*Polisi wamkamata, wamwachia huru
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
MKUU wa Polisi wa Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Onesmo Lianga ameshikiliwa na polisi mkoani Morogoro kwa muda na baadaye kuachiwa kwa
tuhuma za kumpiga risasi sehemu ya makalio mwalimu wa kikundi cha sanaa cha Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Dadie Kitururu (42).
Ndugu wa karibu na marafiki wa Bw. Kitururu alipigwa risasi Mei 11, mwaka huu majira ya jioni katika eneo la Forest wakati akiwa njiani kurejea nyumbani kwake, huku wakishangaa kwa nini polisi amtwange mtuhumiwa risasi badala ya kumtia mbaroni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Bi. Adolphina Chialo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, akisema kuwa siku ya tukio majira ya jioni Bw. Kitururu akiendesha gari alimgonga mpanda baiskeli Salumu Chiga (58), mfanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro mkazi wa Kichangani karibu na ofisi za Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Kilakala na kukimbia.
Alisema kuwa OCD huyo ambaye alikuwa nyuma ya Bw. Kitururu aliyekuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T 320 ANQ Suzuki Samurai, naye akiwa na gari lenye namba T 630 BFZ aina ya Rav 4 alimkimbiza Kitururu hadi eneo hilo la Forest.
Kwa mujibu wa RPC, baada ya OCD kuona Kitururu anakimbia zaidi, alifyatua risasi kwa bastola yenye namba PA06897 aina ya Chinese na kupasua taili la mbele na risasi ikapenya hadi kumfikia Kitururu kwenye makalio.
Kamanda Chialo alisema, baada ya tukio hilo OCD alimkamata mtuhumiwa huyo na kumfikisha katika Kituo Kikuu cha Polisi mkoani Morogoro na kuwekwa rumande na baadaye polisi waligundua kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na majeraha baada ya kuona akivuja damu, ndipo alipopelekwa hospitali kwa uchunguzi zaidi.
"Baada ya kufikishwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro mtuhumiwa huyo alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kutokana na hali yake kuwa mbaya na aligundulika kuwa na kipande cha risasi katika makalio na hivyo kupatiwa matibabu," alisema.
Baada ya kugundua hivyo, ndipo polisi walipoamua kumshikilia OCD huyo kwa kwa mahojiano juu ya tukio hilo na kubaini kuwa alipiga tairi risasi likapenya na kumfikia Kitururu.
haingii akilini risasi ipige taili la mbele halafu ipenye hadi matakoni! hapa naona kuna tatizo la taarifa za kipolisi kwa kuwa mtuhumiwa ni mwenzao. Pili utoaji taarifa wa magazeti usiozingatia taaluma ya maelezo sahihi ya pande mbili.
ReplyDeleteuandishi gani huu!!!!!!!!!!! risasi ipige tairi la mbele mpaka matakoni kwa mtu!!! na wewe mwandishi ukabeba habari jinsi ilivo ukatuletea sisi,ulipaswa uulize sio kuandika andika tu.ndio maana hao makamanda wanawadharau kwa sababu wanajua watawaambia vyovyote na nyie mnakurupuka kwenda kuandika badala ya kuhoji ilikuwaje,hivi wewe mwandishi inakuingia akilini kweli?? au unaandika ili ulipwer mshahara tu??
ReplyDeleteHuyo OCD asidhani alienda shule peke yake naye ashikiwe na police wenzake apelekwe mahakamani kwa kumlemaza huyo mwananchi. Kazi yao hao wenye risasi ndio hiyo hivi kweli upige tairi na risasi ije hadi katika makalio ya huyo mwananchi kweli inaingia akilini. Wananchi tumeenda shule kuliko hata huyo OCD, tena ajivue gamba apelekwe mahakamani, asidhani kwa vile ni OCD aogopwe sheria ichukuwe mkondo wake tena amtibu aliyeumia hadi apone makalio yake, mmezidi kwa vile eti mnazo silaha za kuwamaliza wananchi wasio na hatia, kwa nini usimkamate na kumpeleka kituoni sheria ichukuwe mkono wake? IGP Mwema hebu soma taarifa hizo mzifanyie kazi huyo OCD wenu ajivue gamba hafai, anaweza kuua halafu mseme hakukusudia tunawajua tabia hizo hazifai fuateni sheria na HAKI.
