*Ataka wabunge wanaozikataa waungwe mkono
*Mbowe azifananisha na wizi wa kutisha
Na Martha Fataely, Hai
ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kaskazini, Dkt. Martin Shao, ameunga mkono hoja ya
wanaotaka kufutwa kwa posho zisizokuwa za msingi kwa watumishi wote wa umma na wabunge kwa maslahi ya taifa.
Msimamo huo ulitolewa mjini hapa juzi ikiwa ni siku chache tangu Kambi ya Upinzani Bungeni iwasilishe mapendekezo ya kutaka posho zisizo za lazima kwa watumishi na wabunge ziondolewe kwa kuwa ni mzigo kwa taifa.
Asjkofu Shao alitangaza msimamo huo wakati wa mahafali ya 40 ya Chuo cha Uganga Machame kinachomilikiwa na kanisa hilo, ambapo wanafunzi 48 walihitimu masomo ya stashahada ya utabibu.
Alisema hoja hiyo ni ya msingi hasa kwa kuzingatia kuwa Tanzania ni nchi maskini, ambayo inahitaji uangalizi wa fedha, na siyo kila mmoja kuangalia maslahi yake binafsi.
"Taifa limekuwa likikumbwa na matukio ya wizi, ubadhirifu na ufisadi wa kutisha, hivyo wanapotokea watu wachache ambao wanaonekana kutafuta kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, sisi kama taifa tunapaswa kuwaunga mkono na kukemea pale inapobidi," alisema Askofu Shao na kuongeza kuwa;
"Nchi hii kuna uozo wa watu kuangalia maslahi yao, yaani wao kwanza, tabia hii twapaswa kuiepuka, kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali aangalie na ya wengine," alisema.
Kwa mujibu wa askofu huyo, baadhi ya watumishi wamekuwa wakilipwa posho ambazo zingeweza kusaidia kuboresha huduma za afya kwa kuwapa motisha wale wanaofanyakazi katika mazingira magumu ili wananchi wanaoishi katika maeneo hayo waweze kupata huduma bora.
Alisema ni vyema kwa serikali kuona umuhimu wa kubadili sera hizo ili kuwawezesha watumishi wake kuongezewa mishahara na kupata kipato kutokana na mishahara yao halali na siyo kujilundikia posho.
Askofu Shao alitoa mwito kwa serikali kuona umuhimu wa kuboresha huduma maeneo ya vijijini, hasa kwa upande wa sekta ya afya na kutilia mkazo utaratibu wa kuwapangia vituo vya kazi wataalamu kuanzia ngazi ya zahanati, vituo vya afya na hospitali
Alisema zaidi ya asilimia 80 ya wakazi nchini wanaishi vijijini na hukumbwa na tatizo la upungufu wa huduma hizo, lakini serikali imekuwa ikitoa asilimia 60 ya huduma hizo huku ikichangiwa na mashirika ya dini kwa asilimia 40.
Dk. Shao alisema kanisa limekuwa likijikita zaidi kutoa huduma hizo vijijini, hivyo serikali inapaswa kuunga mkono jitihada hizo kwa lengo kuwaondolea wananchi kero ya kutumia gharama kubwa kupata matibabu.
Awali, akizungumza wakati wa mahafali hayo, Mbunge wa Jimbo la Hai, Bw. Freeman Mbowe alielezea masikitiko yake juu ya taarifa mbalimbali zinazotolewa na vyombo vya habari zikipotosha ukweli wa suala la posho.
Bw. Mbowe alisema anashangazwa na vyombo vya habari kuripoti kuwa ugomvi wa posho ni miongoni mwa wabunge, jambo ambalo alisema siyo kweli, kwani wamekuwa wakipinga posho zisizokuwa na umuhimu kwa watumishi wa kada za manejimeti na wabunge.
Alisema kambi ya upinzani imekuwa ikipinga posho nyingi zinazotolewa au kuchukuliwa na baadhi ya watumishi wa kada za juu ambao kwa siku huweza kuandikiwa au kujiandikia posho zaidi ya mara tatu.
