21 June 2011

Mgogoro wa umeya Arusha wamalizika

*CHADEMA, TLP wakubali kugawana unaibu meya

Na Queen Lema, Arusha 

HATIMAYE mgogoro wa uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Jiji la Arusha baina ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutomtambua
Meya wa jiji hilo, Bw. Gaudence Lyimo (CCM) umemalizika jana kwa makubaliano maalumu ya kugawana madaraka.

Katika Makubaliano hayo, Bw. Lyimo ataendelea kuwa meya na nafasi naibu wake kuchukuliwa na vyama vya CHADEMA na TLP kwa nyakati tofauti, ambapo Diwani Estomih Mala kutoka CHADEMA atashika nafasi hiyo kuanzia sasa hadi mwaka 2014 atakapomwachia nafasi Diwani wa TLP, Bw. Michael Kivuyo.

Mgogoro huo ulitokana na chama hicho kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi wa meya, ambapo ilielezwa kuwa madiwani wa vyama viwiki walifanya uchaguzi bila kuishirikisha CHADEMA na kupata diwani kutoka CCM, na diwani pekee wa TLP kuwa naibu wake.

Kutokana na mgogoro huo CHADEMA walipinga uchaguzi huo kwa maandamano yaliyosambaratishwa na polisi na watu watatu, akiwamo raia mmoja wa Kenya, kuuawa kwa risasi na hadi sasa viongozi kadhaa wa chama hicho wanakabiliwa na kesi ya jinai katika Mahakama ya Arusha.

Lakini sasa hayo yote yamepita, pande zinazohusika zimejirudi na kufikia makubaliano yaliyosababisha wahusika washikane mikono kwa furaha.

Akizungumza katika kikao na madiwani wa Halmashauri ya Manispaa  ya Arusha, Mwenyekiti wa Kikao cha Usuluhishi, Bw. Kivuyo   alisema kuwa wamefanya usuluhishi kwa miezi minne mfufulizo   ambapo vyama hivyo vitatu vilikuwa vinakutana ili kumaliza mgogoro huo ambao umedumu tangu mwishoni mwa mwaka jana baada ya kutangazwa kwa Meya Lyimo.

Bw. Kivuyo alisema kuwa madiwani hao wanalazimika kuungana na  kuachana tofauti zao, kwani iwapo migogoro hiyo itaendelea ndani ya halmashauri hiyo, ni wazi kuwa mipango ya maendeleo itadidimia na kushindwa kufikia malengo.

Alisema kuwa kwa sasa tayari Meya wa Jiji anatambulika kama meya halali kulingana na sheria na taratibu za nchi.

"Sasa mgogoro umeisha na sisi kama madiwani wa vyama upinzani tunatambua Meya ni Bw. Lyimo na pia napenda kuwaambia wananchi  wa Manispaa ya Arusha kuwa kuanzia sasa Naibu Meya wa Jiji la  Arusha ni Bw. Estomih Mala kutoka upinzani ambaye atadumu katika nafasi hiyo hadi 2014," alisema  Bw. Kivuyo.

Hata hivyo, Bw. Kivuyo alisema kuwa kutokana na kikao cha usuluhishi kilichokaa, wameamua kuweka utaratibu mpya kutoka na mambo yaliyojitokeza

Alisema kuwa hali hiyo ya vyama hivyo kuungana kutaleta   mafanikio makubwa ndani ya jiji la Arusha kwa kuwa kwa sasa viongozi hawatasusa vikao na hivyo malengo halisi ya maeandeleo yatajadiliwa kwa kina na viongozi hao.

Alisema kuwa viongozi hao wameamua kuwa na umoja na kusahau machafuko yaliyotokea mjini hamo na kufanya mji huo kuwa na historia mbaya, lakini sasa wamepata viongozi halali wanaotambulika kisheria kulingana na kanuni za muongozo kuhusu viongozi wa jiji hilo.

"Mimi nimefurahi sana kwa sisi vyama upinzani na chama tawala  kuungana na kwa hali hii, basi naweza kusema kuwa yale machafuko yaliyotokea hayawezi kutokea tena na badala yake sisi kama  viongozi tutakuwa na umoja na tutaweza kutatua kero za wananchi  wa jiji la Arusha, hususan katika vikao vya mabaraza ya madiwani," alisema Bw. Lyimo.

