Na Moses Mabula, Tabora
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kwamba kitendo cha Sekretarieti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujivua Gamba kimeleta heshima ndani
chama hicho.
Alisema kuwa kitendo hicho kimerudisha imani na heshima kubwa ndani ya chama hicho, na wananchi kwa ujumla hivyo wapenzi na wanachama wa CCM wakipe kura za kutosha katika Uchaguzi Mkuu 2015.
Dkt. Mwakyembe aliyasema hayo wakati akihubia wananchi
mjini Tabora ambapo alisema kuwa kumekuwepo na maneno mengi kuhusu kujivua gamba kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho taifa.
Alisema kuwa kitendo hicho kinafaa kuigwa na watu wengine ili kuimarisha uhai wa chama.
"Kitendo cha kujivua gamba hakina maana kwamba viongozi waliojivua ni wachafu hapana bali ni utaratibu wa kukijenga chama msije mkasema hao wote waliojivua walikuwa na makosa ndani ya chama ni watu wasafi na waadilifu.
"Nawashangaa sana hawa wapinzani wanapiga kelele nyingi kuwa eti kujivua gamba ni kuvua uchafu nawaomba wasiigilie ni bora wakae kimya wasiingilie mambo yasiowahusu" alisema Dkt. Mwakyembe.
Kuhusu ujenzi wa barabara hapa nchini Dkt Mwakyembe alisema kuwa Serikali imejipanga vilivyo kuhakikisha kwamba barabara zote ambazo zimo katika mpango kujengwa, kazi hiyo inaanza mara moja ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi.
Alisema kuwa serikali kuanzia sasa itakuwa makini kwa wakandarasi wazembe na ambao kazi zao huwa zinafanyika kwa kusuasua ili kama wakibainika kufanya hivyo wahusika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kuhusu uimara wa barabara zinazojengwa chini ya alikiri kuwepo kwa
hali hiyo na kuwataka Wakala wa Barabara nchini (TANAROADS) kuwachukulia hatua kali, bila kuwaonea haya wakandarasi wazembe.
"Ninatoa maagizo kwa Mameja wote wa TANROAD hapa nchini wakaangeni wakandarasi wa hali hiyo kwani lwawama hizo zinaelekezwa kwetu na sio wao.
Hata hivyo aliwataka wananchi waliojenga ndani ya Hifadhi ya Barabara umbali wa mita 22.5 kubomoa haraka wenyewe lasivyo nyumba hizo zitabomolewa na serikali kwa nguvu bila kujali sura ya mtu wala cheo chake.
No comments:
Post a Comment