01 May 2011

Wafungwa miaka 600 kwa kughushi nyaraka

Na  Said Hauni, Lindi

MAHAKAMA ya Mkoa wa Lindi, imewahukumu watumishi wawili kati ya 12 wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, akiwemo aliyekuwa Ofisa Elimu wa halmashauri hiyo
Bw. Shabani Kilonzo, kifungo cha jumla ya miaka 600 jela kila mmoja,baada ya kupatikana na hatia ya makosa 40 kati ya
144 waliyokuwa wameshtakiwa.

Hukumu hiyo imetolewa juzi, baada ya mahakama hiyo kuridhishwa
na ushahidi uliokuwa umetolewa na upande wa mashtaka dhidi ya kesi hiyo.

Waliohukumiwa ni Mpamoja na Ofisa Elimu huyo ni Karani wa Fedha, Bw. Rashidi Kumpita,Muhasibu Msaidizi. Bw. Exavery Julius

Baada ya kutiwa hatiani washtakiwa waliulizwa kama wana sababu za msingi, ili wasipewe adhabu kali kutokana na makosa yanayowakabili, ambapo kila mmoja kwa wakati wake aliomba apunguziwe adhabu, kwa kuwa ni wakosaji wa mara ya kwanza,wanafamilia zinazowategemea wakiwemo wake,wazazi na watoto ambao baadhi yao wanasoma, na hivyo wanahitaji huduma zao.

Mara baada ya utetezi huo, Hakimu Dustani Ndunguru alimuuliza Mwendesha Mashtaka Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Louis Taisamo kama anakumbukumbu ya makosa ya zamani kwa washtakiwa, ambao alijibu hana,lakini aliomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kwa washtakiwa ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia ya aina hiyo.

Pia Taisamo aliiambia mahakama hiyo kuwa kitendo kilichofanywa na washtakiwa hao,kwani fedha walizoziiba ni jasho la wavuja jasho, wamevuruga mipango kazi ya elimu na kusababisha kuporomoka kwa elimu katika halmashauri hiyo.

Alisema fedha walizoziiba pia ni miongoni mwa malipo ya watumishi wa
Idara hiyo ya elimu, hali ambayo ilishusha morali kwa walimu kufanya kazi za uwajibikaji.

Naye, Hakimu Ndunguru akitoa hukumu katika kesi hiyo namba 148/2003,
iliyochukua zaidi ya saa tatu, alisema amesikia vilio vya pande zote
mbili,hivyo kila kosa moja kati ya hayo 40 aliwahukumu kifungo cha miaka mitano jela,na kufanya washtakiwa hao kuhukumiwa jumla ya kifungo cha miaka 600.

Hakimu Ndunguru amewafunga washtakiwa hao chini ya vifungu 384 kinachohusu kula nja,333,335 na 337 kugushi nyaraka za Serikali,265 na 270 wizi wa fedha za umma ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Kutokana na adhabu zote kwenda kwa pamoja, washitakiwa hao watatumikia kifungo cha miaka mitano jela kwa kila mmoja.

Aidha, mahakama hiyo imewaachia huru washitakiwa tisa,baada ya upande wa mashtaka kushindwa kutoa ushahidi ambao ungesaidia kuwatia hatiani.

Walioachiwa ni Bw. Rashidi Mbegumoja, Bw. Andrew  Nakajumo, Bibie Nambuta, Sophia Ummy, Yumvua Mhehe, Mohamedi Ausi, Fatuma Thabiti
Mkwama, Ahamadi  Kondo na Somoe Mwalimu.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka mrakibu msaidizi wa Polisi kuwa washtakiwa hao wote katika kipindi cha mwaka 2002, walikula njama, kugushi nyaraka za serikali za malipo hewa, wakiwa watumishi na hivyo kuiba zaidi ya sh.miloni 200 na kuisababishia hasara serikali.

Wakizungumza nje ya viwanja vya mahakama hiyo, baadhi ya washitakiwa walioachiwa huru, Rashidi Mbegumoja na Ahamadi S.Kondo walisema kimsingi wanamshukuru mwenyezimungu pamoja na Hakimu kwa kuwawezesha kuponyoka katika mdomo wa Simba (kifungo cha kwenda jela).

No comments:

Post a Comment