*Tundu Lisu akamatwa, afikishwa kortini Tarime
*CHADEMA walalamikia maiti kutelekezwa njiani
Hellena Magabe, Tarime na Tumaini makene, Dar
JESHI la Polisi limewakamata na kuwafikisha mahakamani Mbunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na
maofisa wengine wa chama hicho baada ya kudaiwa kufanya mkusanyiko usio halali na kuzuia watu kuzika ndugu zao.
Sambamba na hatua huyo jeshi hilo limedaiwa kuingia mochari ya Hospitali ya Wilaya ya Tarime na kuchukua kwa nguvu maiti nne za watu waliouawa na polisi hivi karibuni na kwenda kuzitelekeza maeneo mbalimbali ili kuzui mkusanyiko wa kuaga maiti hizo kwa pamoja, kwa kile wanachoeleza ni kuzuia uvunjifu wa amani
Bw. Lisu na wenzake wanadaiwa kukutwa katika Hosptali ya Wilaya ya mjini hapa wakilinda miili hiyo baada ya kusikia tetesi kuwa polisi walikuwa na mpango wa kuichukua na kuisafirisha kusikojulikana.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Bw. Casmil Kria alisema watuhumiwa wanakabiliwa na mashtaka matatu, yaliyosomwa mbele ya Hakimu wa Wilaya, Bw. Yusto Ruboroga.
Mashtaka hayo ni kuingia eneo la hospitali bila kibali, kufanya mkusanyiko usio halali na kuzuia watu kuchukua miili ya ndugu zao.
Watuhumiwa hao ambao wanadaiwa kukutwa eneo hilo saa 4:00 usiku baada ya kusomewa mashtaka na kuyakana, walirudishwa rumande kwa 'sababu zakiusalama', na kesho watafikishwa tena mahakamani kwa ajili ya kupewa dhamana, endapo miili ya waliuawa itakuwa imeshazikwa.
Walioshtakiwa ni Mbunge wa Singida Magharibi, Bw. Tundu Lissu (43), Bw. Mwita Mwikwabe (36), Bw. Stancelaus Nyembea (33), Anderson Deogratias (35), Bw. Andrew Andaru (63), Bw. Mwita Marwa (48) Bw. Bashiri Abdallah Seremani (35) pamoja na Ibrahimu Juma Kimi (27) ambaye ni dereva wa Bw. Lissu.
Wakati huo huo, waandishi wanne wa habari pamoja na Mbunge Viti Maalumu, Bi. Ester Matiko (CHADEMA) nao walishikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo Kidogo cha Nyamwaga na baadaye kuachiwa huru baada ya mahojiano.
Wandishi hao ni Bi. Beldina Nyakeke wa The Citizen, Anna Mroso(Nipashe), Bw. Anthony Mayunga (Mwananchi) pamoja na Mabere Makubi wa Chanel Ten ambao walikuwa kwenye msafara wa Bi. Matiko.
Waandishi wengine wa habari waliofika katika mahakama ya wilaya kufuatilia tukio hilo walizuiliwa kuingia na kutishiwa kupigwa
risasi na ofisa mmoja wa polisi.
Ofisa huyo ambaye hakufahamika jina aliwatimua waandishi hao, huku akiomba bunduki kutoka kwa askari mwenzake na kuiandaa
mithili ya kupambana na adui.
“Toka! Toka! Naombeni bunduki yangu hapa naona nyinyi hamjui
kufanya kazi, hatukuja kufanya mchezo hapa waondoe na wale watu upesi mahali hapa wasongee mbali huko hatutaki mtu hapa!” alisema.
Askari hao wakiwa wameziba njia huku ofisa huyo akiendelea kuelekeza bunduki yake kwa raia waliokuwa eneo hilo.
Katika tukio jingine, polisi juzi usiku lilichukua miili na watu waliouawa kwa ngunu kutoka hospitali na kuitelekeza vijijini huku wanandugu wakisijue licha ya kuwa walikuwa wameandaa majeneza yao tayari kwa kuweka miili hiyo, ambayo ingeagwa kwa pamoja chini ya usimamizi wa uongozi wa CHADEMA.
Kauli ya CHADEMA
CHADEMA kimesema kitawasaidia wananchi wa Tarime, waliojeruhiwa au kufiwa katika matukio mbalimbali ya Jeshi la Polisi kuua raia kwa tuhuma za kuvamia na kuiba mchanga katika Mgodi wa North Mara, kwa kufungua kesi mahakamani dhidi ya serikali.