"Jamani nilichokuwa napinga ni hiki, unakuta mbunge analipwa posho ya kujikimu yaani malazi, chakula na mawasiliano sh. 80,000, hii hatuna ugomvi nayo, lakini akihudhuria bungeni hata kama anaumwa yaani hatakaa siku nzima, analipwa pesa ya kukaa sh. 70,000, jamani huu ni wizi wa kutisha," alisema Bw. Mbowe.
Alisema kwa upande wa menejimenti za utumishi wa umma, pia kuna posho zisizohesabika kwani kila mwezi hujikuta wanalipwa mshahara sh. milioni moja na posho sh. milioni tano.
"Watu ambao wamekuwa wakifaidi posho hizi ni wale mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi, wakuu wa idara lakini wale wafanyakazi wa kawaida wala hawapati chochote na ndiyo maana kunakuwa na tofauti kubwa kati ya walionacho na wale wasiokuwa nacho ilihali wote wanalipwa mshahara," alisema.
"Unakuta mtu haonekani ofisini, kazi yake ni kuvizia vikao vya posho, anaingia cha kwanza anasaini na kuondoka, vile vile kama ni ofisa elimu anakwenda kukagua miradi ya elimu analipwa posho na wakati huo ametumia gari la serikali lenye mafuta lakini pia mshahara upo pale pale," alisema.
Bw. Mbowe aliwataka Watanzania kuwaombea kwa kukataa posho kwani kuna hatari ya wao kutolewa roho, kwa kuwa wamegusa maslahi ya wakubwa zaidi. Hata hivyo alisema hawahofii hilo.
Alisema matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi ni makubwa. Alitoa mfano akisema wabunge wanapotaka kusafiri badala ya kutumia usafiri wenye nafuu kwa manufaa ya taifa, wanatumia gharama kubwa bila msingi.
"Kwa mfano, ukishakuwa mbunge tu ujue umeula, kwani kwenye ndege ukipanda unakaa First Class (daraja la kwanza) kwenda Marekani nauli yake ni dola 8,000 (sh milioni 12) wakati ndege hiyo hiyo, ina vipengele vya Business Class dola 5,000 (sh milioni 7.5) na Economy Class sh. milioni 1.8, haya ni matumizi mabaya," alisema.
Alisema kutokana na hali ya umaskini hapa nchini viongozi wanapaswa kuona umuhimu wa kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima ili kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wake.
Awali Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Machame, Dkt. Elisinya Masawe aliwashukuru washirika wa maendeleo wa hospitali hiyo kutoa shirika la Alegent Health la Marekani hususani mwakilishi wake, Bw. Robert Cassworn kwa moyo wa kujitolea kuisadia hospitali hiyo.
wala hatushangai ni walewale katumwa tu siasa za nn sasa makanisani mkiambiwa mvue majoho mnakuwa wakali kuna nn hasa kwenye siasa?pesa za sadaka haziwatoshi?mnatukata na mambo yenu lkn hatushangai hilo jina tu linatupa picha ya ukibaraka
ReplyDeleteSaid unaonekana kama vile wakati unaandika maoni yako ulikuwa unatoka kuamka,mawazo yako bado yameganda,sasa hapo askofu kuzungumzia hiyo hoja kuna siasa gani au kwa kuwa imeanzishwa na wanasiasa.cha msingi utambue tu kuwa hii si hoja ya siasa ni hoja inayogusa maisha yako na bibi yako kule kijijini yeyete bila kujali anashughulika na nini anapaswa kuzungumzia hili.na nikuambie tu kwamba mahubiri si kusoma biblia pekee ni pamoja na kutoa maonyo ili jamii au waumini waelekee katika njia nyoofu.Asante sana baba askofu endelea na kazi.Hussein Mbaruku.