Diwani wa Kata ya Elerai, Bw. John Bayo alisema kuwa mgogoro unapokuwepo baina ya chama kimoja na kingine hauna tija kwa kuwa lengo halisi la kupewa nafasi ya kuongoza ni pamoja na  kuwatatulia wananchi kero zao.

Bw. Bayo alisema kuwa mgogoro huo uliodumu tangu Januari mwaka huu umekuwa na madhara makubwa kwao kwa kuwa haukuwa na umuhimu kwa baraza hilo hata kwa kujadiliana masuala mbalimbali ambayo  yanawalenga wananchi hususani wale wa chini.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Bw. Raymond Mushi alisema kuwa suala  hilo ambalo lilileta madhara makubwa kwa wananchi wa Manispaa ya  Arusha halitarudiwa tena na badala yake wameweka mikakati  maalumu kuhusu kufanya jiji liwe na amani.

Naye Mbunge wa Jimbo la Arusha Bw. Goodbless Lema akizungumza kwa njia ya simu na Majira alisema kama uchaguzi huo umefanyika kwa haki basi kila kitu kiwe kwa haki, usawa na uwazi.

15 comments:

  1. Hii ndiyo nguvu ya watu, bila hii CCM wangefanya wanavyotaka. Tunataka kuona sasa kwamba jiji la arusha linakuwa safi, barabara zinajengwa na ukandamizaji wa wafanyabiashara ndogondogo unamalizika

    ReplyDelete
  2. pamoja na hay yote mmeshinda udiwani?mnajitia tia tu hamna lolote mnalolijua zaidi ya ubishi sasa kipo wapi simlitaka mwenyekiti awe chadema limewashuka hilo ndio mjue sasa huo ni mwanzo tu ccm hamuiwezi na sasa wapo kimya wanajifanya kulumbana mtoana motowake wamewaachia mtu mmoja tu mpambane nae nyie mpo 48 anawatoa jasho ikiingia tim nzima itakuwaje?

    ReplyDelete
  3. HIZO NDIYO SIASA ZA TANZANIA. WANANCHI LAZIMA TUWE MAKINI NA WANASIASA. HAYA SASA NDUGU ZANGU TULIOUMIA NA KUPATA MAJERAHA KATIKA MIILI YETU TULIKUWA TUNASHABIKIA NINI? KWA NINI JAMBO HILI HALIKUFANYWA MAPEMA ILI KUEPUSHA VIFO VYA WENZETU VILIVYOTOKEA? LAKUAMBIA CHANGANYA NA LAKO.

    ReplyDelete
  4. huna lolote we lema umeona eeeeeeeeeeeeee jasho limekutoka utwaambia nn wapambe wakoooooooooo meya ulikuwa unamkataa mpa kwenye vilio sasa utampigia goti?maana kumuwajibisha huwezi huna uwezo huo kikatiba wala kisheria mkiambiwa moto wenu ni wakifuu mnabisha tunawasubiri 2015

    ReplyDelete
  5. Wachangiaji onyesheni basi uzalendo na upendo? Kwani kuna ubaya gani ndugu walio na ugomvi ikafika siku wakapatana? Hii ndiyo demokrasia jamani. Lipi la ajabu kama watu wamepatana. Mbona mke na mume au ndugu waliozaliwa tumbo moja wanakuwa na ugomvi wa muda mrefu kiasi cha kutaka kuuana lakini inafikia muda wanapatana. Hivyo hivyo mgogoro huu wa Umeya umechukua sura mpya wameamua kupatana na kuwa kitu kimoja ili kujenga Jiji la Arusha. Sasa hapa kuna ubaya gani? Tatizo la wakereketwa wa Chama cha Majambazi ni mavuvuzela filimbi mdomoni nyingi sana hawana upendo wowote ndio maana wanajilimbikizia mali wachache huku walio wengi wanaumia kwa kutomudu gharama za maisha. Wanapenda ugomvi sasa kuna mapatano hawaridhiki watu kupatana. Tafadhali geukeni si wakati wa mapambano dhidi ya hali ngumu ya maisha.

    ReplyDelete
  6. Haya sasa Mchague nyie CHADEMA NI CCM gani?

    Mmejidai kuwatukana CUF haya kiko wapi?

    Nyie wafuasi wa MAASKOFU MASHOGA kaoleweni basi. Mwenzenu Slaa kakimbia hayo hayo kanisani, bado nyie mnajipeleka peleka!

