25 May 2011

Nchi kumi kushiriki riadha Dar

Na Amina Athumani

NCHI kumi zimethibitisha kushiriki mashindano ya riadha ya Afrika Mashariki na Kati yatakayofanyika nchini Juni 3 mwaka huu katika Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.

nchi hizo ni Misri, Sudan, Eritrea, Djobout, Zambia, Rwanda, Kenya, Uganda, Zanzibar na wenyeji Tanzania.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu wa Chama cha riadha Tanzania (RT) Suleiman Nyambui, alisema nchi hizo ni miongoni mwa nchi zitakazoshiriki mashindano ya Mataifa ya Afrika.

"Tunategemea kupokea wanariadha wengi kutoka katika nchi hizo, lakini pia kwa upande wetu kama wenyeji tutakuwa na wanariadha wote waliopo katika timu ya taifa, hivyo tunategemea ushindani wa hali ya juu pia tutapata nafasi ya kuchagua timu yetu itakayoshiriki mashindano ya Afrika kupitia mashindano haya," alisema Nyambui.

Alisema timu ya Taifa inaendelea na mzoezi katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku baadhi ya wachezaji wengine wakiendelea na kujiandaa Jijini Arusha.

Mashindano kama hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam mwaka jana katika Uwanja huo wa Taifa na Zanzibar kuibuka washindi wa jumla.

No comments:

Post a Comment