Chama hicho kimesema kuwa hakitachoka wala kurudi nyuma katika kutetea haki za wananchi hususan katika kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinatumika kwa manufaa ya Watanzania wote, kwani hiyo ndiyo kazi ya chama cha siasa chochote duniani, kutumia makosa ya serikali iliyoko madarakani, kama fursa ya kutafuta uhalali kwa wananchi kukipatia kura za kuongoza dola.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, mmoja wa wanasheria wa CHADEMA na mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Bw. Mabere Marando, alisema "safari hii tunataka kuitia adabu serikali kutokana na makosa yake yenyewe."
"Wananchi wale wametuomba tuwasaidie kufungua kesi, nasi tumekubali, tumewaambia wakusanye ushahidi wa kutosha na aina ya ushahidi unaoweza kushinda kesi mahakamani...wote waliofiwa na waliojeruhiwa, wakusanye ushahidi wote, wajitokeze waje CHADEMA ambayo itawatetea kupitia mawakili wake.
"Hakuna chama cha siasa kinashindwa kutumia opportunity (fursa)pale serikali inapovurunda, katika hili serikali imevurunda... hatutachoka, hatutarudi nyuma...tutachukua hatua katika kutetea haki za Watanzania, hakuna binadamu anaruhusiwa kuua, kama ni mahakama pekee yenye mamlaka ya kusema huyu ni mwizi au jambazi," alisema Bw. Marando.
Akitoa madai dhidi ya polisi kuamua kuchukua miili ya marehemu kwa nguvu kutoka chumba cha kuhifadhia maiti juzi usiku, kukamatwa kwa wabunge wawili wa CHADEMA, waandishi wa habari na baadhi ya ndugu wa wafiwa kisha kutekelezwa barabarani kwa maiti ya Emmanuel Magige, Bw. Marando alisema 'Tarime hali ni tete mpaka sasa'.
"Mpaka dakika hii tunayoongea tunaambiwa wananchi wamejumuika pamoja na wafiwa wamechukua majeneza yaliyotakiwa kwenda kubebea maiti hospitalini sasa wanaandamana kwenda kudai maiti zao...wabunge wawili wa CHADEMA, Tundu Lissu na Easter Matiko wako ndani, baadhi ya ndugu wa wafiwa nao wamekamatwa pia wako ndani.
"Jana usiku wa takribani saa nne kasorobo magari mengi ya polisi yalivamia hospitalini polisi wakaingia mochwari hatujui kama waliomba ruksa kwa madaktari au la. Wakachukua maiti zote nne. Hata ndugu wa wafiwa hawakutaarifiwa juu ya mpango huo. Wakaitupia miili ile kama mawe au magunia ya mihongo ndani ya magari yao, bila heshima.
"Maiti mbili zilikuwa za Serengeti, mbili za Tarime, sasa wakati polisi wanaondoka, wananchi wakaanza kupigiana simu, hivyo walivyofika huko wananchi wakawa wanawazomea askari nao wakaamua kushusha maiti na kuzitupa, wakaondoka. Mpaka tunapozungumza sasa hivi maiti ya Emmanuel Magige bado iko barabarani.
"Jana (juzi) usiku Tarime magari ya polisi yalipita yakitangaza watu wasitoke nje, endapo mtu atatoka nje atapigwa risasi," alisema Bw. Marando.
Aliongeza kuwa chama hicho pamoja Jeshi la Polisi kupitia mazungumzo yake yeye na Kamishna wa Operesheni wa jeshi hilo, Bw. Paul Changoja, walikubaliana kuwa miili ya marehemu itachukuliwa kwa magari mpaka Uwanja wa Sabasaba kupewa heshima za mwisho hadharani, kisha kila wafiwa kwa msaada wa CHADEMA wangebeba maiti kwa ajili ya maziko mahali kunakohusika.
Alisema wameshangazwa na uamuzi wa jeshi hilo kubadili makubaliano hayo kwa taarifa za kiintelijensia, huku pia akilaani kukamatwa kwa waandishi wa habari wa magazeti ya The Citizen, Nipashe, Mwananchi na Channel Ten, akidai kuwa serikali inafanya makusudi kuzuia kupatikana kwa habari juu ya sakata linaloendelea Tarime, kuwafikia Watanzania wote.