ReplyDeleteMBOWE KAZA BUTI KWANI SISI WANYONGE TUNAUMIA SANA NCHI HII MATEGEMEO NA MATUMAINI YETU SISI WANYONGE YAKO MIKONONI MWA CHADEMA AT LEAST MNAONEKANA KUWAJALI WANYONGE KULIKO CCM INAYOJIDAI KUWAJALI WANYONGE WAKATI MATENDO YAO NI KINYUME KABISA NA MANENO YAO SASA NDIO TUNAJUA KWELI CCM SIYO CHAMA CHA WANYONGE TENA BAADA YA KUSIMAMA NA WANYONGE WA NCHI HII WAMEAMUA KUSIMAMIA MASLAHI YA WAKUBWA.
ReplyDeleteSafi sana, tumesema kama posho haifutwi majibu 2015. Jamani tunapenda CHADEMA, we acha tu! Asante baba askofu!
ReplyDeleteHuu ndugu Said ana mawazo finyu kabisa, hakuna suala lolote la udini hapo. Cha msingi ni hizo posho za vikao vya wakubwa hao ambazo hata mimi naunga mkono zifutwe kwani ni ubadhirifu mkubwa wa fedha za serikali.Siku hizi siasa imekuwa ni biashara kubwa, mtu anakuwa mbunge kwa muda wa miaka mitano anakuwa tajiri kwa ajili ya posho na marupurupu mengine pasipo kuwasaidia wananchi.
ReplyDeleteAskofu kasema kweli, lakini kayaona leo?
ReplyDeleteHao maaskofu wanaingiza vitu binafsi kwa misamaha ya kodi, mwaka jana wakaja juu walipotaka kufutiwa misamaha hiyo, tusaidiane.
Askofu wa KKKT IRINGA anatuhumiwa kwa UFISADI na mambo kibao, lakini mkali hataki hata kusikia wenzake walipomwendea kumhoji.
Mbowe ametafuna hela za vikao kipindi cha miaka mitano wala hakusema, leo hii anajidai ana uchungu. OMARI SAIDI
Jamani ndugu zangu Watanzania inapotokea utetezi wa chochote kinachugusa wananchi walio wengi tuache ushamba wa kuingiza kauli za udini. Kwani suala hilo litakapopata muafaka ni watanzania wote watahusika bila kujali mkristo wala mwislamu. Sasa kama Askofu ameunga mkono wabunge wanaotetea posho kufutwa kuna ubaya gani? Hizo fedha zikiingizwa kwenye miradi ya maendeleo ni faida ya wote. Na hata wabunge wanaotetea hoja hiyo ya posho si wakristo tu. Hoja hiyo ilianzishwa na Zitto Zuberi Kabwe Mbunge wa Kigoma huyu tunamjua ni mwislamu safi. Kwanini waislamu (wachache sio wote)wanachukia sana wakristo? Sisi wote ni watanzania tunamwamini Mwenyenzi Mungu huyo huyo. Tuache jamani tuyakuza sana haya masuala ya udini kwani hatutafika popote. Sisi wote ni kitu kimoja.
