwatoa John Boko na Mwinyi Kazimoto na kuwaingiza Mbwana Samatta na Athuman Machuppa.

Pamoja na Stars kufanya mabadiliko, Afrika ya Kati iliendelea kufanya mashambulizi mfululizo katika lango la Stars.

Stars ilipata bao lake dakika ya 41, kupitia kwa Samata, ambaye aliachia shuti lililomshinda kipa wa Afrika ya Kati.

Hata hivyo, Stars ilifunga bao lingine kupitia kwa Machupa ambaye aliwapiga chenga mabeki na kipa, lakini mwamuzi wa mchezo huo alilikataa bao hilo.

Afrika ya Kati iliongeza bao la pili na la ushindi dakika ya 45, baada ya mshambuliaji wake kuachia shuti kali lililomshinda kipa Kado.

Stars: Kado, Shadrack Nsajigwa, Idrisa Rajabu, Agrey Morris, Nadir Haroub 'Canavaro', Shaban Nditi, Mwinyi Kazimoto/Athuman Machupa, John Boko/Mbwana Samata, Nurdin Bakari, Nizar Khalfan na Mrisho Ngassa. 

3 comments:

  1. Baadhi wapenzi wa soka wa watanzania walokwepo miaka ya mwanzani mwa 70's na late 80's, watakubaliana kuwa timu hii haitatokea tena golini- omar mahadh bin jabir, 2-leopold taso mukebezi(balimi-kagera), 3-kajole, 4-salim amir (coastal union), 5-jella mtagwa,6-adolf richard,7-omary hussein, 8-hussein ngulungu, 9-peter tino (kipenzi chako), 10-mohammed salim(coastal union), 11-thuweni ally!!!!.....ongezea na nidhamu ya hali ya juu!!!

    ReplyDelete
  2. Huyo ndiye poulsen wenu. Mtamkumbuka Masikio Makisio maana kwa sasa hata umiliki wa mpira uwanjani kwa Taifa stars umepotea au ameondoka nao Maximo.
    Babu kaja kutufia huku bongo na tusitegemee maajabu kwa kiwango kibovu kinachooneshwa na Taifa Stars.
    Hongera kwa vijana wa U-23 ijapokuwa wana kocha dhaifu lakini wanajitahidi.
    Tunaomba mtuondelee haraka huyo Julio arudi kufundisha timu za ligi na sio timu ya Taifa.

    ReplyDelete
  3. Mshikaji hapo juu umenimaliza, babu kaja kutufia ha ha ha yaani tupate kazi ya kurudisha box kwao Denmark? aliponimaliza ni kumchagua Machupa na Banka? nikasema tumevamiwa sasa ngoja tuone, ukweli sasa ndo tumejua Maximo walikuwemo

    ReplyDelete