Kwa upande wao, wajumbe wawili wa Kamati Kuu ya CHADEMA, ambao pia ni kati ya waasisi wa chama hicho, Mzee Edwin Mtei na Mzee Bob Makani, wameiasa serikali kuzingatia uhuru wa sheria katika kushughulikia sakata la mauaji ya Tarime na hata usimamizi wa rasilimali za Watanzania, ambacho ndicho chanzo cha mgogoro baina yao na Kampuni ya Barrick inayomiliki mgodi huo.
Jeshi la Polisi linatumiwa na CCM kwa malengo yake ya kisiasa. IGP wewe ni CCM na unamiliki kadi ya CCM ni obvious kwamba huwezi kutenda haki nakushauri ujiuzulu wadhifa wako kwani una mgongano wa kimaslahi.
ReplyDeleteCHADEMA HOYEEE aluta continua dont give up mpaka mchukue nchi kwa CCM imeshindwa kuongoza badala yake inatumia polisi kuua raia wema
Mungu ibariki TZ, tuepushe na ufilauni huu..hatutaki shida
ReplyDeletesiasa hazina mpango wafaidike wengine waumie wengine watanzania ujinga huu utaisha lini?mnavyojidanganya mnafikiri nani atawapa ahueni ya maisha kama si ww mwenyewe?mnasikitisha sana wabongo
ReplyDeletewezi nao wanapata watetezi wao. mwizi hawezi kumuacha mwizi mwenzie. Uchochezi huu wasifikiri wataingia ikulu kiulaini, waendelee kuwashawihi watu kufanya vurugu kama hizo za north Mara. CHADEMA washitakiwe kwa Uhalifu huu wanaoendelea kuufanya. Tumewachoka Mapema hatutaki Vurugu Tanzania yetu.
ReplyDeleteNi wazi kuwa Watanzania hawajui nini maana ya AMANI. Hivyo kigezo cha amani kisitumike kuhalalisha maovu ya chama tawala hasa pale kinapoamua kukandamiza kwa makusudi wananchi wake walio wema. Kamwe neno "amani" lisichanganywe kabisa na neno "demokrasia". Amani haiwezi kupatikana katika nchi ambayo wanachi wake ni fukara, hawana matumaini, hawana kesho, hawana mtetezi, hawana huduma muhimu za kijamii, wametengwa na dola na ambao nchi yao utawala wa sheria umewekwa tu katika makaratasi. Kusema tuna AMANI ni ubatili mtupu.
ReplyDeleteHii ndio shida ya POLICE wetu. Wanadhani kuwadhibiti wapinzani mara kwa mara tena wakati mwingine kwa mambo yasiyo na msingi kabisa ni kuwafurahisha watawala.
ReplyDeleteWanapenda kutumia visingizio vya usalama na kuepusha vurugu ili kutimiza amri za kisiasa.
Chadema acheni kusababisha matatizo kwa wananchi ili mfanikiwe mambo yenu.Mbona vyama vingine havifanyi kama hayo.Mnadai ccm imeshindwa,nyie mna uhakika mtaweza? Mwanafunzi gani anafaulu mtihani kabla ya kuufanya?
ReplyDeleteSerikali ya CCM ni chumvi iliyoharibika, je itiwe nini hata ikolee? haifai kitu ni kutupwa tu. Wananchi tushikamane tutashinda
ReplyDeleteCHADEMA huu ujinga mnaoufanya hauwezi kuwasaidia kamwe, msidhani watu ni wajinga kama nyinyi. mtawapata haohao wajinga wenzenu. Mbona hamzungumzii chamzo wala polisi walioumizwa? endeleeni kutetea wahalifu .
ReplyDeleteCHADEMA mtavuna mnachopanda , mnafikiri watanzania wote ni wavuta bangi?
ReplyDeleteTUNAJIPANGA, SIKU INAKUJA TUTAWASTUKIZA.PAA.HAMTAAMINI
ReplyDeleteNaapa hapa kwa mwenye kumbukumbu aandike hii MAISHA YAKIENDELEA KUWA HIVI MAKUNDI KAMA MUNGIKI YAPO MBIONI KUCHOMOZA NA NDIPO KARAHA YA MWENYE NACHO NA ASIENACHO ITAJIONESHA DHAHILI: Kwa wale wanaozidi kutetea na wengine kupinga u[NENO BAYA SANA] watakuja kujutia nafsi zao, maana tumeshawachoka u-CCM na u-CHADEMA wenu wakati huku roho za watu zinazidi teketea kama ndafu. Ee MOLA tunusuru hili baradhuri, Amen
ReplyDelete