    ReplyDelete
  7. by MZALENDO HALISI

    JAMANI JAMANI JAMANI!!!!!!!!!!!
    siku zote huwa nawwambia kuwa siasa ni mchezo mchafu. ukiingia kichwakichwa umeumia. CHADEMA waliapa kuwa nafasi ya umeya ni yao. wakaahidi nguvu ya umma kutumika hadi watu wakauawa. jamani tuwe makini na maneno ya wanasiasa. mtu akiitwa mwanasiasa kaa naye mbali. akikueleza jambo ongeza na akili za kwako. usikubali haraka. niliwahi kuandika kua kisheria, yule meya ni halali. nini kimebadilika leo hadi chadema wamuone anafaa. nini kilibadilika hadi chadema wamkatae kikwete na baadaye kumkubali!!!!!!?

    ccm na cuf waliungana znz, chadema wakasema kuwa cuf ni ccm b. hicho kilichofanyika arusha siyo kuungana! jamani jamani jamani wanasiasa muogopeni mungu. zitto kabwe anaendesha hammer ya mil 110. mbowe anaendesha vogue ya mil 80. leo hii baada ya zitto kupata anapiga vita posho za wabunge wapya na wachanga! mnajua hiyo hammer hela yake imetoka wapi? mnakumbuka kipindi zitto anatetea mitambo ya dowans inunuliwe na serikali? mnajua alipewa nini????????????/ maskini watanzania tunachezewa a\na politicians. wanaoandamana ni sisi walalahoi. wakubwa wanajuana wenyewe.

    hata ukiniamsha usingizini usiku wa manane nitakuambia kuwa mfumo wa chama kimoja ni bora sana. mnashindana humo humo chamani na maendeleo yanapatikana.

    ReplyDelete
  8. Mtu kama hujui siasa usichangie hoja, mafanikio hayaji bila kufuja jasho. Viva Chadema kazi mzuri, CCM wanafikiri wanaweza kutupeleka puta siku zote. Sasa wacheze ngoma, sisi tunamaliza mchezo 2015, No CCM!

    ReplyDelete
  9. hayoooooooo ya CUF Zanzibar tunayaona kwa CDM.Nini mliwacheka

    ReplyDelete
  10. Wewe unayesema mfumo wa chama kimoja ni mzuri nafikiri hujui hata unacho kisema.Siku zote maendeleo huwa yanakuwa mazuri kwa sababu ya ushindani kati ya vyama pinzani angalia hata marekani wao wameendelea na wana vyama viwili unafikiri wao ni wajinga.wangekuwa na chama kimoja basi na kusiwe na haja ya uchaguzi.Angalia hata makampuni ya simu tuliyonayo sasa yamesababisha hata ngarama za kupiga simu kuwa rahisi.sasa hivi kuna huduma za simu kila kona ya nchi.Hii ni tofauti sana na ilipokuwa na shirika la posta na simu pekeyake.

    ReplyDelete
  11. mbn china inaendelea tena kwa kasi na chama kimoja? mi nzdhan c waafrika bongo zetu mbovu tu, coz mi naamin ht mkiwa na chama kimoja chenye watu makini na wazalendo nchi itaenda fresh tu

    ReplyDelete
  12. Kilichofanywa na CHADEMA na CCM kinastahili pongezi.CHADEMA walikuwa na haki ya kupigania walichokipigani na hatimaye kukipata.Hivi wanajeshi wanapoenda vitani na kufa wakati viongozi wanaohamasisha vita ipiganwe ni wajinga?Hii ndio hali na haikwepeki ni lazima mtu amwage jasho au damu kwa neema ya mwingine.

    ReplyDelete
  13. Haya yule Askofu wa KKKT kimbelembele na aseme sasa. Amezoea kuunga mkono na kutafuta cheap popularity. Askofu umekaa miaka 30 madarakani huoni kwamba unatakiwa kuwa umestaafu au umekuwa CCM. KKKT mnatakiwa kujivua gamba

    ReplyDelete
  14. TUITISHE MDAHALO MWINGINE KATI YA CUF NA CHADEMA, TUJADILI KWA NINI WAMEKUBALI KUOLEWA WOTE. CHADEMA MMEKUWA KAMA MACHANGU DOA

    ReplyDelete
  15. Mwacheni Baba Askofu kwani kondoo wake wanamtambua naye awajua kondoowake mchungajimwema. Hao hawaondolewi na magazeti yote yanaongozwa na nguvu za Roho Mtakatifu.

    ReplyDelete