ReplyDeletehaiingii akilini kabisa, hata mkidanganya kivipi bado haiji, maana mmezoe kudanganya kila kukicha. huyo anatakiwa kumtibu mwenzake na kuhudumia familia yake hadi hapo atakapopona maana mnawaonea sana raia wasio na hatia.
ReplyDeletetutajalipiza kisasi si tunakaa nao mtaani hawa?
ReplyDeletePolisi wa nnchi ya Tanzania ni wahatari hawafai hata kwa kuwa kuiga ni balaa, wauwaji na hawana tena mvuuto. wanauwa bila kujali kwani wanajua mtetezi wao yupo, wanauwa nakisha wanapandishwa vyeo. kikwete utatumaliza duuuuuuuuuuuuuuuuuuu
ReplyDeleteAjabu kweli. Eti polisi walimpeleka hosp baada ya kuona anavuja damu. Kweli risasi ya matako unaweza ukaenda polisi ukiwa kimya bila hata kugugumia kwa maumivu?
ReplyDeleteNapata shida na maelezo ya kusuka ya polisi lakini napata shida zaidi na mwandishi aliyeibeba taarifa bila hata kuhoji mambo ya msingi ambayo yamepindwa na hayaingii akilini
WATANZANIA HAO. RISASI MWENDO MDUNDO. SAWA WAKUBWA
ReplyDeleteMIE HATA MWANDISHI NAMLAUMU,JINSI ALIVYOIANDIKA HABARI SI RAHISI KWA MSOMAJI KULIELEWA TUKIO LENYEWE. INAWEZEKANA MWANDISHI HAKUFANYA UCHUNGUZI WA KUTOSHA AU HABARI PIA IMETOLEWA NA POLISI ILIMRADI TU KUTOLEWA NA KUTAFUTA SABABU YA MTU KUUMIZWA KWA KUPIGWA RISASI. ALITAKIWA KUIANDIKA ILI KUMRAHISISHIA MSOMAJI KUTOA MAAMUZI
ReplyDeleteKweli kama Kamanda wa Polisi amenukuliwa kwa usahihi taarifa ina mapungufu makubwa na inaonekana kuelemea upande mmoja. Kwanza sio risasi moja iliyopigwa kwani magari mengi tairi iko mbele zaidi ya dereva,na zaidi, risasi imebaki kwenye jeraha wakati tairi imedaiwa kupasuliwa na risasi. Kosa lililotokea ni la usalama barabarani, gari lina namba na sheria inasema mhalifu anaweza kukamatwa kwa mazingira yale uwezekano wa kumkamata dereva baadae ulikuwa mkubwa lakini kwa kitenda cha huyo OCD ni kosa la jinai la kuharibu mali na kujeruhi. Busara haikutumika,kwani alipaswa kuchukua namba za gari, kujulisha polisi na kumpeleka majeruhi hospiali. Matumizi mabaya ya silaha yamezidi kwani ingeweza kupitiliza na kuua au kujeruhi wasiohusika.
ReplyDeleteDaima hapo zamani tulipokuwa tukipiga shabaha kutumia bastola au hata rifle ndogo tulikuwa tukiweka matayiri ya gari nyuma ya target ili kuzuwia risasi zisiende mbele zaidi.
ReplyDeleteMWISHO WENU MAPOLISI NI 2015 MTAKOMA, WAULIZENI WENZENU WA KENYA.