ReplyDeleteSaid inaonekana wewe ni moja kati ya wabunge wa jamhuri ya muungano wa TANZANIA(CCM) wanao ng'ang'ania posho AU elimu yako ni ya darasa la saba. Binafsi sioni sababu ya watumishi wa umma kupewa posho zisizo za msingi na ingali mitaani umasikini na tabu nyingi dhidi ya raia wa tanzania vinanuka. kwa nini hizo pesa serikali isitumie kwenye mambo ya msingi kwa ajili ya maslahi ya watanzania wote.Nakushukuru sana ASKOFU DR SHAO KWA KUJUA NA KUTAMBUA HILO KWAN NI WACHACHE SANA WENYE MOYO KAMA HUO. CHADEMA KAZA BOOT TUPO NYUMA YENU TUNAKUJA TUMECHOKA NA CCM
ReplyDeleteMaasakofu kuweni na agenda yenu msingoje kuunga mkono. Lakini nyie wenyewe ni mamilionea wenye majumba na magari ya kifahari wakati waumini wenu ni waenda kwa miguu isiyo na viatu kuja kanisani mwenu. Na zaidi hebu jiulizeni mbona wengi wenu hata katiba zenu mnazipindisha umri wa kustaafu ili mkae madarakani. Shao amekuwa namba moja au namba mbili mwenye dayosisi yake miaka 34 sasa. MMMhhhh. Ajenda ya kwanza huko makanisana ondoeni posho mnazopeana, pili anaglieni katiba za dayosisis zenu zinahitaji kukarabatiwa na mwiso ondoa boriti jichoni kwako kabla ya kuondoa kibanzi cha mwingine baba askofu
ReplyDeleteKweli bwana maaskofu wetu hawana agenda zaidi ya kujificha nyuma ya vyama vya siasa. Juzi juzi walikuwa wapiga debe la CCM (wongo baba Askofu) saa hizi wako Chadema. Ni mamilionea wenye majumba makubwa na ya kifahari na viti maalumu ( na vyumba maalumu vya kulala!!!) kwenye hoteli zao na safari na posho za ulaya haziishi. Haya baba askofu mika 35 madaraka ya juu na mwenzako huko Arusha nasikia ana miaka 4o0 ya uaskofu siku hizi analala kanisani kwenye ibada anakoroma
ReplyDeleteJAMANI JAMANI JAMANI!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteNchi inaelekea pabaya. tukatae tukubali viongozi wetu maaskofu wanatuchanganya sana. serikali ktk bajeti ya mwaka jana ilifuta misamaha ya kodi kwa mashirika ya dini isipokua kwa vyombo vya ibada tu. kwa mfano vipaza sauti, nguo na misaada ya chakula. sababu kuu ni kwamba misamaha hiyo inatumiwa vibaya kwa wafanyabiashara uingiza biashara zao kupitia mgongo wa dini. serikali inakosa karibu bilioni 55 kila mwaka kwa misamaha ya dini. maaskofu walikuja juu. sasa hivi wamedandia la posho za wafanyakazi. AMA KWELI MKUKI KWA BINADAMU .......
UZALENDO UKO WAPI!!!!!!!!!!!
Sokoine's cousin....
ReplyDeleteNishawaambia ukiona mitoto fulani haina tabia nzuri (kukosa maadili mema) ujue hata mzazi nae yupo hivyo hivyoo!!
kwani nani ni mzazi wenu wa tanzania hivi sasa??????
Acheni upumbavu watanzania...!!!! mtakuwa wajinga maisha yote!!!
Watu kama SAID wanaangalia kasema nani na wala si kasema nini
ReplyDeleteMashirika ya dini yanachangia kiasi kikubwa kwenye huduma za jamii, msamaha wa kodi ni haki yao. Ni jukumu la vyombo vya dola (PCM,POLICE MHAKAMA n.k) kubaini wanaotumia msamaha kwa faida binafsi.
Omari saidi anasema Mbowe katafuna posho miaka 5. Si bora Mbowe kuliko CCM ambao wametafuna posho miaka 40 na bado wanang'aka?
Hivi, viongozi wa dini wanapokemea ualifu kama WIZI, KUUA nk inamaana wanakuwa wanaingilia kazi ya POLISI ama MAHAKAMA. Nini wajibu wao kwa jamii? Mbona wanapotoa huduma za ELIMU ama AFYA hamsemi imeingilia kazi za watu? Watanzania imefika wakati sasa tuondoe ushabiki wa kiitikadi ama kidini. Ni vema tukawa na mtazamo chanya wenye kutuunganisha na kutuletea maendeleo kwa umoja wetu.
ReplyDeleteAskofu wa KKKT tunajua siri zenu na utajiri wenu na maposho mnayolipana safri za ulaya haziishi
ReplyDelete