24 June 2011

Inter Milan yachemsha kwa Tevez

MILAN, Italia

INTER Milan imefikia ukingoni katika mbio zake za kumwinda, Carlos Tevez baada ya kushindwa mshahara wa pauni 150,000 anazotakiwa kulipwa mchezaji
huyo kwa wiki.

Desemba mwaka jana mshambuliaji huyo wa Manchester City, alichafua hali ya hewa  Eastlands baada ya kuwasilisha barua ya kutaka kuondoka ndani ya klabu hiyo, lakini baadaye akaondoa maombi hayo.

Mbali na maombi hayo, pia licha ya kuiongoza Manchester City kutwaa ubingwa wa kombe la  FA na likiwa la kwanza baada ya kipindi cha takribani miaka 35, Muargentina huyo amekuwa bado akihusishwa kuhamia mjini Milan kwa mkataba wa pauni milioni 40.

Hata hivyo kwa mujibu wa mtandao wa Tribalfootball, Mkurugenzi wa Michezo wa klabu hiyo, Marco Branca alisema jana kuwa mshahara anaoutaka Tevez ni mkubwa mno.

Akielezea hali hiyo, Branca alisema: "Tevez ni mchezaji mkubwa na mwenye uwezo mkubwa lakini hakuna jinsi. Mshahara wake ina maana upo nje ya uwezo.

"Soko kwa sasa ni la kichaa na vigumu kushindana," aliongeza kabla ya kusema kuwa hivi sasa wanajipanga na fedha zao kwa ajili ya kanuni mpya za matumizi ya fedha.

"Hatufanani kwa kiwango, kodi kuanzia katika maandalizi hadi siku ya mechi na England. Tutatafuta wachezaji chipukizi wenye vipaji ambao tutawaendeleza," alisema Mkurugenzi huyo.

No comments:

Post a Comment