09 June 2011

Mwarobaini wa watumishi hewa watajwa

Na Mwandishi Wetu

ILI kubaini watumishi hewa serikali imepanga kufanya sensa kwa kuandaa siku maalumu ya kulipa mishahara ya watumishi wa umma kupitia
dirishani.

Utaratibu huo ulitangazwa mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mustapha Mkulo, wakati akisoma Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012, bungeni jana.

"Serikali itafanya sensa maalumu kwa kuandaa siku ya kulipa mishahara dirishani tena kwa kushtukiza," alisisitiza Bw. Mkulo.

Mbali na hatua hiyo, alisema serikali itaendesha ukaguzi kwa malipo ya mishahara kupitia Ofisi ya Mkaguzi wa Ndani.

"Ili kudhibiti matumizi ya fedha serikali itahakikisha mifumo inafuatwa," alisisitiza.

Kuhusu miradi ya maendeleo, alisema itaratibiwa na kitengo cha Mkaguzi wa Ndani ili kuhakikisha miradi inaendena na thamani iliyokusudiwa.

Akizungumzia maslahi ya watumishi, Bw. Mkulo alisema serikali itazidi kuimarisha utaratibu wa malipo ya mishahara na likizo kwa wakati.

Hatua nyingi iliyotangazwa na Bw. Mkulo ni ya kuhakikisha mafao na pesheni ya wastaafu inalipwa kwa wakati. Aliongeza kuwa serikali itatoa mafunzo kwa watumishi wa hazina ndogo watakaokuwa wanashughulikia malipo ya watumishi wa hazina ndogo.

2 comments:

  1. Mbona serikali inachelewa kusimamia ili kuzibiti hii mishahara hewa.......? kila siku ni kulalamika tu au ninyi vigogo ndiko mnako neemekea.? "TUNATAKA UTEKELEZAJI"

    ReplyDelete
  2. Hizi zote ni hadithi za abunwasi. Mimi sioni ni kama watumishi kulipwa dirishani ndio kutadhibiti watumishi hewa. Ipo mianya mingi tu inayoweza kutumiwa mfano kuna watumishi wako masomoni, wagonjwa au wako kwenye miradi nje ya nchi. Sasa huyu mtumishi aliyemasomoni mkoa mwingine au nje ya nchi naye utamtaka aje Dar es salaam, mwanza au Arusha kupokea mshahara dirishani? Hii siku ya kupokea mishahara dirishani maana yake siku hiyo watanzania wengine hawahudumiwi siku hiyo maanake itakuwa kama holiday, watumishi wote hawako wako kwenye mishahara. Pia tutakuwa tunachochea majambazi kuwasubiri watumishi hawa hasa wanaofanyia kazi maeneo kuviziwa na majambazi na kuporwa mishahara yao. Nadhani tatizo letu hasa ni ukosefu wa upeo wa kufikiri. Bado upeo wetu wa kufikiri ni ule wa enzi za ujima au enzi za nuhu. Wakati wenzetu duniani kote wanatumia sayansi na tecknolojia kuweka mifumo ya kudhibiti malipo hewa sisi bado tunaendekeza mbinu za kiujima. Hivi kwanini serikali haiwezi kuweke unique identifier namba kwa kila mfanyakazi ambayo anaitumia maisha yake yote ambayo inahifadhi kumbukumbu zake zote, na namba hiyo hiyo mtumishi akaitumia hata kama akiajiriwa sekta binafsi. Hii itakuwa kama passport yake ya kusafiria. Halafu chombo kingine kinakuwa na kazi maalumu ya kukagua usahihi wa taarifa na kunakuwa na maswali maalumu yanayoulizwa kwa kushitukizwa kupitia mtandao wakati mtumishi huyu ana up date kumbukumbu zake kila mwaka. Ipo mifumo ya kiteknolojia kama commino inaweza kusaidia mno kudhibiti vitu kama hivi. Jamani husisheni wataalamu kuwasaidia kuweka mifumo ya kisayansi tuachane na njia za mazoea.

    ReplyDelete