BARCELONA, Hispania
KLABU ya Barcelona inajiandaa kusaka pauni milioni 50 ili kumnunua kiungo na nahodha wa Arsenal, Cesc Fabregas kwa kutaka kumuuza mshambuliaji wake
David Villa (29) kwa Chelsea na Manchester City.
Miamba hiyo ya Catalan, watalazimika kuuza baadhi ya wachezaji wake kwa ajili ya kuongeza fedha za ada ya Fabregas. Na Villa ada yake inaweza kuwa pauni milioni 40.
Mchezaji huyo aliyeisaidia Hispania, kutwaa ubingwa wa Dunia 2010 nchini Afrika Kusini alijiunga na Barcelona miezi 13 iliyopita kwa ada ya pauni milioni 35, akitokea Klabu ya Valencia na alifunga magoli 23 katika kikosi cha Pep Guardiola, msimu uliopita.
Guardiola yuko tayari kumwachia Villa, lakini anaweza kufanya hivyo kama anaweza kupata fedha zinazoweza kusaidia kumnunua Fabregas na kumwondoa Emirates.
"Wazi anataka kubakia na Villa, hasa kutokana na mchango alioutoa katika mwaka wake wa kwanza akiwa na Barca. Anamwona David kama mchezaji mkubwa kwa ajili ya kupata makombe zaidi msimu ujao.
"Lakini anajua kwamba anaweza kumtoa kafara kwa ajili ya kupata fedha za kusaini wachezaji wengine. Manchester City na Chelsea wanaweza kufurahia kumnunua Villa."
Barcelona inajitahidi kupunguza madeni yake. Akizungumzia kuhusu kupungua kwa madeni ya klabu hiyo Makamu Rais wa klabu alisema: "Deni limepungua kutoka pauni milioni 474 hadi milioni 429 na deni halisi kutoka pauni milioni 383 hadi pauni milioni 324.
"Tunataka kuamua kuhusu hatima yetu ya baadaye kwa kufanya hivyo, tunalazimika kupunguza deni kwa kiwango kinachokubalika."
No comments:
Post a Comment