Na Zahoro Mlanzi
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, leo inatarajia kuipa Yanga zawadi ya fedha sh. milioni 42 baada ya kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania
Bara huku.
Vodacom pia itatoa zawadi nyingine mbalimbali zikiwemo timu za Simba ambayo itapewa sh. milioni 17 baada ya kushika nafasi ya pili na Azam sh. milioni 11 kutokana na kushika nafasi ya tatu katika ligi hiyo.
Zawadi hiyo ni sehemu ya udhamani wa Vodacom Tanzania katika ligi hiyo inayoratibiwa na kusimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Meneja Udhamini na Matukio wa kampuni hiyo, Rukia Mtingwa ilieleza kuwa makabidhaino hayo yatafanyika kwenye hafla maalumu ya chakula cha mchana katika hoteli ya Paradise.
Alisema wana furaha kuona kwamba vipengele vya udhamini kikiwemo hicho muhimu cha zawadi ya fedha taslimu kinatekelezwa, hivyo kutoa ari zaidi ya ushindani wakati ligi inapochezwa.
“Lengo la Vodacom ni kuona soka ikipiga hatua zaidi na hiyo ni pamoja na kuwa na ligi yenye zawadi zinazochochea ushindani na kesho (leo), Yanga itakabidhiwa fedha zake kutokana na kazi waliyoifanya wakati wa ligi hadi kuwa bingwa,” Alisema Rukia.
Alisema mgeni rasmi katika hafla hiyo atakuwa Waziri wa Habari, Vijana na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi ambapo pia timu zingine za Simba na Yanga ambazo zilishika nafasi ya pili na ya tatu, kila moja itakabidhiwa zawadi zake.
Rukia alisema zawadi hizo pia zinawahusu pia wachezaji walionga’ra kwenye msimu huo akiwemo mfungaji bora sh. milioni 3.1, kipa bora sh. milioni 2.6, mwamuzi bora, kocha bora sh. milioni 3.1 na timu yenye nidhamu sh. milioni 6.2. Fedha hizo za zawadi zinafikia sh. milioni 90.8
Aliongeza kwamba washindi wote, hata wachezaji mmoja mmoja watarajie mabadiliko makubwa katika zawadi hususani kiwango cha fedha kwa kuwa zimeongezeka tofauti na msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment