MADRID, Hispania
MSHAMBULIAJI Real Madrid, Cristiano Ronaldo juzi ametoa mchango kwa wachezaji wenzake kwa kuvunja rekodi ya ufungaji magoli katika La Liga.Nyoya huyo
kutoka Ureno, alifunga magoli mawili na kufanya afungwe jumla ya mabao 40 katika ligi ya msimu huu, wakati ambapo timu yake ilishinda mabao 8-1 dhidi ya timu iliyoshuka daraja ya Almeria.
Ronaldo ameipita rekodi ya mabao 38, iliyowekwa na Hugo Sanchez (1989/90) na Telmo Zarra (1950/51).
"Sababu yangu kubwa ya kutaka kufunga magoli mengi ni kwamba mimi na wachezaji wenzangu tunaelewana sana," alisema Ronaldo mwenye umri wa miaka 26.
"Ninaelewana na wachezaji wenzangu na wanaelewana na mimi. Nisingeweza kufunga magoli 40 katika La Liga bila ya wao."
Hakuna mchezaji aliyewahi kutwaa Pichichi, tangu walivyofanya hivyo, Sanchez aliyeshnda mfululizo kuanzia mwaka 1984/85 hadi 1987/88.
Ronaldo alisema amefurahishwa kuona timu yake ikimaliza ligi kwa kupata ushindi mnene.
"Tumefurahi kumaliza msimu huu kwa mtindo huu. Si kitu rahisi kufunga magoli 102, kwa hiyo ninawavulia kofia wachezaji wenzangu," alisema.
"Kocha alikuwa akitaka kumaliza msimu kwa magoli mengi, ili kuanza mwingine kwa malengo na tulifanya hivyo."
"Itakuwa ngumu kufunga magoli mengi kwa mara nyingine, lakini hakuna kisichowezekana na nitafanya kazi tena hivyo."
Kocha msaidizi, Aitor Karanka alimpongeza Ronaldo kutokana na uchezaji wake msimu huu.
"Idadi ya Ronaldo inashutua. Ana kipaji ni imara na ana malengo. Amevunja rekodi kwa kuwa ni mchezaji wa kusisimua," alisema.
No comments:
Post a Comment