ReplyDeleteKwanza nasikitika mwandishi kurahisisha hivyo hii taarifa. Kuna wahusika watatu hapa, aliyegongwa anayejiita ocd na huyu aliyegonga. Kwa kuanzia mwandishi ulipaswa kukimbia kufahamu maelezo juu ya hawa ndiyo iwe taarifa, hii bado sana. Kamanda wa polisi mimi sitegemei kwa cheo chako ujikanyage kiasi hicho kwenye maelezo yako, unadhalilisha taaluma hizi. Tatu, Rais wa jamhuri ya muungano, msiwe mnaruhusu ujinga huu kutokea ndio unaowapunguzia credits katika utawala, watu sasa hivi wanasikiliza wanafikiria vizuri. Hata ukadanganya kiasi unavyoweza ukasema sheria imesema kama ilivyosema kwa marehemu mkuu wa mkoa wa Tabora baada ya kumuua kwa risasi dereva, kinachopandwa kwa wananchi huwa si sheria unayoitaja, mnazidi kuwafanya wananchi wahifadhi maovu juu ya maovu ambayo yamekuwa yanatetewa eti sheria imesema(hakuna palipotaja sheria kwenye tukio hili lakini nafahamu mwisho wake ni sheria ya kumbeba ocd). Mwisho wa siku wananchi wakihifadhi vya kutosha huwa wanakosa nafasi zaidi ya kuyatunza, huwa wanatafuta pa kuyatolea na ndipo sheria huwa haina nguvu tena. Ni angalizo tu.
ReplyDeletepamoja na polisi kuwa hawkutoa taarifa vizuri kwa kuficha ukweli,pia mwandishi huyo ni kilaza/kimeo mwandishi ni mdadidisi na mchokoza mada kwanza huwa anatakiwa kujua ukweli afu anaenda kukonfem kwa pande zote, wewe nani alikudanganya utapew ukweli bila kuutafuta,hata mimi na kapisto kangu najua kutumia vzr,hiyo ni ujanja ujanja tuu,hakuna na haiwezekani risasi iingie kwene tairi then itoboe bati afu iingie kwene makalio,NEVER ! Najua uwezo wa pistol si mkubwa kiasi hicho,namaanisha effective range/malengo sahihi na penetration,uwezo wa kutoboa kitu! any way kuna makosa hapo wasinifanye nianze toa somo kwene net,kwani tunaelewa vyakutosha ,polisi nao wajivue gamba kwani kuna baadhi wanwachafua sana kwa mengi.Wakati wao ndio kimbilio letu huku wakija na sera tamu ya polisi jamii !
ReplyDeleteasanteni sana polisi wa tz na viongozi waliopo madarakani huo ndio utawala bora alafu mnataka polisi jamii kwa mtindo huu sidhani naiombea amani tanzania yangu
ReplyDeletemnatafuta matatizo na jamii tarime aijaisha ya zombe mmechakachua kweli baba jk wewe ni bubu kemea auuchunguzi ufanywe ili ukiondoka madarakani uondoke kwa heshima na kukumbukwa tujivue gamba honi mnao mlaumu mwandishi mnakosea yeye anapewa taarifa rasmi na msemaji wa polisi huyo ndo wakulaumiwa
ReplyDeletePolisi wetu mmezidi uoga na hivyo mkijikuta kutumia nguvu kupita kiasi kwa kila tukio. Shame on you!!!
ReplyDelete1. Bastola ilikuwa ni ya serikali au yake binafsi.
ReplyDelete2. Kama ni yake binafsi ameitumiaje kwenye trafic case.
3. Kama aliweza kuifukuza gari ya mtuhumiwa , je hakuweza kushika/kuandika namba na kuzipeleka kituoni ili gari hiyo itafutwe kwa utaratibu bora zaidi na mtuhumiwa/dreva kuchukuliwa hatua?
4. Je OCD ambaye si wa eneo fulani anawezaje kufanya kazi eneo jingine bila ya mawasiliano na OCD wa eneo husika?
5. Huyu kwa sasa ana kesi ya kujeruhi kwa kutumia silaha, je amesimamishwa kazi hadi mwisho wa kesi?
OCD anauelewa mkubwa na namna ya kumkamata mhalifu, ingekuwa huo ndio utaratibu unaotumika wananchi wangapi? ambao wengukuwa vilema na wengine kupoteza maisha, kunasababu gani gari kuwa na namba?, mbona hatupati maelezo ya pande zote, anatetewa yeye tu, huyo mwendesha baiskeli aliumia au vyanzo vinatafutwa
ReplyDelete